Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Eti wanaweza kuchukua nchi ya Urusi, we umerogwa.
Kwa hali halisi ilivyo nchini Urussi hivi sasa, Wagner PMC wanaweza wakapindua utawala wa Putin, uwezo huu wanao kabisa. Kumbuka, hata Ukraine na NATO, hususani utawala wa Marekani na Uingereza wanaweza wakawatumia Wagner PMC katika mission ya kuzima vita ya Urussi nchini Ukraine pamoja na kuudhoofisha utawala wa Putin. Aidha, Wagner PMC wanaweza kupata msaada wa kijeshi kutoka Ukraine na Nato (In short, DEVIL'S ADVOCATE THEORY itafanya kazi yake hapa).
Vile vile, wananchi wa kawaida wa Urussi ambao ndugu zao wamefia vitani Ukraine au ambao wanauchukia utawala wa Putin watawaunga mkono Wagner PMC hali ambayo itaudhoofisha zaidi na zaidi utawala wa Urussi hali ambayo inaweza kufanya nchi ya Urussi kuvunjika na watu kujitenga Kisha kuanzisha nchi zao kama ilivyomeguka Shirikisho la Urussi la zamani USSR.
 
Wapiganaji wa Wagner waelekea Moscow kuuondoa utawala wa kijeshi unaoongozwa na SERGEI SHOIGRU. Kiongozi wa Wagner anadai kwamba majeshi ya urusi yamekuwa yakishambulia kambi zao nchini UKRAINE.

Huu Uzi nitatoa update ya kila kinachoendelea.

=====
Update: Maafisa wa Ukraine wasema watatumia 'mapinduzi ya kijeshi' nchini Urusi kurejesha eneo lililochukuliwa

Katika tishio moja kwa moja kwa mamlaka ya Putin, Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa Wagner, aliishutumu jeshi la Moscow kwa kupiga bomu askari wake na kudhibiti jiji muhimu la Urusi mapema asubuhi.

Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali wa jeshi binafsi maarufu zaidi ulimwenguni aliahidi kwenda kwenye mji mkuu kwa kulipiza kisasi.

Katika hotuba isiyokuwa ya kawaida, Bwana Putin alilitaja tukio hilo kuwa "uhaini" na akasema wale wanaounga mkono vitisho na njia za kigaidi watapata adhabu isiyoweza kuepukika.

Rais wa Ukraine, Zelensky, alivunja ukimya na kusema kuwa hii ni mfano mwingine wa "udhaifu kamili wa Urusi".

=====

Mamlaka katika eneo la Lipetsk nchini Urusi waagiza watu kubaki nyumbani

Mamlaka katika eneo la Lipetsk nchini Urusi walitoa wito kwa watu kubaki ndani ya nyumba zao kwa sababu za usalama.

Walitoa onyo hilo kutokana na ripoti kuwa wapiganaji wa Wagner walikuwa wakitumia eneo hilo wakati wa safari yao kuelekea Moscow.

=====

Wagner wateka makao makuu ya jeshi la Urusi ukanda wa Kusini
Gavana wa Voronezh, nchini Urusi alisema Jumamosi kuwa huduma za dharura zilikuwa zikijaribu kuzima tanki la mafuta linalowaka katika kituo cha mafuta.

Zaidi ya askari zimamoto 100 na vifaa 30 vya kuzimia moto walikuwa wakifanyia kazi katika eneo hilo, alisema Gavana Alexander Gusev kupitia Telegram.

Awali Jumamosi, chanzo cha usalama nchini Urusi kiliiambia Reuters kuwa wapiganaji wa Wagner walidhibiti vituo vya kijeshi katika jiji la Voronezh, umbali wa kilomita 500 (maili 310) kusini mwa Moscow. Reuters hawakuweza kuthibitisha madai hayo.
=====

NDEGE YA RAIS YADAIWA KUONDOKA MOSCOW, WAGNER WAKIDAIWA KUKARIBIA MJI

Inadaiwa Wapiganaji wa Wagner wameendelea na mapambano na sasa wamefika katika Mkoa wa #Lipetsk, takriban Kilometa 450 kutoka Moscow

Aidha, inaelezwa kuwa Ndege za Kivita za Urusi zimeshambulia misafara ya Wapiganaji wa #Wagner na tayari Wanajeshi wameshajipanga katika nafasi za kuulinda Mji Mkuu, Moscow

Kiongozi wa Wagner, Yevgeny #Prigozhin amedai kuwa Wapiganaji wake wamepokelewa kama 'Wakombozi' na kuwa waliweza kuchukua Makao Makuu ya Kijeshi huko #Rostov bila mapigano

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa Ndege ya Rais imeonekana kuondoka #Moscow, hata hivyo Ikulu imedai kuwa Rais #Putin bado yupo katika Mji Mkuu huo
Mpaka sasa hivi wamesharudisha eneo gani?
 
Link ya Ukristo na waisrael wa Leo ni ipi?
Link ipo mkuu ukrsto upo ndani ya uyahudi sababu umetokana na uyahudi havitengani.Na hakuna waisrael wa leo hizo ni propaganda za waarabu kutaka kusema kua leo hii pale israel wale sio vizazi vya wayahudi...Wayahudi ni wale wale miaka yote popote pale walipo duniani.....Ni sawa na kuuliza link ya farao wa misri wa wanubi na wakushi wa ethiopia kabla ya uvamizi wa waarabu maeneo ya mto nile...Baadae wakasema mafarao walikua waarabu
 
Kama kuna support Wagner watapata basi ni kutoka Russian nationalists ( who are more hostile towards Ukraine).
Hakuna happy ending Upande wa Ukraine.
Huo muda wa Russia kupigana kumaliza then kuja kuipiga Ukraine wanautoa wapi. Unakumbuka October revolution ya 1917, Russia ilipojitoa WW1 baada ya kupigwa na Bolsheviks walipochukua nchi hawakuendelea na vita tena. Walitumia muda wao kupigana wenyewe kwa wenyewe, kupigana na remnants za serikali iliyopita na kujiimarisha utawala wao.

Muda hauruhusu hao nationalists kupigana na Ukraine. Sababu ikitokea Putin hayupo kutakuwa na pro-Putins, nationalists na Wagners na washirika wao watakaoasi jeshini na usalama. Hapo Ukraine itarudisha maeneo mengi sana, itahitajika nguvu kubwa zaidi kupigana nayo kuliko walivyoanza au wanavyoendelea sasa. Serikali itakayoundwa na kudi lolote kati ya hayo matatu ikitumia nguvu kuingia Ukraine inayaachia makundi mawili mwaya wa kujijenga.

Kawaida ya coups au mutiny hufuatia counter-coups kama msipoelewana. Russia haina watu wenye nguvu na popular, Putin aliwaondoa. So akijitokeza mwenye ushawishi na nguvu akaungwa mkono atakuwa ndio anaanza na moja huo muda wa kuifikiria Ukraine hana.

Russia kuna factions na ubaguzi, mfano huyu Shoigu ndio kabisa hawezi waambia lolote. Mtuva mwenye asili ya Asia kutoka mji wa vichochoroni uko anawaambia Western Russians wa St. Petersburg na Central Russians wa Moscow. Ndio sababu Chechens walianzisha zile vita mbili, ukiwa wa mashambani uko kwenye ngano hakuna anayekuthamini. Shoigu kawekwa pale sababu hawezi ungwa mkono hivyo hawezi fanya mapinduzi.

Waziri Mkuu yule Mishustin kapoa kama uji wa mgonjwa, Kadyrov ni wakuja hawaambii kitu Warusi halisi, Dmitry Medvedev ni pro-Putin ila mnyonge na dhaifu mbele ya vyombo vyote, Dmitry Rogozin ni mwehu fulani anaweza leta chokochoko ila tangu HIMARS zimshambulie kwenye birthday party mwaka jana sijamsikia tena sijui operation aliyofanyiwa ilimuacha hali gani. Hapo juu anabaki mtu mmoja tu, mkuu wa usalama wa taifa ambaye inasemekana ndio alikuwa anaandaliwa kuwa mrithi wa Putin.

Atakayepita hapa itabidi aue vigogo kadhaa (hii itafanyika 100%, that's how Russia exist). Au yeye mwenyewe anaweza uwawa, mfano Prigozhin sio presidential material hata kidogo. Then uhamisho, kustaafisha watumishi muhimu, exiles, asylums, kuvunjika kwa baadhi ya organs za jeshi, polisi na usalama na mengine yatafanyika.
Ikiwa Putin atabaki tutarajie mabadiliko machache ila mauaji mengi na nadhani hatotaka kuendelea muda mrefu atawaachia msala usalama kama ambavyo Godfather wake alivyomuachia.
 
Wanajeshi zaidi ya laki 4 wa Urusi wameweka vizuizi 1800 katika barabara inayoelekea mji wa Moscow. Kila kizuizi kimoja kina wanajeshi zaidi ya 300 wa Urusi ili kuwazuia wapiganaji wa Wagner kufika Moscow. View attachment 2667541
Mkuu upewe maua yako, unatoa updates kwa video kabisa. Source yako ni ipi? Naona kama nachelewa kupata updates za huu mtanange.
 
Back
Top Bottom