Uongozi wa UDSM watoa angalizo uwepo wa CHATU maeneo ya Shule ya Msingi Mlimani

Naunga mkono hoja
 
Watu wa Dar Es Salaam buana!
Yaani chatu ni tishio kweli mpaka barua kuuubwa na kwenye vyombo vya habari?

Ebu njooni huku kwetu KISIWANI NYAMASANJE CHITARE MAJITA HAPA muone tunavyo watumia mamba kama vigoda vya kukalia.
 
Hadi limezwe jitu ndiyo mamlaka zitamuondoa huyo nyoka aliye mponza ADAM na Hawa kula tunda
Hakuna atakayemezwa hapo kama Tahadhari iliyotolewa itazingatiwa kikamilifu. Halafu Tukumbuke huyo nyoka yupo porini ambako ni makao yake HALALI. Ndo mana tunashauriwa kuweka mazingira yetu safi kwa kuondoa vichaka au mapori; kwani usipofanya hivyo unastawisha makao ya viumbe wengine tofauti na binadamu. Labda itokee ameingia ndani ya nyumba au Mabweni ya wanafunzi.
Vp wanafunzi hawafanyagi "fatique" kila jumamosi ya kwanza katika mwezi? Au wamesoma sana hawawezi kushika kwanja? Nakumbuka hili lilikuwa ni Agizo la Mh. Magu.
 
Nilikuwa sijawahi pita njia ya goba kuitafuta mlimani city aisee kama ndo ule ndo msitu wa udsm bhasi mnaweza kesha kumtafuta kumbe dar bado tuna ardhi kubwa snaaa..!
 
Watu wa Dar Es Salaam buana!
Yaani chatu ni tishio kweli mpaka barua kuuubwa na kwenye vyombo vya habari?

Ebu njooni huku kwetu KISIWANI NYAMASANJE CHITARE MAJITA HAPA muone tunavyo watumia mamba kama vigoda vya kukalia.
Ni kweli watu wa Dasilamu wanashangaza kama sio wanasikitisha kwa vituko vyao.
Laiti wangelifika huku Umasain ndani ndani huku wajionee jinsi chatu anavyodharaulika na hakuna mtu anahangaika naye ila tunakwepesha kuchunga mbuzi na kondoo eneo hilo au kwenda na mbwa mahali hapo kwani mbwa lazima atajipeleka mwenyewe kwa chatu na aliwe kiulaiiiini. Ukisikia mara moja tuu kwii-kwiiiii. Ujue huyo mbwa imeenda.
 
Mzee Nyani hata chatu wa Afrika wanameza watu ingawa hutokea mara chache.
Inawezekana maana hata mtoto mdogo ni mtu pia.

Lakini, kuna documented cases za hao African rock pythons kumeza watu?

Maana mpaka sasa documented cases za giant snakes kumeza watu zipo Indonesia huko.

Sijawahi kuona case yoyote ile ya anaconda, Burmese na African rock python kumeza watu.

It seems matukio yote ya watu kumezwa na giant snakes yanatokea south east Asia.
 
Dah!
Alirudisha?
 
Nyoka aina ya chatu unamwogopaje?
Wasomi bhana, nyoka hana sumu yoyote, hashambulii, yeye anawinda tu tena chatu ni mwoga sana kwa binadam
 
Huyo Chatu kaja na mwanafunzi wa first year.
Ila watu wa Dar waoga sana, huku Tukuyu tunaishi hao hao chatu hawana madhara
 
Sio rahisi kupata documented cases lakini hiyo haimaanishi kwamba cases hizo hazipo. Huku vijijini yapo mambo mengi au matukio mengi sana ambayo Taarifa zake hazikutolewa; sio kwa makusudi ila ni kutokana na Teknolojia hafifu au Taarifa zake zimebaki kama simulizi tu miongoni mwa Jamii.
 
Sawa.

Lakini ili kupata uhakika tunaenda na ushahidi/ ithibati.

Mpaka sasa tunachokijua ni kwamba matukio hayo yametokea southeast Asia yakihusisha retics.

Yawezekana hata Afrika yapo. Yawezekana hata Amerika ya Kusini yapo.

Tofauti ni kwamba, huku ushahidi tunao. Kule ushahidi hatuna.
 
au ni janja ya wasiojulikana kuna mwekezaji kaandaliwa kisa msitu unahifadhi chatu
 
Unazifahamu kazi za TAWIRI?
 
Africa na kumbukumbu kama hizo ni ngumu. Tukio linatokea na kupita bila kumbukumbu yoyote.
 
Africa na kumbukumbu kama hizo ni ngumu. Tukio linatokea na kupita bila kumbukumbu yoyote.
Kwa zama hizi si vigumu kivile.

Asilimia kubwa ya watu wana simu janja siku hizi.

Matukio mengi sana yanakuwa captured kwenye simu.
 
Dah!
Alirudisha?
Hakurudisha alienda nayo mitini bahati nzuri akaiangusha anavyoruka. Ngedere wa UDSM wakorofi na wachokozi mno hawaoni shida kuja kuchukua chakula mezani unapokula.
 
Reactions: Cyb
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…