Kama kuna support Wagner watapata basi ni kutoka Russian nationalists ( who are more hostile towards Ukraine).
Hakuna happy ending Upande wa Ukraine.
Huo muda wa Russia kupigana kumaliza then kuja kuipiga Ukraine wanautoa wapi. Unakumbuka October revolution ya 1917, Russia ilipojitoa WW1 baada ya kupigwa na Bolsheviks walipochukua nchi hawakuendelea na vita tena. Walitumia muda wao kupigana wenyewe kwa wenyewe, kupigana na remnants za serikali iliyopita na kujiimarisha utawala wao.
Muda hauruhusu hao nationalists kupigana na Ukraine. Sababu ikitokea Putin hayupo kutakuwa na pro-Putins, nationalists na Wagners na washirika wao watakaoasi jeshini na usalama. Hapo Ukraine itarudisha maeneo mengi sana, itahitajika nguvu kubwa zaidi kupigana nayo kuliko walivyoanza au wanavyoendelea sasa. Serikali itakayoundwa na kudi lolote kati ya hayo matatu ikitumia nguvu kuingia Ukraine inayaachia makundi mawili mwaya wa kujijenga.
Kawaida ya coups au mutiny hufuatia counter-coups kama msipoelewana. Russia haina watu wenye nguvu na popular, Putin aliwaondoa. So akijitokeza mwenye ushawishi na nguvu akaungwa mkono atakuwa ndio anaanza na moja huo muda wa kuifikiria Ukraine hana.
Russia kuna factions na ubaguzi, mfano huyu Shoigu ndio kabisa hawezi waambia lolote. Mtuva mwenye asili ya Asia kutoka mji wa vichochoroni uko anawaambia Western Russians wa St. Petersburg na Central Russians wa Moscow. Ndio sababu Chechens walianzisha zile vita mbili, ukiwa wa mashambani uko kwenye ngano hakuna anayekuthamini. Shoigu kawekwa pale sababu hawezi ungwa mkono hivyo hawezi fanya mapinduzi.
Waziri Mkuu yule Mishustin kapoa kama uji wa mgonjwa, Kadyrov ni wakuja hawaambii kitu Warusi halisi, Dmitry Medvedev ni pro-Putin ila mnyonge na dhaifu mbele ya vyombo vyote, Dmitry Rogozin ni mwehu fulani anaweza leta chokochoko ila tangu HIMARS zimshambulie kwenye birthday party mwaka jana sijamsikia tena sijui operation aliyofanyiwa ilimuacha hali gani. Hapo juu anabaki mtu mmoja tu, mkuu wa usalama wa taifa ambaye inasemekana ndio alikuwa anaandaliwa kuwa mrithi wa Putin.
Atakayepita hapa itabidi aue vigogo kadhaa (hii itafanyika 100%, that's how Russia exist). Au yeye mwenyewe anaweza uwawa, mfano Prigozhin sio presidential material hata kidogo. Then uhamisho, kustaafisha watumishi muhimu, exiles, asylums, kuvunjika kwa baadhi ya organs za jeshi, polisi na usalama na mengine yatafanyika.
Ikiwa Putin atabaki tutarajie mabadiliko machache ila mauaji mengi na nadhani hatotaka kuendelea muda mrefu atawaachia msala usalama kama ambavyo Godfather wake alivyomuachia.