TUNDU LISSU ATOA USHAHIDI WA FEDHA CHAFU MBELE YA KAMATI KUU
Leo Tar 11 Kikao Cha Kamati Kuu Kimeketi na Kujadili maswala mbalimbali, Moja ya Agenda Muhimu ilikua ni Swala la Fedha Chafu ambalo liliibuliwa na Makamu Mwenyekiti Bara Mh Tundu Lissu akiwa Iringa wiki iliyopita alipofanya Mkutano wa Hadhara.
Katika Taarifa yake Mbele ya Kamati Kuu, Mh Lissu amedai Alikutanishwa na Abdul Mtoto w Rais kwa Usaidizi wa Mh Wenje Nyumbani kwake Dar Es Salaam. Na Katika Mazungumzo yake ambayo yalirekodiwa alidai amekwenda Kujitambulisha kwake. Pili anataka kudumisha Mahusiano yake kama Mtanzania kwa kuwa anaamini katika Amani na mshikamano. Hatamani uhasama na Mh Tundu. Baada ya Mazungumzo yote alidai ana shukrani kwake ya Kukubali kuongea nae, akasema anaomba kumkabidhi kiasi cha Fedha ambazo Mh Lissu hajataja Kiwango chake. Mh Lissu akahoji kwa nini apewe Peke yake? Mbona tuko wengi? Kwa nini Mimi peke yangu? Ndio Abdul mtoto wa Rais akadai kuwa wenzako tuko nao karibu, tayari mara kadhaa tumezungumza na kuna kiasi wamekubali kupokea na wanapokuwa na Changamoto tunawasiliana. Mh Lissu mbele ya Kamati Kuu akawataja Wajumbe wa Kamati Kuu Watatu akiwemo Wenje Ambae ndio alifanikisha Mpango wa Kukutana na Abduli Nyumbani kwake Tegeta Kujipatia Shilingi Milioni Mia Moja, Mh Heche Ambae alijipatia Shilingi Milion Mia Moja na Hamsini, Mh Peter Msigwa Ambae alijipatia Shilingi Milion Mia Moja, Pia Mh Joseph Mbilinyi ambae kiwango chake hakijatajwa na Mh Lissu. Ushahidi wote wa Mazungumzo yake na Abdul Mh Lissu ameutunza katika Flash Disk ambayo amedai ataikabidhi Kamati Kuu ya Chama.
Katikati ya Mjadala, Mh Peter Msigwa amedai kuwa yeye alipokea kweli na kuambiwa pia Hata Mwenyekiti wa Chama Mh Freeman Mbowe alipokea fedha Kutoka Serikalini bila kutaja ni kiwango gani.
Pia Team ya Usalama wa Chama Chini ya Shetani ilitoa Taarifa Mbele ya Kamati Kuu Kuonesha Mihamala ya Peter Msigwa ambayo imethibitisha uwepo wa Fedha Kutoka Kwa Vigogo Serikalini.
Lissu hana Rafiki kwenye Mambo asiyoyaamini