Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Kumbe alikulia kota!? Ndio maana anamdomo.....
 
Mpimeni tezi dume
 
Swali langu kubwa ni hili:
Who does what?
Ni nani anafanya kipi?
Katika mkoa wenye mji?
Kuna
RC
RAS
DED
MAYOR
Wakuu wa idara zote:
Afya, elimu, kilimo, mifugo, miundo mbinu, mazingira, maji, ustawi wajamii/wazee/watoto/jinsia nk
Then kuna wabunge, madiwani, wenyeviti wa kata na vijiji na
WEO na VEO

Mimi nadhani kazi kubwa ya mkuu wa mkoa ni kuhakikisha kuwa

1. Kuna mgawanyo wa
kazi unaoeleweka
2. Kila kiongozi ama mfanyakazi anajua kuna fedha na vitendea kazi gani
3. Kila moja anajua majukumu yake
4. Kila moja amewezeshwa kutekeleza majukumu yake
5. Kuna ufuatiliaji na usaidizi wa karibu kutoka watu wanaoleweka wenye kujua nidhamu ya kazi.
Matamko mengine yaliyofanywa hayana maana kama wafanyakazi na viongozi hawajawezeshwa.

Kufunga maduka mpaka saa nne wakati watu wamelala na jiji ni chafu
bado haina maana.
Weka sheria na adhabu ya malipo mazingira ya mahali yakikutwa pachafu kama wanavyofanya Moshi.
Kwanini tunashindwa kujifunza kwa wenzetu?
Shimo linakaa barabarani na kuleta ajali kwa zaidi ya mwaka moja lakini hakuna kati ya viongozi wote hao anajua kuwa ni jukumu lake.
Ama barabara haina alama
Ama pomba la maji limepasuka
Ama kifusi cha vumbi kimekaa barabarani kwa mwezi mzima bila kutandazwa
Ama vumbi imetumika badala ya maram katika matengenezo ya barabara fulani
Ama kuna gereji kila mahali badala ya sehemumaalumu na ndiyo maana kuna magonjwa mengi ya kansa nchini
Ama barabara hii ama daraja hili ni mbovu inahitaji matengenezo.
Ama ufuko wabahari ni mchafu ila hatujui anayehusika
Au kuna ngombe na mbuzi wanachafua mazingira mitaani lakini hakuna mwenye usemi
Barabara nyingi Dar hazina majina na vitongoji na vijiji vingi Dar havina majina lakini hatujui anayehusika!

Ebu tuache kusifia kwanza
Haya mambo ya msingi yafanyike kabla ya makubwa yasiyowezekana!
RC siyo Mungu lakini ashirikishe viongozi wake ili kilamoja afanye wajibu wake, apate sifa zake
Badala ya RC kusema morning mpaka evening kuwa huu ni mkoa wangu! Mkoa wangu!
Tunachotaka ni mambo muhimu yakae sawa!
Amen!
 
Punga at work
 
Taratibu mkuu... Nissan nyeupe zimetapakaa popote zinakufikia lol
 
 
Nikiwa kama mkaazi wa jiji la dsm naomba wakaazi wenzangu wa jijini na wengine kutoka mingine tujadili je ktk matamko yote ya Makonda ni mangapi yamefanikiwa kwa100%?
 
Nikiwa kama mkaazi wa jiji la dsm naomba wakaazi wenzangu wa jijini na wengine kutoka mingine tujadili je ktk matamko yote ya Makonda ni mangapi yamefanikiwa kwa100%?

Kuvuka dhoruba kali aliyoipata mwaka 2017. Sasa imekuwa historia tu. Maisha yanasonga kama kawa, kama dawa za Bi. Havijawa.
 
Mateja kupungua mitaa ya ufipa waliokuwa wamejaa kuzunguka makao makuu ya chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…