Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hapo ndipo tunakosea. Yaan CDM mnaona ni chama cha malaika. Hamtaki iguswe kabisa. Ikiguswa tu, anayegusa anatukanwa. Tukienda hivyo hatutafika.

Wakati wa mgogoro na Zitto Kabwe nilifika pale ufipa Kinondoni, nikashuhudia Dr Slaa anamtukana matusi ya nguoni jamaa mmoja ambaye alikuwa mhasibu, kwa madai kwamba anapeleka Siri kwa Zitto.Wakati huo Dr Slaa akiwa katibu mkuu wa chama.

Aikuchukua muda yule jamaa akapigwa sumu, kwenye kilevi. Lakin akapona kwa bahati. Na akakimbia, mbali na CDM. CDM sio malaika, wana mfumo wa sumu kama CCM, hauachi glass ya maji ukaenda msalani.
Nani CDM?
 
Mkuu huyo dada alikuwa kwenye kipindi, na alikuwa anajibu anachoulizwa. Hata hayo ya ccm kaulizwa, na alijibu katika mfumo uleule wa uchawa Ili apate maisha.
Alishindwa vipi kujibu kidiplomasia kwamba asingependa kuzungumzia CHADEMA na maswali yajikite kwenye mambo ya CCM kwa sasa? Wanasiasa wote makini hujikita kuongelea mambo ya vyama vyao na hata kama ni vijembe huwezi kukuta anatamka waziwazi jina la chama kingine. Peneza bado ana akili za kinyumbu.
 
yule dogo ni nyumbu jike
 
TUNDU LISSU ATOA USHAHIDI WA FEDHA CHAFU MBELE YA KAMATI KUU

Leo Tar 11 Kikao Cha Kamati Kuu Kimeketi na Kujadili maswala mbalimbali, Moja ya Agenda Muhimu ilikua ni Swala la Fedha Chafu ambalo liliibuliwa na Makamu Mwenyekiti Bara Mh Tundu Lissu akiwa Iringa wiki iliyopita alipofanya Mkutano wa Hadhara.

Katika Taarifa yake Mbele ya Kamati Kuu, Mh Lissu amedai Alikutanishwa na Abdul Mtoto w Rais kwa Usaidizi wa Mh Wenje Nyumbani kwake Dar Es Salaam. Na Katika Mazungumzo yake ambayo yalirekodiwa alidai amekwenda Kujitambulisha kwake. Pili anataka kudumisha Mahusiano yake kama Mtanzania kwa kuwa anaamini katika Amani na mshikamano. Hatamani uhasama na Mh Tundu. Baada ya Mazungumzo yote alidai ana shukrani kwake ya Kukubali kuongea nae, akasema anaomba kumkabidhi kiasi cha Fedha ambazo Mh Lissu hajataja Kiwango chake. Mh Lissu akahoji kwa nini apewe Peke yake? Mbona tuko wengi? Kwa nini Mimi peke yangu? Ndio Abdul mtoto wa Rais akadai kuwa wenzako tuko nao karibu, tayari mara kadhaa tumezungumza na kuna kiasi wamekubali kupokea na wanapokuwa na Changamoto tunawasiliana. Mh Lissu mbele ya Kamati Kuu akawataja Wajumbe wa Kamati Kuu Watatu akiwemo Wenje Ambae ndio alifanikisha Mpango wa Kukutana na Abduli Nyumbani kwake Tegeta Kujipatia Shilingi Milioni Mia Moja, Mh Heche Ambae alijipatia Shilingi Milion Mia Moja na Hamsini, Mh Peter Msigwa Ambae alijipatia Shilingi Milion Mia Moja, Pia Mh Joseph Mbilinyi ambae kiwango chake hakijatajwa na Mh Lissu. Ushahidi wote wa Mazungumzo yake na Abdul Mh Lissu ameutunza katika Flash Disk ambayo amedai ataikabidhi Kamati Kuu ya Chama.

Katikati ya Mjadala, Mh Peter Msigwa amedai kuwa yeye alipokea kweli na kuambiwa pia Hata Mwenyekiti wa Chama Mh Freeman Mbowe alipokea fedha Kutoka Serikalini bila kutaja ni kiwango gani.

Pia Team ya Usalama wa Chama Chini ya Shetani ilitoa Taarifa Mbele ya Kamati Kuu Kuonesha Mihamala ya Peter Msigwa ambayo imethibitisha uwepo wa Fedha Kutoka Kwa Vigogo Serikalini.

Lissu hana Rafiki kwenye Mambo asiyoyaamini
 
CHADEMA WALA RUSHWA KUMBE HIVI JAMANI HAKUNA CHAMA CHA UPINZANI TANZANIA
 
Hili shtaka mbona Mwikabe Waitara aliliibua akiwa TAMISEMI nakumbuka TAKUKURU walichunguza ila wakaona hakuna ufujaji wa pesa. Same to CAG alifanya forensic audit kwa CHADEMA hiyo 2020 mbona hakupata ushahidi? Hivi JPM alivyochukia upinzani angegundua ufisadi si angekifuta chama kabisa!!
Tindo ana chuki binafsi na mh mbowe, sijui aliwahi kufanywa nini na huyo mzee.
 
Ni kweli mkuu, lakini haipunguzi ukweli wa baadhi ya ayasemayo.
Wewe jamaa umelishwa bangi ya wapi. Yaani mtu akiongea kitu kuhusu mtu usiyemkubali basi automatically kinakuwa cha kweli. Inawezekana na wewe ndio wale wale wa Da Mange kasema.
 
Hapo ndipo tunakosea. Yaan CDM mnaona ni chama cha malaika. Hamtaki iguswe kabisa. Ikiguswa tu, anayegusa anatukanwa. Tukienda hivyo hatutafika.

Wakati wa mgogoro na Zitto Kabwe nilifika pale ufipa Kinondoni, nikashuhudia Dr Slaa anamtukana matusi ya nguoni jamaa mmoja ambaye alikuwa mhasibu, kwa madai kwamba anapeleka Siri kwa Zitto.Wakati huo Dr Slaa akiwa katibu mkuu wa chama.

Aikuchukua muda yule jamaa akapigwa sumu, kwenye kilevi. Lakin akapona kwa bahati. Na akakimbia, mbali na CDM. CDM sio malaika, wana mfumo wa sumu kama CCM, hauachi glass ya maji ukaenda msalani.
Ulichukua hatua zipi kutafuta haki ya huyo aliyewekewa sumu ? Zaidi ya kubwabwaja na ku publish taarifa za uongo mtandaoni.
 
Kwa MTU mwenye akili akishindana na mpenzi wake halafu akahamia kwa mpenzi mpya, hawezi kusema mabaya ya mpenzi wa zamani hadharani.
Tumia akili, je huyo x wako naye akianza kusemamapungufu yako hasa Yale ya ndaaani ndani huko, utapenda.?
 
Amelisemaje?
Kwamba inawezekanaje akina Mdee wamsifie sana mwenyekiti wao kuhusu wao kuwepo bungeni? Cha kushangaza Hadi Mbowe ameonekana na Mdee wakigonga cheers kwenye sherehe fulani. Isitoshe Mbowe kafikia mahali pa kuwaalika akina Mdee kwenye harambee ya kanisa huko kwao Machame. Pia namna kesi ya kina Mdee inavyoendeshwa huko mahakamani ni kama cdm haiko serious na kesi hiyo.
 
Ubavu wake ni mdogo sana dhidi ya Mbowe.

Mbowe ligi yake na vikao vyake ni akina JK.

Hapo wanamsikiliza tu halafu wanacheka huku wakigonga cheers binti akipata taabu aka akitaabishwa na walioko mgongoni mwake halafu kibaya inawezekana hajui hata kwanini analopokwa.
 
Alishindwa vipi kujibu kidiplomasia kwamba asingependa kuzungumzia CHADEMA na maswali yajikite kwenye mambo ya CCM kwa sasa? Wanasiasa wote makini hujikita kuongelea mambo ya vyama vyao na hata kama ni vijembe huwezi kukuta anatamka waziwazi jina la chama kingine. Peneza bado ana akili za kinyumbu.
Kuiponda cdm hadharani ni nguzo kuu ya kupata cheo ghafla ndani ya ccm. Na cheo kinasogea haraka sana iwapo Kuna ukweli Fulani utaongea ambao utaibeba ccm, au kuharibu haiba ya cdm.
 
Najua wewe hapendi Mbowe aeendelee kuwa mwenyekiti wa Chadema. Mbali na hilo , una tatizo lingine binafsi na mh mbowe ?
Mimi sio kwamba sipendi Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa cdm, bali ni sitaki kabisa. Sina tatizo binafsi na Mbowe maana hatujuani kabisa. Mimi namjua kutokana na umaarufu na nafasi yake, lakini mimi hanijui hata kidogo.

Kimsingi kabisa Mimi sio muumini wa kiongozi yoyote wa kuchaguliwa kukaa nafasi Moja kwa zaidi ya miaka Kumi, na sababu hasa ni kuwa kiongozi akikaa zaidi ya miaka 10 kwenye nafasi Moja anaweza kuharibu mazuri, ama kuongoza kwa mizengwe. Mifano halisi ya viongozi hao ninao. Na Mbowe anaangukia kwenye hali hiyo Sasa. Hivyo hili jambo kwangu kwa Mbowe sio personal, bali ni kwa afya ya Taasisi.
 
Back
Top Bottom