Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
We jamaa una chuki sana na Mbowe sijui alikufanya nini.
Wewe ni miongoni mwa wanachadema wachache wanaofurahia Mbowe akitukanwa hadharani kwa tuhuma ambazo hazijawahi thibitishwa.
Unadhani kwa kufanya hivyo ndiyo utaonekana objective humu Jamii Forum.
Acha hizo.
Naona unachanganya chuki na misimamo yangu. Tafuta popote ninapomtukana Mbowe, hadi useme nikiona anatukanwa napata faraja. Suala la Mimi kutokubaliana na kiongozi yoyote kukaa madarakani zaidi ya miaka 10 ni la principle zaidi. Kwenye hili sihitaji support ya yoyote, au kukubalika kwa yoyote.
 
Asingeweza; hakuwa na mamlaka hayo. Teknik ya hayati JPM ya kuufuta upinzani ilikuwa ni utendaji kazi uliotukuka, uliokuwa unapelekea wapinzani wahame wenyewe kutoka upinzani kurudi CCM
Katafute mjinga wa hivyo, ama unadhani hatukuona kipi kulikuwa kinaendelea kwenye ile hadaa ya kuunga mkono juhudi?
 
CHADEMA wavumilie kwasababu wao ndo wamemfundisha huyo Peneza matusi. CHADEMA ni chama kikuu cha matusi. Acha Peneza awape dawa.
Kwani ametukana wapi? Au kwakuwa kusema ukweli huko ccm kunachukuliwa kama matusi? Naona unalazimisha dhana zako kufit inn kwenye mahojiano ya Upendo.
 
Dada anafunguka vibaya huko clouds FM kuhusu mambo ya cdm. Anamuanika Mbowe hadharani.
Haya mambo ni ya kizamani mno. Haya mambo ya kutoka chama A na kukishambilia baada ya kutoka yalikuwa yanashangiliwa wakati wa ile miaka ya akina Mkapa. Mimi mtu hawezi kukaa kwenye chama kwa muda mrefu tu halafu atoke aanze kusema ubaya wa chama wakati muda wote alikuwa huko.
 
Mbowe yupo kibiashara zaidi. Ndio maana, hataki kuachia uenyekiti. Yupo hiari haya mambo ya CCM na ufisadi wao uendelee, huku yeye anaendelea na biashara yake ya ruzuku na wabunge.

Yaan akipata wabunge let say 100.Kila mbunge akatoa one million kwa mwezi, ni 100,000,000 kwa, mwezi. Kwa mwaka anapata 1.2 billion. Kwa five years anapata 6 billion. Kwann atoke kwenye uenyekiti??? Hapo bado ruzuku ya 2 billion.
Kwanini Mbowe anakutumia sana kuliko sisi wewe chama, huoni uo ni ujuha, Mbowe washikilie hapo hapo,
 
Alichoongea Peneza ni upuuzi mtupu. Kwa mfano kasema kuwa alikuwa mdogo na CHADEMA walikuwa hawampi nafasi ya kwenda naye kwenye mikutano ya operesheni Sangara ila akawa anafosi hadi kwenda huko kwa kujilipia mwenyewe. Kimsingi unaona hapo CHADEMA hawakuwa na kosa kubebabana na binti mdogo kwenye harakati zao ambaye anatakiwa awe chini ya uangalizi wa wazazi. Peneza anadhihirisha tabia yake mbovu aliyokuwa nayo kwa muda mrefu. Mimi ni mwanaCCM damu ila Peneza hana maadili kabisa.
Hongera unajitambua
 
Hawezi kuwa anaongea ya uongo yote. Suala la Mbowe na kina Mdee amesema kweli.
Hapa sasa.
Ningejuwa kaongea nini juu ya hili, nadharia yangu ingekamilika kabisa. Kwa bahati mbaya sipo karibu na 'CLOUDS' kwa sasa.

Ungetoa mstari mmoja tu, alichosema juu ya hili, ingesaidia sana mkuu 'Tindo'.

Mbowe alishafanya makubwa sana ndani ya CHADEMA, ambayo yangempa heshima kubwa katika historia ya chama hicho na Tanzania kwa ujumla.
Kuendelea kung'ang'ania kuwa kiongozi wakati huu, kutamwondolea sifa zote, na huenda akakiua chama chenyewe.
 
Uzi umeenda mbali huu, kuna post yangu humu humu nimeweka alichosema kuhusu hilo. Ila anaonyesha shaka ya dhahiri kuhusu Mbowe na Mdee Hadi kufikia kualikana binafsi kwenye sherehe, na michango madhabahuni. Kikubwa ni mwenendo wa cdm kwenye kesi ya hao COVID 19.
 
Nautafuta "mchango huo."
Lakini usisahau pia kutapatapa kwa CCM wakati huu tukielekea chaguzi muhimu. Watatumia kila uchafu; hata kuua wakiweza, ili waendelee kutuweka mateka wao.
 
Amesema kuhusu pesa walizokuwa wanachangishwa wao kama wabunge, hawafahamu zimetumika kufanya Nini. Na ni kweli hizi pesa zimekuwa zikitolewa porojo. Huyu Upendo kwakuwa ana hasira ataongea mengi ya hasira, lakini humo ndani tutapata ukweli.
Aangalie hasira zisije zikamuharibia future yake. Sijamsikiliza kwa kweli ila sijui kama alishawahi kuuliza kwenye vikao vyao kwa kuwa nae alikuwa kiongozi mkubwa tu. Au kwa sababu alkkuwa ndani aliogopa kutingisha ndevu za boss.
 
Back
Top Bottom