Urusi ni nchi ya kijamaa? Mbona ina vyama vingi (Multipartism) tofauti na China??

Vyama vya upinzani vipo vingi tu huko Urusi, japo vimeminywa.
 
Vyama vya upinzani vipo vingi tu huko Urusi, japo vimeminywa.
Kwanini Russia sio kama China ingawa wote ni wajamaa?? Ulishawahi kusikia Wachina wanapiga kura ya kumchagua Rais??
 
Presidential election ya China imekaaje mkuu??
Presidential election ya China haina maana yoyote Rais wa China ni kama ceremonial figure tu nguvu ipo kwa chama cha kikomunisti katibu mkuu wa China ndio mara nyingi ni paramount leader japo sio mara zote ukiwa na nguvu ndani ya chama cha kikomunisti za kiushawishi haiitaji hata uwe Rais au Katibu mkuu unaweza kuwa kiongozi mkuu wa China bila vyeo hivyo mfano alikuwa Deng Xiaoping.

Haya Rais wa China anachaguliwa na bunge la watu wa China wajumbe wana hiyo nafasi ni kama uchaguzi wa waziri mkuu katika nchi zinazo tumia Parliamentary democracy
 
Ulishawahi kusikia Wachina wanapiga kura kumchagua Rais??
Unaweza usiisikie hivyo lakini anachaguliwa na majority indirect kupitia uchaguzi wa wajumbe waliochaguliwa na wananchi nao wanafanya uchaguzi wa Rais.

Rais wa China anachaguliwa kutoka chini kwenda juu.

Ni kama leo Tanzania wabunge ndio wawe wanachagua Rais
 
Kwanini Russia sio kama China ingawa wote ni wajamaa?? Ulishawahi kusikia Wachina wanapiga kura ya kumchagua Rais??
Russia sio wajamaa unachanganya Russia na USSR
 
Mfumo wa kidemokrasia una uhusiano gani na economic ideology?
Inawezekana kuwa na kimoja bila kingine au kuwa navyo vyote.
 
Ukweli mchungu huu. Safi sana.
 
Fact ni kwamba ujamaa ni mfumo wa kiuchumi na vyama vingi ni mfumo wa kidemokrasia, mfumo wa upatikanaji wa viongozi. Ujamaa unaweza kulinganishwa na ubepari(capitalism).
Mfano: China ni mixed capitalism ya chama kimoja. Yaani Capitalism inaweza kuishi ndani ya chama kimoja au Vyama vingi vikaishi ndani ya ujamaa.
 
Kuna zile zilikuwa tegemezi kwa nyingine kama Tajikistan na Kyrgyzstan.
 
Navyoelewa Medvedev aliwekwa na Putin kuwa Rais kama zuga tu. Putin alimpisha Medvedev kuwa Rais, muda wake ulipoisha akarudi tena kuwa Rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…