lukubuzo Samsis
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 2,947
- 3,466
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja limeanza kufanya uchunguzi zaidi kuhusu tukio la Msimu Jaffari (33), kudaiwa kuchoma moto gari ya mumewe, ambaye wiki iliyopita alitoa taarifa ya kuongeza mke wa pili katika ndoa yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Kesi hiyo imeripotiwa katika Kituo cha Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
Kamanda Hassan alisema tukio hilo, limeripotiwa mwishoni mwa wiki huko Kitumba Wilaya ya Kati Unguja. Gari aina ya Spacio inayomilikiwa na Abdallah Hijji (43) ilitiwa moto usiku.
Mke wa kwanza wa mtu huyo, anatuhumiwa kufanya tukio hilo. Alisema taarifa za awali katika uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi, unaonesha kwamba Hijji alitoa taarifa kwa familia na mkewe wake wa kwanza, kwamba anakusudia kuongeza mke wa pili.
‘’Uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi katika hatua za awali unaonesha kwamba tukio hili linahusishwa na wivu wa kimapenzi, ambapo mume alimjulisha mkewe nia ya kuoa mke wa pili na kama unavyojua wanawake wengi hawapendi ukewenza. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na ukweli halisi wa tukio hilo,’’ alisema.
Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili, kwa kuwahoji watu mbalimbali huko Kitumba, umeonesha kwamba Hijji aliongeza mke wa pili wiki iliyopita. Hatua hiyo ilimtia hasira mke wa kwanza, ambaye kabla ya ndoa hiyo alikuwa akitoa tahadhari kwa mumewe, kwamba asithubutu kuoa mke mwingine.
‘’Huyu mwanamke hataki ukewenza, kwa muda mrefu amekuwa akimuonya mumewe asijaribu kufanya kitu hicho na akifanya atajuta,’’alisema jirani ya Hijji, Haji Omar ambaye alidai amekuwa akishuhudia mara kwa mara ugomvi wa watu hao.
Jeshi la Polisi limesema uchunguzi utakapomalizika, jalada la kesi hiyo litapelekwa Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.
Chanzo: HabariLeo
Kushare panauma. Bora mimi ni mkristo ndoa ni moja. Chepuka huko nje ila hauoi mtu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo lazima aridhie ila ni lazima apewe taarifaHivi siyo kwamba lazima mke wa kwanza aridhie kwanza ndipo mme unaongeza mke wa pili? Na kama ndivyo iweje jamaa aongeze mke bila kupata ridhaa ya mke mkubwa?
Tena ni Malaya wa kuokotewa mbali. Wakiwa hawajafikisha wake wanne wanadanganya nitakuoa , dini inaruhusu. Wakifika wanne sasa ni umalaya na wakati mwingine wanatafuta sababu za kutoa talaka ili waendelee kuoa.Hata awe na wangapi kama ni mzinzi ni mzinzi tu, mie kuna familia nilikuwa nawafahamu yule tena mwl alikuwa na wake wa 4, alikuwa anawatoroka wote anaenda kudanga na michepuko huko [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mpaka nilikuwa namuuliza hao wake zako umewapa nini kuwafanya wajinga hivyo !
Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa nimekusikia 😂 😂
Mpare OGIyeee! Ahsante kwa kufahamu asili yako ni wapi
Yetho ja misi?Mpare OG
Sasa hapa umekwepaje kushare?Kushare panauma. Bora mimi ni mkristo ndoa ni moja. Chepuka huko nje ila hauoi mtu.
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Umesahu na kukuridhisha sio nguvu zenyewe za kutegeshea mlimani unaweka gogo halafu anaenda kiongeza mke! Hapo si ndiyo mwanzo wakutafuta vipozeo, ukute mtu anapata stimu baada siku 4 mpaka wiki halafu anajishauwa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Tunanogewaga huko nnje tunahamia kabisa afadhali kuwa wazi kuliko makandokandoKushare panauma. Bora mimi ni mkristo ndoa ni moja. Chepuka huko nje ila hauoi mtu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuchepuka ni tabia..Sasa huoni anaechepuka anakuwa na wanawake wengi zaidi ya huyu alieongeza? Halafu uwezekano wa mchepukaji kuleta maradhi ni mkubwa kuliko alieo
Sent using Jamii Forums mobile app
Wale wanavumilia maigizo tu au pana mshiko...kinyume cha hivyo....Haya mambo uyasikie tu yasikutokee
Hivi nyie baadhi ya wanaume mnafikili kila mwanamke ni kama wake wa Dr mwaka?
Angewachoma wote mume na huyo mwanamke
Ikiwa hivyo basi nayeye aruhusiwe kuchepuka.Hiyo ni kwa upande wako Mkuu.
Mwanamke hajadhulumiwa hapo ndo kafanyiwa ustaarabu kuliko kuchepuka kimya kimya na kuleta magonjwa.
Hakuna dhulma hapo labda kwako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi waliooa wake wawili au wanne ndio hawachepuki kabisa???Hiyo ni kwa upande wako Mkuu.
Mwanamke hajadhulumiwa hapo ndo kafanyiwa ustaarabu kuliko kuchepuka kimya kimya na kuleta magonjwa.
Hakuna dhulma hapo labda kwako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Na Bado zile Bikira 72 za ahadi.Na ukristo unawanyanyasa Sana wanaume, by nature wanaume ni watembeza bakora haswa na pia tuna matamanio ya kuwa na wanawake zaidi ya mmoja(kuonja taste tofauti), hivyo kuniletea vifungu vya kunikataza nisiwe na zaidi ya mmoja ni uonevu wa hali ya juu, Nani ataijaza dunia, hii idadi kubwa ya wanawake Nani ataisitiri!? Kama mwanaume umekamilika tuongezeni wake ili tuwasitiri
Sent using Jamii Forums mobile app
Yani unaniuliza swali ambalo mimi nimekuuliza.
Waruhusu wewe wale ambao unawamiliki.