Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozido miaka 40 watanielewa.
Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".
Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikiuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.
Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.
Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana na cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunayoyaona kuwa ni maadili mema.
Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.
My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi ndiyo tulikosea?