Ndugu nakushaori usiache hiyo kazi ya ualimu wala usidanganyike na wala usidanganywe hata kidogo kuacha kazi, cha msingi unaweza kupiga hizo mishe zingine huku ukiwa unaendelea na ajira yako. Wakati tuko kanda ya ziwa miaka minne nyuma kuna mwalimu kama wewe aliachaga kazi serikalini akaingia katika NGOs ya watu wa Wamerekeni hapa na pale lile shirika likafunga ofisi kulingana na sera za mwendazake hiyo ilikuwa mwaka 2020, mpaka hivi tunavyokwambia jamaa bado yupo kwenye kuti kavu na uamuzi aliouchukua kipindi kile mchizi anajuta sana. Kiongozi kama umeajiliwa serikalini usiache kazi eti ukajiajiri, usiache kazi serikalini eti uende sekta binafsi huo ni uchawi Comrade nakuhusia tulia hapo ulipo usishawishike kuacha kazi serikalini, wewe uliona ajira gani mwajiliwa hata kama akipatwa na maradhi ya muda mrefu ya kumfanya ashindwe kufika ofisini lakini bado ataendelea kulipwa ili mradi kuwe tu na taarifa zake katika ofisi husika je kwa sekta binafsi hili suala linawezekana? ajira ni serikalini, ajira ni serikalini, namalizia tena AJIRA NI SERKALINI......................................................................................