TUZITII KATIBA ZETU
Katika Ulimwengu wa KIROHO naonyeshwa UVUNJIFU WA KATIBA PASIPO KUWA NA SABABU ZA MSINGI.
MAONO haya yananiumiza sana HASA kwa kuzingatia WANACCM TUKO WENGI MNO WENYE UWEZO NA UPEO MPANA WA KIUELEWA NA KIUTENDAJI.
Vitendo vya UPENDELEO NA VYA KIBAGUZI katika Ulimwengu wa KIROHO tuonyeshwa vinashamiri.
Naamini HAYA MAONO NI KAMA NDOTO tu na hayana Ukweli.
Ila najiuliza ikitokea ikawepo uhalisia wa Mambo haya ni wazi hali itakuwa ni ya kuumiza kwa wanaccm WAFIA CHAMA.
Naamini HAKUNA MTU ALIYE JUU YA SHERIA WALA ANAYESTAHILI KUPENDELEWA DAIMA.
Niliwahi kusoma Kitabu cha Binadamu na Maendeleo uk 28 - 31
Mwl JK Nyerere aliwahi kuandika,
" Uhuru wa mtu binafsi utakuwa na maana Kama shabaha yake ni MAENDELEO.
Mtu anaweza kutetea haki zake barabara Kama haki HIZO anazijua na ANAJUA JINSI YA KUTUMIA NJIA ZA KATIBA iliyopo kutetea HAKI HIZO.
Hata ujuzi wa namna Hiyo ni MAENDELEO.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 uk 27 kifungu 26(1)(2)
Kila mtu ana wajibu wa KUFUATA na kuitii katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano.
Kila mtu ANA HAKI , kwa kufuata UTARATIBU uliowekwa na sheria KUCHUKUA HATUA za kisheria kuhakikisha hifadhi ya katiba na sheria za nchi.
Tusome Kanuni za Uvccm toleo 2017 uk 18 kifungu 14(b)
Niliwahi kusoma Kitabu Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 175
Mwl JK Nyerere aliwahi kuandika
Hatuwezi kupuuza katiba ndiyo sheria ya msingi , Sheria ZINGINE ZOTE zinatokana na katiba.
Haiwezi kupuuzwa na hatuwezi kuendelea na UTARATIBU wa kupuuza katiba ya nchi yetu.
Niliwahi kusoma Kitabu Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 175
Mwl JK Nyerere aliwahi kusema,
Ufa wa nchi ni kuendesha MAMBO bila KUJALI SHERIA
Wanaccm wenzangu katika Ulimwengu wa KIROHO naonyeshwa vitendo vya UPENDELEO na vya KIBAGUZI vikuendelea.
Katiba ya ccm 1977 toleo 2017 uk 1 - 3 ibara 5 (16)
Kwa hiyo Malengo na madhumuni ya ccm yatakuwa kuona kwamba katika nchi yetu HAKUNA AINA YEYOTE YA Dhuluma, VITISHO , UBAGUZI, RUSHWA , Uonevu , na/ au UPENDELEO.
Tukisoma tena Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 uk 18 Ibara 9(h)
Kwamba aina zote za Dhuluma , vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au UPENDELEO zinaondolewa nchini.
Tukiendelea kusoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 uk 20 ibara 13 (4)(5)
Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu AU MAMLAKA yoyote inayotekeleza madaraka yake CHINI ya sheria yoyote au katika UTEKELEZAJI wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya nchi.
Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno " kubagua"
Maana yake ni kutimiza haja , haki, au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia Utaifa wao , kabila, pahali walipotokea , MAONI YAO YA KISIASA, rangi, dini, jinsia, au hali yao ya MAISHA kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au KUHESABIWA KUWA DHAIFU AU DUNI na kuwekewa VIKWAZO au masharti ya VIPINGAMIZI AMBAPO watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa FURSA au faida iliyo nje ya masharti au sifa za LAZIMA, .
Wanaccm wenzangu katika Ulimwengu wa KIROHO naona UKIUKWAJI WA UTARATIBU WA UINGIZAJI WANACHAMA NA UPOKEAJI WA WALE WANAOTOKA UPINZANI NI MAKWAZO kwa jamii ya Wanaccm WAFIA CHAMA.
Katiba ya ccm 1977 toleo 2017 uk 6 Ibara 8