UPDATE: Padri afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kulawiti watoto 10 Moshi

Huu ni upuuzi wa mashetani wa kanisa katoliki. Mbona nyuzi nyingi za huu upuuzi wao, hujaziona hizi; Chato: Katekista wa kanisa Katoliki akamatwa kwa tuhuma za kubaka mtoto wa miaka 8
Jiongeze wewe ficha ujinga wako, kwani kanisa ndio limemtuma afanye hayo makosa yake. Hakuna masheikh waliowahi kubaka au kulawiti huko madrasa na sehemu zingine, je uislam ndio umewatuma?

Hakuna anayemtetea huyu padri, kafanya makosa sheria ifuate mkondo wake ila kitendo cha kulaumu taasisi kana kwamba ndio iliyomtuma ni kukosa akili.
 
Suluhisho la hili ni rahisi sana. Acheni kuwapeleka watoto kwenye hayo yanayoitwa mafundisho ya dini. Mnawakosea sana na kuwaharibia future zao kwa mambo yasiyohitajika katika umri wao
Zamani ilikuwa ni sifa kwa Wakatoliki na Waanglikana (High church) kuwapeleka Watoto wao kutumikia misa kanisani na kulelewa katika mashirika ya Mapadri

LAKINI kwasasa, ni bora kabisa Mtoto hata asipate mafundisho ya kutumikia wala komunio kama ndio upumbavu huu unafanywa na mapadri namna hii.
 
Martin Luther was a Padre and Failed to stay alone

Let them Marry.
 
Serikali ichunguze au iunde tume ya kuchunguza mapadri wote wa Hilo kanisa katoliki nchini

Kuna wengi wanafanyiwa huo uchafu hila hawasemi tu, hata Hawa mashoga wengi asilimia kubwa walianza kuliwa na hao watu, haiwezekani dume zima linaambiwa heti lisioe mke, nyege zake apeleke wapi sasa?

Ndio chanzo Cha kuwa na mashoga wengi nchini na duniani kote, hata humu mitandaoni wengi ambao wanamtetea huyo padri au mapadri, unakuta nao Ni mashoga na walisababishiwa na hao watu,

Mimi mkristo lakini Hawa watu hawafai wachunguzwe haraka wanatuletea mambo machafu aisee, japo sio wote, hila asilimia kubwa Ni waffiraji hao watu
 

Attachments

  • Screenshot_20220929-072853.png
    140.2 KB · Views: 10
Mapadri wasifae kwa sababu ya uovu wa watu wachache?, hakuna masheikh ma ustadh ambao wameoa lakini wanalawiti, hakuna watu wa familia walio oa lakini wanalawiti na wanabaka. Hivi vitu vipo na ni hulka ya mtu binafsi sio taasisi

Wewe una chuki zako binafsi ila makosa kama haya watu wa angle zote wanayafanya.
Ushoga umetokana na utandawazi hao ma padri utakua unawasingizia tu, je nchi za kiarabu au nchi ambazo ukatoliki haupo kwa kiasi kikubwa hakuna mashoga?,

Simtetei padri wala siungi mkono alichokifanya, na naomba achukuliwe adhabu kali kwa alichokifanya
 
Hawa mapadri wanakula na kunywa vizuri wana usafiri bado wanalala pazuri

Hio protini wanayozalisha halafu eti wasioe wala kuonja papuchi


Mnajisumbua bure waruhusuni tu wale hata ma sister
 
Martin Luther was a Padre and Failed to stay alone

Let them Marry.
Upadri ni wito mkuu, bahati mbaya mapadri waovu kama hawa ndio wanaochafua taswira nzima ya nia njema ya wito huu.
Mapadri hawaoi kwa sababu upadri mbali ya kua wito ni sadaka (lengo nzima lipo hivyo achana na hawa wanaoharibu kazi)

Sadaka ya upadri ni ile ya kutokuoa, Rejea mfano wa Mathayo 19:12 Yesu alipoongea kuhusu Matowashi (Japo hapa padri lazima awe mzima upande wa nguvu za kiume kwa sababu lengo kuu la sadaka ni lazima ikuumize, uitoe kwa moyo wote) mfano: sio mtu tu hana uwezo wa kusimamisha alafu anaamua kua padri ili kuficha matatizo yake hapana.

Ukatoliki unaamini kumtumikia Mungu kumegawanyika katika wito wa aina mbili,
1. Wito wa Utawa (Mapadri, Masista n.k)
2. Wito wa Ndoa

Hakuna mtu analazimishwa kua mtawa wala mtu analazimishwa kufuata wito wa ndoa, haya ni maamuzi na uhuru wa mtu mwenyewe kuchagua. Hivyo siamini kama itatokea mapadri wakaruhusiwa kuoa sababu uhuru wa kuchagua upo before mtu haja execute uchaguzi wake

Pia kwa maoni yangu binafsi naona mapadri wakiruhusiwa kuoa sasa kila mtu si atataka kua padri, atakua na familia focus itapungua na kuhamia katika familia yake, pia gharama za kuwalea wao na familia zao zitakua kubwa na ghali zaidi.
 
Hawa mapadri wanakula na kunywa vizuri wana usafiri bado wanalala pazuri

Hio protini wanayozalisha halafu eti wasioe wala kuonja papuchi


Mnajisumbua bure waruhusuni tu wale hata ma sister
Sharti moja muhimu sana katika mchakato wa kuwapata watu wa kusomea/kuandaliwa kuwa mapadre ni kuwa muhusika lazima awe rijali. Ili mtu awe padre mkamilifu, anatakiwa azishinde tamaa hizi (za kingono). Hii itaonyesha kuwa kweli ulidhamiria kumtumikia Mungu. Lakini ukishindwa kushindana na tamaa hizi, basi, huko ulienda kwa bahati mbaya.

Kwa wakatoliki, upadre na ndoa, ni madaraja matakatifu mawili tofauti. Ukibahatika kupata daraja moja kati ya haya mawili, basi daraja lingine huwezi kulipata (they are mutually exclusive). Hata masista na mabruda, nao hawatakiwi kuoa au kuolewa, maana nao pia wamejitoa ili kumtumikia Mungu kikamilifu.

Mtume Paulo ameandika katika waraka wake kwa Wakorinto, kwamba, mtu akishindwa kuishinda tamaa ya mwili (uzinzi), basi na aoe, kuliko kuendelea kuwaka tamaa ya mwili. Lakini, alipendelea zaidi watu wabaki kama alivyokuwa yeye (wasioe), ili wawe na muda mzuri na wa kutosha wa kumtumikia Mungu.

Hapa mtume Paulo anasema kuoa au kutooa si dhambi, lakini ukiamua kumtumikia Mungu (kuwa padre), basi inakupasa uachane na masuala ya ndoa (na uzinzi). Haiyumkini mtume Paulo alisema haya ili kuepusha muingiliano wa masuala ya kibinadamu na yale ya kumtumikia Mungu (mgongano wa kimaslahi). Ukiamua kumtumikia Mungu, basi mtumikie kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Padre anatakiwa asshughulikiwe kama panya road!
Ni aibu sana sana kwa Kanisa langu katoliki!

Ni aibu kubwa sana kwa Jimbo la Moshi!
Askofu Minde please huyu shetani msimfiche!
Enzi za askofu Amani aliwasafisha wote wenye tabia kama hizo naona wamerudi kwa kasi ya tozo
 
Huu ni upuuzi wa mashetani wa kanisa katoliki. Mbona nyuzi nyingi za huu upuuzi wao, hujaziona hizi; Chato: Katekista wa kanisa Katoliki akamatwa kwa tuhuma za kubaka mtoto wa miaka 8
hili siyo kwa kanisa Katoliki peke yake,hata misikitini ,mashuleni ,na kwenye familia zetu hizi tabia zinakuwa kwa kasi ya ajabu.
ni lazima Kama Watanzania bila kujali dini zetu na tofauti zetu kila mmoja aombe kwa Imani yake na kukemea hili jambo ambalo linakwenda kuliangamiza taifa letu
 
Kwani ni huyo tu? Makasisi na mapadri wa Kanisa katoliki wanayafanya hayo dunia nzima, tena hawakuanza leo wala jana, ni uozo wa miaka na miaka, Mpaka Umoja wa Mataifa umepiga kelele.
Kama walivyo walimu wa madrasa..wote wale wale
 
Inasikitisha kwakweli, mbona Hawa viongozi wa dini ya kikristo hizi tuhuma zinawaandama Sana, nashauri wafanyiwe uchunguzi na wengineo, huenda haya yanafanyika Sana ila Kuna wahanga Wengine wanashindwa malalamiko yao wapeleke wapi
 
Kanisa limezidi huo uchafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…