Nikiwaambia watu Russia ni superpower uchwara wanabisha. Nataka kumtag Bwana Utam ila sioni username yake, nisaidieni anatumia jina gani nimwambie atoke mafichoni.
Russian Army ni kama imepooza bado, response ndogo sana na speed ya kinyonga. Airforce ndio inapambana sababu inaweza respond mapema.
Wakati hapo Moscow hakuna heavy weapons ziko uko Western parts, ambayo ndiyo Urusi inaamini itavamiwa na NATO. Mji mkuu hauwezi pewa silaha nzito sababu majenerali wa hapo wanaweza fanya mapinduzi, silaha zipo pembezoni uko mkitoka nazo kufanya mapinduzi serikali inajipanga kwa masaa au siku kadhaa mpaka mfike mji mkuu itakuwa ishaita units nzito za upande mwingine wa nchi.
Silaha muhimu zilizopo Moscow ni anti ballistic missile systems, silaha nyingi sana za kupambana na maandamano na askari wengi watuliza ghasia na kamatakamata wale kina OMON.
Wagner ingeteka zaidi eneo la magharibi, ila Moscow sio kwamba ipo katikati sana ya Russia. Iko kama magharibi nayo, St. Petersburg inaweza kuwa capital ya muda kama Moscow itakuwa na fujo. Na command jets zinaweza ruka angani, ile Antonov iliyodunguliwa leo ni ya mawasiliano na intelligence, likely ilikuwa inafanya isolation na kusikiliza kutengeneza coordinates za simu kupata Prigozhin yuko wapi ili afanyiwe precision strike ya makombora. Najua Prigozhin anajua hizi mbinu, sio muda muafaka wa yeye kutumia TEHAMA. Kina Putin hawaoni shida kutuma tactical ballistic missile hata wakifa thousands, who cares maana watu wenyewe washakuwa waasi.