Mzee alichokifanya Putin kwa Rais/mwanadamu yeyote mwenye akili timamu angekifanya.
Kuna maamuzi/matendo ambayo mazingira na nyakati huyafanya yawe ya kishujaa au ya kipumbavu.
Hakuna mtawala yeyote timamu anapenda maandamano au mapigano yafanyike kwenye ardhi yake hata kama ana jeshi imara kiasi gani sababu huathiri shughuli zote za kimaisha lakini hatari zaidi huwezi jua mwisho wake utakuwaje. Pia uasi mara nyingi huwezi jua wahusika na scale yake ikoje. US na ubabe wake wote, haruhusu vita kupiganwa kwenye ardhi yake.
Russia yuko vitani na Ukraine kwa sasa, itakuwa ni ujuha kuchagua vita na wagner badala ya suluhu ya amani.
Nguzo muhimu ya jeshi ni Military Inteligency unit. Hii brain of jeshi. Muscles bila brain ni ng'ombe. Kazi ya leo Urusi, naona ni ufanisi wa MI ya Urusi.