Jimbo ninaloishi mimi madiwani wote ni ccm na mbunge pia lakini hakuna chochote kinachofanyika na madiwani na mbunge hawajawahi kufanya mkutano hata mmoja tangu wachaguliwe hapa changamoto zilizopo zitaibuliwa na nani?Shidanata sio ukijani shida tumezoea siasa holela! ni ukweli ulio wazi kuwa waafrica vichwa vyetu haviwazi kushikamana kwaajili ya maendeleo yetu sie tupo ili tukwamishane tu! hatupendi hata kidogo mtu fulani afanikiwe na hapa ndipo white wanapotutumia kwa udhaifu wetu huu!
Siasa za kiafrica hazioni hatari wanasiasa wake wakikesha barabarani wakiandamana! siasa za kiafrica kila kukicha mikutano ya hadhala. Hizi siasa za kiafrica usitegemee bunge liwe na wabunge wengi wa chama pinzani alafu utegemee bajeti kupita! Hivi ata reli ya SGR isingejengwa kama humo bungeni kungekuwa wabunge wa upinzani na baadae wangekuja wao kuomba kura kwa kigezo wale wameshindwa kufanya sie tutafanya.
Kiukweli baada ya kuzuia mikutano ya kisiasa nchi imeathirika sana viongozi wengi hasa wa ccm wamebweteka maana hakuna wa kuhoji, na inawezekana na wewe ni miongoni mwao.
Kuna maendeleo gani wakati viongozi hawabanwi?
Mimi naamini kuna majimbo ya wapinzani ambayo yana maendeleo makubwa pamoja na kuwepo mikutano ya hadhara kabla ya awamu hii kuingia madarakani, mikutano kazi yake ni kuhamasisha maendeleo siyo vurugu pia ni haki ya msingi ambayo hutambuliwa na sheria ya vyama vya siasa ya 1992
Sent using Jamii Forums mobile app