Unadhani kwanini vijana wanapenda sana kuajiriwa serikalini kuliko kampuni binafsi?

Hela za kuiba zipo nje nje, na pia hata ukiiba kama siyo mchoyo ukiwagawia na wakubwa hakuna kesi.
 
Mm kwa experience yangu koz now niko serikalini, hapo mwanzo nilikuwa huko private. Private unafanya kazi mpka unakoma. No time to rest, hakuna mafao sijui kama mama mjamzito wa hela ya likizo. Et mdada akipata mimba boss anachukia kwamba umepunguza nguvu kazi. To gvmnt ni virce versa
 
Kwa michango hii, basi output ya wengi wetu ni mbaya sana kiasi kwamba we can easly be replaced. Kama unajiamini unapush na una mchango mkubwa kwenye kampuni, huwezi fukuzwa au achishwa kazi kizembe. Sana sana utalazimishwa upewe mkataba wa muda mrefu na mkopo ili usiondoke.

Ukiwa unajiamini na utendaji kazi wako, huwezi kuogopa kufanya kazi private za maana ambao ndio kuna real growth na kama mmeona wenyewe, hata marais wanapenda kuwapa watu waliotoka private sector sehemu za kiuongozi kwenye mashirika na taasisi zetu za umma.

Tuboreshe michango yetu, tuache uvivu na uzembe na wizi na excuses nyingi.
 
Serikalini ni sehemu ambayo unaweza ukawa na miradi yako binafsi na unaiendesha bila bugudha na vitisho vya kufukuzwa kazi. Kuna ujamaa sana serikalini tofauti na kwa mtu binafsi ambaye focus yake ni kuwatumikisha hadi mzalishe faida.

Mshahara wa private lazma uutolee jasho haswaa!
 
Hayo mashirika pia kupata sio rahisi. Kuna kitu kama MDH ama AMREF hebu niambie unaingiaje huko😅
 
Kwa kifupi serikalini kuna benefits kibao zinazoambatana na kibarua chako. Unahakikishiwa kazi na support ndio maana watu wengi hupendelea serikalini.
 
Hao Roche na Gsk ni wepi mkuu tuanze kusuka cv

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hii ndio sababu hatuendelei kama nchi. Watu wanafikiria kuajiriwa serikalini ambako anajua hata akifanya makosa kiasi gani bado atabaki kazini na zaidi zaid anaweza kuhamishwa eneo moja kwenda jingine.
Makampuni binafsi hayana mambo hayo ilhali wapo watu wengi mtaani wenye sifa sawa na wanatafuta kazi.
Nilitamani sana Serikali ingeanza kutoa ajira kwa mikataba ya miaka mitatu mitatu na kuendesha ofisi za umma kama makampuni yafanyavyo ikiwa ni pamoja na kuwaondoa kabisa kazini wazembe.
Ndani ya miaka hiyo iangalie productivity ya mtumishi kulingana na rules/agreements watakazo kua wameziweka.
Yakifanyika haya, basi hata tatizo la ajira linaweza kupungua kwa wanaohitimu. Maana juhudi yako ndio itakufanya ubaki kazini.

Natamani iwe hivyo lakini!
 
Hela za kuiba zipo nje nje, na pia hata ukiiba kama siyo mchoyo ukiwagawia na wakubwa hakuna kesi.
Ajira Private sector ndo mpango mzima Contract ikiisha unalamba NSSF yako unarekebisha mambo unaanza na moja sio serikalini usubiri kustasfu miaka 55 kwa hiyari ndo ulambe mkwanja swala la Job security sio kweli Mwendazake alitumbua majipu watu kibao bila kufuata taratibu za utumishi wa umma.
 
Adhani elimu ya pensheni haijaeleweka
 
Huyo hakuwa anaplan kama ilivyo Kwa vijana wengi, pia maisha ni ndoto je unataka uwe wapi Kwa muda gani, only 35% ya kazi za serikali ndio zipo kwenye asali 65% watu wanateseka bila kujijua wakisubiri maisha mazuri pindi watakapo staafu, yaani uteseke 30yrs kabla ya kustaafu
 
Kosa mnalolifanya ni kugenerised hivi mlikuwa private za maana au mnaongelea vibarua?
 
Kwa kifupi serikalini kuna benefits kibao zinazoambatana na kibarua chako. Unahakikishiwa kazi na support ndio maana watu wengi hupendelea serikalini.
Hata huko serikali ni only 35% waliobaki mnavyosema per dm hata hawaelewi
 
serikalini patamu, wiki ya pili sijaingia class na nitaingia kuanzia tar2 baada ya hotuba ya mama, akiongea anavyotaka yeye nitamaindi sana
Sasa chukua your salary gawanya Kwa mwezi husika then tofuta hizo week mbili mwajili wako amepoteza kiasi gani? Utakuta nothing,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…