Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Tatizo kubwa la kimaadili ni watawala kutembelea misururu ya maV8 huku wanafunzia wakiwa wanasomea vyumba vya vumbi, vijijini hawana mabomba ya maji na vijana wengi hawana ajira au wanaendesha bodaboda.
 
Vitabu vya dini ni muhimu sana, nyinyi wenyewe na watoto zenu wanyimeni vyote msiwanyime maadili mema, na hakuna pakuyapata maadii mema zaidi ya kwenye dini.
Watu wengi wanaojidai kuvijua vitabu vya dini wameifanyia vibaya sana nchi hii kwa ufujaji, ufisadi na dhuluma za kila aina kwa watu wengine.
 
Ujinga na ushamba ni huo wa kufuatilia nani kavaa nini. Mtu kuvaa nguo fupi au za kubana inakuathiri vipi wewe au watu waliomzunguka??
 
Sahihi
 
Wazazi wamelegeza kamba ya kuhakikisha waliowaleta duniani wanaenenda katika mstari ulionyooka. Malezi, na si ya kizazi hiki tu, kwani waliozaliwa nje ya ndoa wako miaka nenda, miaka rudi, tangu enzi na enzi. Lakini je, linapotokea hilo, hukemewa au kupongezwa?
Tukiacha uzazi wa hovyo, vipi wizi, rushwa, ubadhirifu, ambavyo kwa sasa serikali na wanaoiongoza, wanavipigia chapuo, na wao wala si watoto.
Tz inakoelekea, sijui ni muujiza gani utokee na kulikomboa hilo taifa. Uozo kila nyanja!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mbona nchi hii watu wake wengi wana dini ila rushwa na dhuluma za kisiasa zimejaa??
Kua na dini na kuishi kwa misingi ya dini ni vitu viwili tofauti,

Unaweza ukawa na dini ila ukawa hufuati misingi,nidhamu,matakwa ya dini yako,So hapo unakua kama vile huna dini tu,

Mfano,Dini inasema,usizini,usiue,usidhulumu mali ya watu,usiibe...ila wewe ukawa hufuati hayo,hapo wakulaumiwa ni wewe na sio dini yako.
 
Ulitaka nieneze chuki za upagani?


Kama wewe huna dini unataka wote tusiwe na dini? Kukosa dini ndiyo chanzo kikuuu cha ukosefu wa maadili.

Kama huna dini hayo maadili utajifunza kutokea wapi?
Wajinga kama hao usiwe unawajibu maana wanatupoteza kabisa na hii mada yako
 
Utadumishaje maadili wakati national cake wanakula wachache na wengi tunateseka tu.

Maisha yenyewe hayana usawa hayo maadili mema yanatoka wapi??
 

Maadili sikuhizi hayapo, ukiishi maisha mema, wanawake wanakuona mjinga tu.
Kuna watu ni wema ila mazingira yanawabadilisha.
 
Mmonyoko wa yanaenda sambamba na kuwa brainwashed. Kizazi cha kileo kimekuwa brainwashed na nyimbo za kuhamasisha ngono tena kinyume na maumbile. Na wasanii wanaoimba hizo nyimbo ndiyo wanao alikwa kwenye mahafla ya serikali.

Nilibahatika kukutana na msanii mmoja wa hip-hop, nikamuuliza kwanini hata serikali haiwapi mialiko wakati nyimbo zenu zimejaa "madini"

Akaniambia siku zote watawala wanapenda sana watu waliokuwa brainwashed ili iwe rahisi kuwatawala na kuwamanipulate.
 
Kwa hiyo unamaanisha maadili mabovu yanasababishwa na serikali?
 
Hapa si tunazungumza kuhusu maadili kiujumla, mi nimefanya specifications tu.
Labda niulize tena kivingine; "wanawake" wamehusika vipi na kuporomoka kwa maadili kiujumla?

Inawezekana una point nzuri, tulizana, shusha pumzi, kunywa maji, fikiri kidogo halafu ujibu kwa kina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…