Miaka hio India ndio walikamata Uchumi wa Dunia, walipishana wao na China, so walikua vizuri kwenye suala la mitaji.
View attachment 3583421
Hapo Gujarat wakati huo na Hadi Leo ndio moyo wa India, mabilionea 108 Kati ya 190 wa India ni wagujarati na wafanyabiashara wakubwa walitoka hapo kuna sehemu Inaitwa "Kutch" watu wa huko wakawa Nicknamed "Kutch moneybag". Hata wahindi wa Tanzania hao Ismailia wanaongea kihindi kwa lahaja ya "kachi" ambayo inatoka huko.
Hao jamaa walisambaa Dunia nzima kuanzia Indonesia na Malaysia Asia ya Mbali, Hadi kwa Waarabu Sehemu kama Dubai kwa kiwango kikubwa wamehusika wao kujenga, nenda UK na USA wamehusika kikubwa biashara za huko Hadi huku kwetu.
Huku kwetu kabla sultan hajakuja alipinduliwa kule Oman, akakimbilia India ya zamani ambapo alitegeneza "koneksheni nao" alivyorudi Oman na baadhi wakawa part ya Elites wa Oman, hata Alivyokuja Zanzibar alikuja nao, kama nilivyoweka huko juu waziri Mkuu wa Zanzibar alikua ni Mhindi aliitwa Sir Topan, Hawa jamaa ndio walikua financer wa miradi ya Sultan, wao walitoa hela na mipango, kuleta technology, Sera za nchi etc. wengi wasiojua hawa jamaa pia ndio heart ya Ukoloni wa muingereza walikua na hela na wao ndio walimuwezesha muingereza kutawala maeneo mengi.
So walipokua huku walijenga Znz, wakaja wakaijenga Dar Shule kama Jangwani, Tambaza, part ya muhimbili na nyumba ambazo Leo ni za NHC etc huwezi kamwe Eti uletwe na muingereza kujenga Reli then uporomoshe Maghorofa, Hospitali, Shule na miradi ambayo hata waingereza wenyewe wakoloni hawana uwezo wa kujenga.