Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Urusi Imetudhalili sana Kama Ndio hivi mamluki anasonga kama mlenda kwa ugali duh....Hivi hii nchi kumbe haikua na chochote ni mkwara mbuzi tu....Sasa Putin na jeuri yake si atakua anazimia huko...Najisikia aibu sana mashoga yanaiangusha Urusi dah

Marekan ni noma, hawa Mbwa wanaenda kumuweka papeti wao Urusi, kazi kwisha
 
Sisi waislamu tunawaona mayahudi ni wabaya kuliko wakristo.La kushangaza wakristo wengi wanawaona ni ndugu zao kuliko waislamu.
Ami ukirsto umezaliwa ndani ya uyahudi na uyahudi ni dini mama ya ukrsto,hivyo adui wa wayahudi ni adui wa wakrsto...Kwakua wakrsto hawawapendi waarabu ambao ni mahasimu wa wayahudi basi hawawezi kua na undugu na dini iliyoanzishwa miaka 700 au zaidi baada ya ukristo na yenye tamaduni za kiarabu mahasimu wa wayahudi
 
Lazima kuna watu wengi wapo nyuma ya Wagner. Anajua kabisa akiingia Moscow, mengi yatatokea. Putin amekwishahisi Urais wake unatafutwa. Kwenye hotuba yake amesema kwamba watu wanafanya maasi kwaajili ya tamaa ya madaraka.
Yeye mwenyewe hapo anajisema.Kisa cha kubadili katiba ni nini?Kama si tamaa ya madaraka ili awe Rais wa maisha.
 
Kuna watu hawajui PMC hawawezi kusonga mbele maana hawana ndege vita hawana baadhi ya ammunition walizokuwa wanapewa na Jeshi. Hivyo cant fight RF.
Unahisi hayo maaamuz ni yao binafs mbona huwa mnafikir harib sana , kwamba wamekurupuka sio?
 
1. Mpaka hiyo coup itokee na ifanikiwe....
2. Na tofauti zao zote wanachofanana ni kitu kimoja, they all hate the West.
3. Unclear mpaka sasa nini kinaendelea, sababu hakujawahi na Coup ya hivi duniani ( nilizofanikiwa kuzisoma).
This is the takeover, ni revolution. Alafu sio lazima kila kitu kiwe sawasawa na kilichotokea miaka iliyopita, historia inajirudia lakini haikopi na kupesti.

Wote wanaichukia West na West haina mpango nao, they are weak. USSR ilikuwa inawachukia West ikavunjika, Russia ikabaki na chuki kwa West ila ikawa dhaifu hivyo haikufanya kitu. Si ni Marekani hiihii ilitoa hela ili Russia ipunguze silaha za nyuklia, si Marekani hii iligharamia kuharibu na kurudisha Russia zile nukes za Ukraine. Soon utaona Marekani inamwaga mkataba na wanachekeana kwa muda, mgeni atakaribishwa mpaka aje kuota meno waanze na moja Western watakuwa wamesogeza siku
2007-06-02_bush_putin_515.jpg


Russia ilitulia ilivyokua kidogo ikatunisha mabega, badala ifanye uwekezaji mkubwa na kuvutia biashara, research, development, miundombinu, teknolojia, manufacturing na mengine yenyewe ikaendelea na kujitutumua kijeshi tu. Sasa ikiwa weak zaidi ya hapa na chuki yake dhidi ya West itakuwa haifanyi chochote
 
Sawa Mkuu
Binafsi naona ni njamaa, maana kabla ya hapo wamekuwa na mgogoro mkubwa sana.

Wagner walimalalamikia kuwa jana Shoigu aliwapiga mabomu, hivyo Wagner wakasema wanaenda mfata Shoigu na mwenzake.

Maajabu walipofika mpakani wakaachwa wakapita hadi makao makuu ya jeshi, wakapateka.

Putin akatangaza kuwa Wagner wamechagua njia isiyo sahihi hivyo wauawe
, Baada ya hapo Wagner imebidi liwalo na liwe ndo maana wakaanza enda Moscow

Cha ajabu hawajashambuliwa hadi wanakaribia Moscow

Na viongozi wengi wameondoka
 
Ni kawaida ukimtumia mtu kuua watu usipomuwahi ukamuua yeye ipo siku atakugeuka.
Yes, hii mbinu aliitumia muasisi wa kampuni yetu. Kabla ya kumkabidhi u-CEO bwana Ben ten alimtuma shushushu akamchimbe Ben ten, ndio mwamba akagundua kuwa Ben 10 aliwah kumRIP jamaa flan kwa wivu wa mapenzi.

Then muasisi akamuita Ben 10 nakumpa file lake, jamaa hakuamini kama jinsi watu walivyochimbua makaburi yake, so muasisi baada ya kumkabidhi u CEO Ben ten akamwambie mtu fulani ndio ameleta hilo file so anza nae maana kwakua anajua huo upuuzi wako atakusumbu... Soon baada ya kukabidhuwa kampuni AKAMRIP mwamba...
 
Huyu Prigo siyo mtu wa mchezo. Siyo kichaa, anajua anachokifanya.

Kwanza analijua kikamilifu jeshi la Urusi, anazijua silaha za Urusi, anajua akiba ya silaha za Urusi, anajua msimamo wa wananchi walio wengi. Na kwa vyovyote vile atakuwa ana mawasiliano na baadhi ya makamanda wa jeshi la Urusi na wapiganaji pia.

Putin anaweza kujiona bado ana askari wengi, kumbe siyo askari wake. Ikumbukwe toka mwanzo, askari wa jeshi la Urusi, licha ya kuwa na silaha nyingi, kikubwa walichokuwa wamekikosa ni morali.

Ufahamu kuwa ndani ya hilo jeshi la Urusi, wengi ambao wamekuwa wanapelekwa mstari wa mbele, ni askari wasio na mafunzo ya kutosha. Ni wale walioandikishwa na kulazimishwa kwenda vitani. Na hilo lilifanyika baada ya Urusi kupoteza askari wake wengi elites mjini Kiev, na siku za mwanzo za mapigano kusini mashariki mwa Ukraine, vifo vilivyohusisha makamanda wa ngazi ya juu wa Jeshi la Urusi.

Askari hao wote wanaona kabisa kuwa maisha yao yapo hatarini kwa kuendelea kupigana nchini Ukraine. Kwao ni rahisi zaidi kupigana dhidi ya Serikali yao kuliko kuendelea kupigana Ukraine ambako nchi za Magharibi wameapa kuendelea kuisaidia Ukraine, hata kama vita itachukua zaidi ya miaka 10.
Kuweni na akiba ya maneno msije kulikimbia jukwaa.
 
Back
Top Bottom