Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

Kwahiyo unataka tutoke kwenye mjadala kitaifa turudi kwenye mjadala wa kichama ?
Nambie ni kitu gani ambacho kinawanufaisha wao halafu ni maumivu kwa mwananchi walishawahi kukipinga kwa dhati???
 
Kwa vyovyote kwenye uchaguzi huwa tunachagua story lakini story inayoeleweka na kutekelezeka.

Kama mtu katupigia story miaka 50 na bado tunamwamini huoni kosa ni la kwetu wenyewe kuamini uongo ule ule kwa miaka nenda rudi ?
Hata sioni kosa letu, tunaporwa haki zetu ndio sababu, "chama dola" hakina jipya tena.
 
Mbona hujafungua code umeona nini?

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Waliompenda Magufuli ni hasa wale wenye maisha duni? Nikuhakikishie JPM alipendwa na watu wa kada zote, walio duni na wasio duni pia. Ieleweke kwamba hulka ya binadamu ni complex huwezi kumtathmini binadamu kwa vigezo rahisi rahisi kama uwepo wa mzunguko wa hela mtaani. Hakuna viongozi waliokuwa easy-going na walioachia hela mtaani kama Mwinyi na JK, lakini kuna sehemu ya watanzania inawaona kama miongoni mwa viongozi wabovu kuwahi kuiongoza Tanzania. Kinyume chake JPM amependwa na watanzania takribani asilimia kubwa kwa sababu zingine zinazogusa mioyo ya watu. Kuna mambo ya msingi yanayogusa mioyo ya watu zaidi ya pesa, na ni kama vile JPM aliyajua, na ndiyo maana huku mtaani watu wengi wanaamini JPM ni kiongozi bora kabisa wa nchi yetu kupata baada ya Nyerere.
 
Sema Sababu inajulikana Tz iko na wapumbafu wengi yaani Leo
mBunge wa ccm awe mtetezi wa wananchi badala ya cccm yake na watu wanamuamini

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Ukimkosoa Mama kwa hoja hana ujanja wowote , pamoja na yote huyu ni miongoni mwa walioharibu Katiba mpya hadharani na gizani , faili lake lipo , tunamwangalia tu atakachofanya
Watu wanataka kujificha kwenye kichaka cha uanamke ikiwa mwenyewe kasema hakuna ubongo tofauti Kati ya mwanamke na Mwanaume kinachotakiwa mama afanye kazi afuate sheria zaidi ya hapo atapwaya

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Huu ndio ukweli

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Nambie ni kitu gani ambacho kinawanufaisha wao halafu ni maumivu kwa mwananchi walishawahi kukipinga kwa dhati???
Hili swali nimeshakujibu kule juu labda kama umeishiwa maswali mengine ya kuuliza useme.
 
Shukrani sana kwa hii comment unajua kuna watu hawataki kuamini kwamba Nchi hii bado iko na wajinga wengi wasiojua nafasi zao

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Sawa kinachotakiwa ni hoja kinzani itoke ndani au nje sawa tu. Na mtu ambaye si mbinafsi atasaidia upinzani ukue na unaweza kukua pia.
Watanzania kwa ujumla waowanatakiwa kufahamu hili kwa faida ya nchi na sio kundi...
 
Uko vizuri Mkuu na ushahidi wa hili ni UPORAJI wake wa uchaguzi.
Watu tunamfurahia Mama kwa sababu Tulishamchoka MAGUFULI na Siasa zake za kikatili,
Ukweli ni kwamba CCM imechokwa kuliko kitu chochote duniani.
Kama mtoa mada anaamini Mama anapendwa waruhusu Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.

Nakuhakikishia Samia hawezi kwenda kinyume na matakwa ya CCM,na moja ya takwa kubwa la CCM Ni dhuluma kwa kila Jambo.

Mama mtago wake Ni mdogo tu,ama awe upande wa CCM ama awe upande wa wananchi.

Ikiwa Kikwete mwanasiasa nguli ndani ya CCM walimdhibiti suala la Katiba mpya ingawa yeye ndio alielianzisha likamshinda na heshima yake ikashuka sembuse Mama mchanga katika Siasa?

Kama CCM wanajiamini kuwa mama anapendwa waruhusu Katiba na Tume ili chaguzi ziwe za haki waone mziki wa Upinzani.
Mimi nimeichoka CCM katika maisha usione hivi,hata wanipe Lori la fedha ntawasaliti tu.
 
Unawashaurije Chadema wanapoambiwa wapeleke Hoja zao kwa Shibuda

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Umeongea ukweli..japo sina wasiwasi. Upinzani upo na watu smart sana kama Mbowe
Wakati Magufuli anaingia madarakani tulisikia maneno Kama haya,kuwa Sasa upinzani umekufa na akapewa kila Jina,Tingatinga,mtumbua majipu,mbadala wa Nyerere,kiboko ya mafisadi n.k
Amekufa kaitwa kila Jina baya hapa duniani,Hadi watu wanatamani kwenda kujisaidia juu ya kaburi lake.

Kwa kifupi pamoja na viongozi wake lakini ukweli Ni kwamba CCM imechokwa.

Mama anafurahiwa tu kwa sababu mkatili Magufuli kaondoka.Lakini mama Hana jipya Ni Kama akina Kikwete tu na Mwendazake wote Ni CCM.
 
Waliokuwa wanalalamika sauti zao ziliishia kwenye kibuyu ila sauti za wapambe zilienea kote. Ni watu wachache walipata kujua pande mbili za shilingi. Watu waiokuwa wamechoshwa ni wale waliokua na fursa ya kujua ukweli na kuutafuta na kuuchambua. Wanafiki wenye uelewa walitikisatikisa tu mikia yao hawakuthubutu kubweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…