Natambua sio lazima na mimi binafsi sijafunga ndoa na wala sina mpango huo, lakini kusema haina ulazima haimaniishi ya kwamba ndio hauwezi kuyaona mapungufu. Sawa ndoa sio lazima, je ni sawa wanawake kuitumia kama mradi ambao unaacha maumivu kwa wanaume?
Suala la kupaza sauti sio la wanaume peke yao. Hata mwanamkr anaeona muundo haupo sawa anaweza kupaza sauti maana mwanaume sio boyfriend au mumeo tu. Hata kaka ako, mtoto ako wa kiume nao ni jinsia ME kesho na kesho kutwa wanaweza kunasa kwenye mtego. mfano hizo sheria mnazosema ni kandamizi kwa mwanamke hamkuzipinga peke enu kuna wanaume waliwaunga mkono
Mimi nimefunga ndoa na Ina zaidi ya miaka 14 kama sijakosea...
Hakuna mwanamke anaye tumia ndoa kama mradi baada ya kuachana na wengi hawapendi
Hili suala la mradi nalijibu hivi kwa mawazo yangu na si kisheria maana sina taaluma hiyo....
Mwanaume ana miaka 30 anaoa Binti wa miaka 18 na baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 8 inatokea mizozo na mnaachana!!!! Hapo wa kuonewa huruma ni binti kwa sababu kwa umri wa mwanaume miaka 35 ni wazi alijiandaa kwa ndoa huku huyu Binti wa miaka 18 - 23 hakuwa amejindaa bali alivishwa majukumu pengine hata asiyoyajus maana yake ni Nini???
Nadhani hata watunga Sheria za ndoa Kuna mengi ambayo waliyachambua na kuja na maamuzi yaliyopelekea Sheria zitungwe.
Kiukweli wanawake wanatumika mnoooo!!!!
Hivi unaijua uchungu wa kuachwa na watoto wewe!? Maumivu mitazamo ya jamii....
Wanaume wan unyanyasaji wao ambao huumiza sana wanawake hata kuwateteea ni ngumu mnooo...
Mfano unataka tutetee wanaume ambao
1. Mimi nazalisha nalea tu sioi
Hivi unaujua uchungu wa kulea mtoto bila baba halafu mitandaoni eti single Maza wamejaaa
2. Mwanaume mwenye wake wengi na mahawala.
Hivi unaujua uchungu wa kushare wewe
3.Mwanaume hatimizi majukumu
Wewe mwanaume usiyejua kutimiza majukumu... Hivi unaujua ndoa nyingi zilizodumu ni mama ndie kasimama ukibisha hili kamuulize mama yako mzazi...
Kutumia pesa Kama fimbo.
Yaliyomo ndani ya ndoa ni makubwa mnoo wanaume wenye pesa wananyanysa sana wanawake ndani ya ndoa Tena Nina shuhuda japo siwezi kuandika.
Sasa basi kuwatetea wanaume ni ngumu mnoo sababu wanayofanya kunyanyasa wanawake ni mengi.
Ninachojua mwanaume yoyote yule akitaka ndoa hubadilika na akitaka kuitunza huipambania sana.
Mengine tuache nature itawale