Ushahidi wa Nyaraka na vielelezo kuhusu UZanzibar wa Rais Samia huu hapa

Halafu mbona mnangaika na huyo bibi kizee aliepata uraisi Kwa mgongo wa magufuli
 
Wewe sio Mungu
 
Ni kweli Tanganyika imejificha pale TAMISEMI. Maana ukiangalia kwa makini TAMISEMI ndio Tanganyika yenyewe.

Bado tumebaki kwenye muundo uliochukuliwa sababu ya aina ya itikadi za ulimwengu wa wakati ule. Kwa sasa ni wazi haziwezi kukidhi mahitaji.

Mjadala ni mrefu sana.
 
Lakini Tukijitoka kwenye TAMISEM..
Twende kwenye Serikali ya Muungano..

Kwanini Waziri Mkuu Wa JMT hana Usemi Zanzibar ???
 
Gud mbona nape anasema Samia ni mngoni
Kama kweli Nape amesema kuwa Samia ni mngoni, walio karibu naye wamwahishe haraka Milembe hospital.

"Sisi kule Zanzibar hatuna makabila. Mtu akiniuliza wewe ni kabila gani, namwambia mimi ni Mzanzibari" - Rais Samia.
 
Akamatwe kuishi Bara bila kibali
 
Jibu hoja za Lisu acha kulialia.Huu Muungano unatakiwa upitiwe upya na upigiwe kura ya maoni kuuhalalisha.
Una mambo mengi ya hovyo
 
Kwa wananchi wa kawaida (wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara), tutumie muungano kama fursa badala changamoto. Fikra zielekezwe kwenye kupanuka kwa masoko, ushirika wa kibiashara na ubunifu, urafiki na hata mahusiano ya kijamii.
Migogoro na kero za kisiasa zitaondoka pole pole baada ya wananchi kuwa wamoja.
Pande zote ziangalie maboresho ya muungano kwa uelekeo chanya zaidi.
Hata hivyo, changamoto za wanasiasa ni kawaida na muhimu katika kuweka mambo sawa kwenye jamii au taifa lolote (hoja zijibiwe kwa hoja).
 
Hizi ni pumba, peleka wakale nguruwe. Jeshi la ulinzi liko wapi na Mkuu wa Majeshi ni nani?

Mwaka 1920 Wajerumani walikuwa hawatawali Tanganyika kwa kuwa walishindwa vita vya kwanza mwaka 1919 na Tanzania ikawa colony la League of Nations. Muingereza akawa anastasia kama trustee.

Acha kuandika pumba, kajipange upya
 
mimi naona hoja za Lissu ziko sawa na za Jussa mbona jussa anaeleweka huko zanzibar watanganyika sisi ndiyo tatizo kwenye muungano kwa ukinyonga wetu kuhusu nafasi ya Tanganyika kwenye muungano hata km ilikufa,Kuna watu wananifaika na koti hili
 
BAada ha Vita vya Kwanza vya Dunia 1918 Ujerumani aliachia Baadhi ya Makoloni na hapo ndiyo Muingereza alipoanza kutawala..

Muingereza ilibidi kubadilisha Jina kutoka Ujerumani ya Africa Mashariki (East African German) na kuwa Tanganyika na hiyo ilifanykka Kutoka mwaka 1918 mpaka 1920..

Kuhusu Majeshi..
Jeshi la Wananchi Lilianzishwa mwaka 1964 baada ya Tishio la Mapinduzi lilifanyka mwaka huo na Rais kuvunja Jeshi la Tanganyika Riffles ambao ndo walikuwa wanajeshi wa Nchi..

Japo.Zanzibar walikuwa nao wana majeshi yao na kumbuka kabla ya Kuungana na Tanganyika walikuwa na Kiti Umoja wa Mataifa (Usisahau Hilo)..

Hata Hivyo zanzibar Pia wana Majeshi yao ambayo sio mali ya Muungano kama KMKM, JKU, Etc..

Nafikiri Kama Una hoja Weka mezani tujadili..
Kejeli, matusi wala hasira hazitakusaidia kitu..

Mimi naongea Facts na Uhalisia uliopo
 
Zamani Walikuwa Na passport yao ila Sijui ilifikia wapi waliamua Kuifuta..
Mtanzania Bara ni nani?
Kwanini mnaweza kutamka Mzanzibari lakini manashindwa kutamka Mtanganyika..?

Vipi mtu anayeishi Ukerewe Yeye haishi Visiwani??
Vipi anayeishi Mafia sio Mtanzania Bara??

Ok hiyo Sio Mada yangu ila Kikubwa zamani alikuwa nayo passport ila baadaye ikapurushwa..
Na kuhusu Kupewa Kitambulisho cha Mkazi ni Mara nyingi lazma uwe mzawa wa Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya zanzibar...

 
Miaka 60 hamkufanya kitu ndio iwe wiki moja ?
 
Dah, mbona hili linafahamika muda mrefu; kwamba Tanzania tuna waTanzania raia wa Zanzibar, ambao uraia wao huo ni muhimu zaidi ya uTanzania wao?
U-Tanzania kwao, ni nafasi tu ya kujinufaisha wao wenyewe na waZanzibar wenzao.
Kwa hiyo hili lisitushangaze sana, labda kwa vile tui watu ni 'slow learners', sasa ndiyo Tundu Lissu kawastua akili zao na kuanza kulitambua hili.
Watu wana bendera yao, katiba yao, serikali yao, na wanajitambulisha wao ni waZanzibari; bado mtu utakuwaje na mashaka nao kuhusu uraia wao?

Wanaweka mbele uZanzibar wao, lakini inapokuja wakati wa maslahi yao kulindwa, hapo hawasiti hata mara moja kujitambulisha kama waTanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…