Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Jimbo ninaloishi mimi madiwani wote ni ccm na mbunge pia lakini hakuna chochote kinachofanyika na madiwani na mbunge hawajawahi kufanya mkutano hata mmoja tangu wachaguliwe hapa changamoto zilizopo zitaibuliwa na nani?

Kiukweli baada ya kuzuia mikutano ya kisiasa nchi imeathirika sana viongozi wengi hasa wa ccm wamebweteka maana hakuna wa kuhoji, na inawezekana na wewe ni miongoni mwao.
Kuna maendeleo gani wakati viongozi hawabanwi?

Mimi naamini kuna majimbo ya wapinzani ambayo yana maendeleo makubwa pamoja na kuwepo mikutano ya hadhara kabla ya awamu hii kuingia madarakani, mikutano kazi yake ni kuhamasisha maendeleo siyo vurugu pia ni haki ya msingi ambayo hutambuliwa na sheria ya vyama vya siasa ya 1992

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hiyo miswada mibovu na mikataba mibovu huwa inapitishwa na wapinzani.
 
Na wewe pia ni kiongozi huko kijani ambapo wanalazimisha hata jambo lisilofaa lishangiliwe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo wewe unajua zaidi ya majaji waliositisha likizo kuja kusikiliza.
Wapinzani mnafanya mambo ya kutia aibu kabisa;

Mtu anaamua kwa makusudi kabisa kukiuka masharti ya dhamana; wenzake wanaamua kukutana huko hotelini na kumtangaza kuwa ni mfungwa wa kisiasa. What a shame.
 
ZZK tapeli wa siasa at work.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa Upinzani Tanzania kwa movement hii. Bila shaka itaonesha picha kwa Magufuli na Serikali yake kwamba Watanzania TUNATAKA UTAWALA WA SHERIA na siyo kinyume cha hapo...!!!
Kama JPM anataka kuleta habari za Rwanda na Burundi asahau hilo. Mwalimu JK Nyerere(rip) katuachia AMANI lakini mafisi wa CCM leo wanataka kuiangamiza nchi kwa tamaa zao za kungangania Ikulu!!!
 
Kwahiyo wewe unajua zaidi ya majaji waliositisha likizo kuja kusikiliza.
Hahaha watu wanapata shida sana humu JF, Kuna mtu nimemtisha kule utasema mi ndiye TISS kumbe wapi mbwigika tu mmoja toka vichochoroni huko! Naona nawe jamaa yangu hapa unaambiwa wewe ni kiongozi huko timu ya mtani wa jadi! Lakini yote kwa yote wote wananchi tunahaki ya kutetea, kukosoa na kushabikia pale panapobidi alimradi hatukiuki tu sheria, mi ni CCM lakini nikikutana na hoja ya kukosoa iliyoshiba wala sina ata kinyongo na mtoaji alimradi awe na evidence tu.
 
Hii kitu sio kituko!! Unapinga mswaada ambao haujawa sheria au wanapingwa usijadiliwe bungeni? Mahakama inaweza kuingilia mswaada ulioko ktk muhimili wa Bunge kwa kujadiliwa?
Someni hiyo Ibara ya Katiba ya JMT muone kuwa hawajakurupuka kufungua kesi.

30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

2)......

3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

4).......

5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, na Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika, kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha hitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusika katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na sheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa ni halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda uliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupi zaidi ndio uzingatiwe.
 

Wewe badala ya kuongelea mada unatoa ushuzi tu
 
Nchi inajengwa na watu wenye mitazamo chanya ;

Sasa Hawa wetu ambao wanadhani kuwa mwanasiasa wa upinzani ni kupinga Kila kitu sidhani Kama ni msaada sana kwetu.

Huko kwa wenzetu Kuna baadhi ya Mambo huwa wanakubaliana. Hapa hali ni tofauti.
Mkuu unasahau kuwa mawazo yanayotamalaki ni ya mtu mmoja ambaye akili yake ina flip flop. Leo anaweka sahihi Kesho anatengua bila utaratibu wa kisheria. Nadhani ukajifunze zaidi maana ya nebo chanya.

Muswaada huu unatokana na akili za kutilia shaka.
 
Mkuu mbona unanichanganya?Hoja ya hao wasanii ni kulizuia bunge kufanya kazi yake ya kutunga sheria au kuomba mahakama itamke kua muswada wa sheria ya vyama ni batili?
Naona unahamisha magoli kisayansi
Kwa upeo wangu mdogo wanatakiwa waiache sheria ipite,wakaipinge mahakamani,lakini hawana uwezo wa kulizuia bunge lisitunge sheria
Hii ilishindikana pia wakati wa kutunga sheria ya bunge la katiba,wapinzani walijaribu kuitumia mahakama wakakwama
 
Kwa hiyo? Kuwa muwazi ili tufanye yetu!
 
Mawazo yako na ya ******** hayana tofauti yamejaa chuki, ujinga, roho mbaya na kila aina ya ujinga

2020 John Walker out
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…