Hebu njoo tujadili na tufikirie wotee kwa mifano thabiti ......
1. Namjua John,
Alikuwa afisa biashara Halmashauri kubwaa, matajiri wakawa wanamfata na kumtafuta ili mambo yao ya kwenye biashara yaende.
John alikua na connection BRELA, TBS, TRA, kifupi taasisi 15 zinazosimamia biashara.
Ghafla John ndoa ikawa ngumu, imembidi John ahame Halmashauri kwenda kuanza maisha huko Halmashauri ya chaka ili tu awe mbali na mkewe.
Kakimbia madili mjini kisa NDOA..!!!
Ndoa imesepa na ikaondoka na pesa/madili.
Alichagua amani ya moyo na kuacha madili yoteee mjini.
2. Namjua Salum,
Walianza mahusiano na mkewe wakiwa hawana kitu.
Mke na mume wali "bond" sanaa maana ni wapambanaji.
Maisha yakawanyookea.
Salum alikuwa ni mtumishi wa Halmashauri, mke mama wa nyumbani.
Kila shilingi kumi akiipata anapeleka kwenye mipango ya ndoa.
Ndoa ikawa ngumu na kuachana kukaingia.
Salumu aliondoka hana kitu, kisa anamuachia kila kitu mkewe ili aleee watoto wao wa4.
Yeye anaenda kuanza upya kwengine..!!
Wanaume tunanyanyasika sanaa kiuchumi kisa ndoa.
3. Namjua Peter,
Jamaa alimua kuoa na kujenga mjengo.
Yaani alijenga jengo la mil 150 hivi kwa kukadiria na ni ghorofa nzuri.
Baada ya miaka 7 kulimaliza lile ghorofa aliandaa ka-ibada fulani na kutukaribisha sisi marafiki tukazindue nyumba.
Kufupisha story, waliishi kwenye lile ghorofa kwa miaka 3 na hapa navyoongea na wewe mahakama wanalipiga mnada kwa Mil 200, kisa NDOA..!!
Na juzi kwa macho yangu nimeziona karatasi za mahakama zenye thamani ya mjengo..!!!
Mateso, shuruba na mahangaiko ya ujenzi ya miaka 7 yameyeyuka vuuuppp, kisa NDOAAA...!!!
4. Namjua Michael,
Mshkaji wangu muhaya.
Huyu alipo ajiriwa tu alianza yale majigambo ya kihaya.
a. Nioe mtoto mzuri
b. Ninunue gari, halafu ndio nijenge.
Kweli bwana akaoa, akanunua crown.
Navyozumza na wewe hapa, Crown ilishauzwa na kila mtu ana time lake sasa hivi...!!!
Hiyo ni NDOA...!!!
5. Someni kwanza hawa, halafu nitaendelea .........
CONCLUSION
Mateso yotee ya.....
1. Kubeba mabox ulaya
2. Kutukanwa na madiwa Halmashuri
3. Ku "danki" taasisi zotee zinazochunguza ufisadi unaoufanya
4. Ku "toili" kwenye jua na mvua, usiku na mchana.
Mateso yotee yale kisa mke/familia wale vizuri, walale pazuri, yaani wasiteseke YANAKUJA KUHARIBIWA NA NDOA .....!!!
Wewe uliye kwenye ndoa umejipangaje na haya..!!???
NDOA ni ujinga mkubwa sanaaaa.
#YNWA
#YANGA_BINGWA