Mimi siku zote nitaendelea kumtetea mzee Shoigu. Ni mtu mtulivu asiye na mambo mengi na hana madhambi mzee wa watu.
Prigozhin inawezekana hakushambuliwa kabisa kabisa, alitafuta justification. Na kwa sababu Urusi ni nchi ya uongo na propaganda kila mmoja anajua kuzitumia vizuri na kutengeneza.
Prigozhin aliona aibu kumtaja Putin moja kwa moja, pia aliona upinzani unaweza kuwa mkali. Akaona aanze na kumtaja mzee Shoigu asiye na makuu, then makamanda wa jeshi watapunguza makali kidogo alafu taratibu asome upepo amtaje Putin. Vilevile Prigozhin alijua fika akimfuata Shoigu atamlazimisha Putin kutoa tamko la kumzuia na kutaja maneno fulani ambayo atayatumia dhidi yake, ikawa hivyo naye akakwepa aibu ya direct. Nikikuita wewe mjinga alafu ghafla ukanivamia na kunipiga kipigo kikali huku unatamka "mjinga nani?" kuna uwezekano ulikuwa unanitafutia kisa.
Cha ajabu anayeongoza msafara wa Wagner kwenda Moscow ni huyu jamaa mwenye alama za Nazi mabegani. Russia tuliwaambia Nazis wanao wenyewe nchini wako wakashupaza shingo, wakawa wanataja sababu uchwara za denazification na demilitarisation ndani ya siku tatu. Kumbe sasa imekuwa Nazification of Russia ndani ya siku ngapi hizi
View attachment 2667661