Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Haaahaa 😆 ☺️ kuna siku Kuna ka brother kangu kana MWILI mdogo mdogo sikuwai kuonana nako tangia nikiwa mdogo.

Siku moja nikawa nimeenda kinyerezi nikamkuta kavaa jezi yake yupo na brother angu mmoja nikasalimia habari za leo kajamaa kakagoma kakasema nikape shikamoo tukalumbana nikakasalimia kwa shingo upande.

Baadae ndio brother mwingine AKAJA aka ni introduce kwake ni brother mkubwa na ana wadhifa kubwa tuu mpaka NIKAONA AIBU Ila Kuna watu Wana miili midogo midogo mpaka wanaweza kunyimwa kiti ugenini 🤓
Hata mimi kuna braza kwa mama mkubwa nae ana mwili kama huo,anapenda shikamoo balaa,sasa sisi tunamchukulia poa,ila anaitaka kwa nguvu zote

Haya maisha bwana wengine hawataki shikamoo na wengine wanaitaka basi ni shida tu kwakweli
 
Kuna kipindi niliamkia sana makinda huko kanda ya ziwa. Siku moja mama mmoja akasema kijana wangu nakuona unaamkia sana wadogo zako hata kama unataka kuoa usukumani usifanye hivyo. Nisilikia aibu sana tangu siku hiyo hadi leo salamu yangu kubwa ni habari.

Na nikikutana na mtu simuelewi naanza kwa kuchangamsha maongezi bila salam. Isitoshe wengi siku hizi hawaipendi.
😂😂😂
 
Shikamoo maana yake nakushika miguu, ndio maana kuna wengine hupinda goti wanapoamkia wakubwa. Na marhaba maana yake ahsante.
Sasa vijakazi walipokuwa wanaamkia mabwana zao ndio walikuwa wanapiga goti na kusema shikamoo. Then wakuu nao huitikia marhaba huku wanawagusa kwenye vichwa vyao
Aisee,sio poa kabisa hii sslamu
 
Mtaalamu sjui tunatofautiana mie niko kwenye forties lakini sina mvi hata moja nywele bado nyeusi tii. Ajabu kwenye ndevu ndio naona mvi tena ni kidevuni nazo si nyingi zipo kama mbili au tatu.

Itakuwa umerithi maana kuna watu wana miaka 30 kichwa chote mvi
Nitakuwa nimerithi expert wangu,kwa kawaida mara nyingi kidevu ndio huanza kupata mvi
 
Kipind nimetoka toka tu chuo nimanza kazi, mkurugenz wangu ambaye ndio mwenye kampuni alikua amenizid umri wa miaka 10 na siku pekee aliopata shkamoo yangu ni siku naingia kwenye interview. Baada ya hapo mpaka naondoka kazin sikiwah mpa shkamoo.

Ukiachana tu na wewe kuona uzito kuamkia, hata watu wazima ukitazama kwa makini utakuja kugundua kuwa hawapendelei sana kuamkiwa na vijana kuanzia rika flani , labda awe mzee may be
 
Sio kweli ,wanasalimia kwa kichaga , huko kwa wa Iraq karatu na babati ukivaa ukapendeza halafu sio mtu wa huko ndio unasalimiwa shkamoo na marika yote.
Kule kwa wairaq na hasa kwa wafugaji wote wanajua Shikamoo ni salamu ya Mwalimu na mtu mtu mgeni. Hivyo ukiwa mwalimu utakuwa unapokea Shikamoo za wanafunzi wa wazazi wao. Pia ukiwa siyi mtu wa kabila lao utakuwa shikamoo kwa sana.
 
Kule kwa wairaq na hasa kwa wafugaji wote wanajua Shikamoo ni salamu ya Mwalimu na mtu mtu mgeni. Hivyo ukiwa mwalimu utakuwa unapokea Shikamoo za wanafunzi wa wazazi wao. Pia ukiwa siyi mtu wa kabila lao utakuwa shikamoo kwa sana.
Yeah wewe unawajua vizuri mno
 
Na umri huo unasalimia watu shikamoo ili iweje? Aah wee mi nilishaacha labda wale wazee kabisa
Ukiwa mkubwa halafu ukose pesa , then upitwe na kitoto ambacho juzi juzi tu ulikiona kina jipupulia bila salamu ,ndio utajua mziki wake unakuaje.
 
Nyongeza: Mwisho wa hii salamu ni umri gani?? Coz marehemu baba at 65s alikuwa anamuamkia baba mkubwa mwenye 70s.

Ilikuwa inanishangaza lakini siku zinavyoenda naona kaka zangu bado shikamoo wanaitaka na usipoitoa kosa! As-salamu alaykum unaitoa na Shikamoo unatoa!
Hii salamu maadam mtu ni mkubwa kwako unatakiwa uitoe

Sisi nyumbani tulilazimishwa kuamkiana,huyo mdogo wangu wa kike alikuwa hani amkii,mama ndio akamwambia ebu mwamkie kaka yako,mwanzoni alikuwa anacheka akiniamkia ila now ameshazoea

Dada yangu nae nilikuwa simwamkii,kupitia shinikizo la bimkubwa basi namuamkia

Sisi wenyewe wala hatukujali ila bimkuwa ndio akashika bango
 
walimu tunasalimiwa mpaka na babu na bibi zetu shikamoo mwalimu unajshtukia ila unaitikia tu🤠🤠
 
Back
Top Bottom