Ulishawahi kuwa kwenye mahusisno na msichana anayechagua vyakula? Mimi nilimlaza njaa siku mbili akaanza kula ugali dagaa

Maboga,magimbi,biriani ni misosi mitamu sana kwangu
Ndiyo ujue binaadam/watu tunatofautiana.

Kuna wengine makande hawali kabisa ila mimi Kande ukiweka na parachichi hapo pembeni ni hatari FIRE
 
Hamna kilichonipata huo ushauti nilipewa na dingi kuhusu Hawa warembo.

"Huna mbele Wala nyuma kama mchezo wa sabuni" hii alinitamkia yule mwanamke shetani kabisa
🤣 mbona hujakutana na shetani bado..!!
 
Me huwa sina washkaji
Na washkaji niliokuwa nao zamani siwezi kutembea na mademu au na ex zao
Wewe ni snch na ndivyo washkaji wengi walivyo
 
Mimi sijawah kuubaliana na hii kitu, dada zangu hawana vitambi na tumelelewa maisha haya toka utotoni.
Na mimi huwa nawakomalia wanangu wasije kabisafuatisha hii tabia ya mama yao.

Ila wanawake hajui kipimo cha chakula ,sasa kwanini apike wali mwingi na ubakie halafu hauli? Kwanini asipike wa kutosha kwa usiku tu au kubakisha kidogo kwa watakukula? Mimi mwenyewe sipendi kula chakula kilicholala napenda kula fresh kilichopikwa kwa siku hiyo.

Nilichogundua baadhi ya wanawake hawataki kupika pika uvivu so anapiga chakula kingi akitegemea wengine waje kula kesho yake yeye asijishughulishe.
 
Acha tu. Nisiseme sana
 
Hao wengi wao hawajafikia level ya kujitafutia maisha,wakianza kujitegemea akili za budget zinakaa sawa
 
Mimi nilimlaza njaa siku moja kagoma kula eti hataki kitimoto.Siku hizi ni mlaji mzuri mambo ya imani na vyakula wapi na wapi.
 
Dagaa wamekuwa ghali kuliko nyama, utashangaa maisha yanavyozidi kuwa magumu.
 
Niliwahi kuwa na kabinti ka namna hiyo, hata chakula kanachokula unakuta kanagusa na kuacha...nikamwambia haya sio maisha mama, kama hutaki chakula ni bora tusiagize kuliko hiki unachokifanya.
 
Baadae ukaanza kufukia misosi, unakula kama nyangumi, maugali na michuzi yote unafukia kontena zima.
Njaa itakufunza nenda jela au boarding school za SERIKALI au zamia hata dar es salaam bila pesa Wala ndugu..

Mzee utakunywa maji ya chumvi na utayaona normal.

Mfano Mimi naonaga mbagala wanauza makwasu kwasu nikimaanisha..wanachemsha ngozi za ng'ombe na kuuza supu , pumbu za mbuzi ,ng"ombe na mapupu, bandama,vichwa vya kitimoto, miguu ya nguruwe
Mkuu 😊 utakula Mbona njaa ni best teacher.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…