Ushauri: Nimepewa RB kwa kosa la kufanya fujo kanisani

Weee! Huyo na mke. Yaani nipangiwe masharti Kwa mke wangu ninapo muhitaji.
 
Kwenye ulokole Kuna makanisa genuine kabisa ambayo hayana vitu vya kijinga jinga na ratiba zinaisha mapema,watu wanapata muda wa kuhudumia familia zao ukiona kanisa Lina Imani mara chumvi,mafuta,udongo,na mavitu hayaeleweki jua hao ni wahuni kama wahuni wengine
 
Makanisa mengi ya kilokole yanavunja sana ndoa za watu. Mimi mke wangu alikuwa anasali kwenye kanisa la kilokole kabla ya kumuoa. Sasa wakati nachumbia mchungaji akaja juu kwamba Binti hawezi olewa na mkatoliki. Akafikia hatua ya kuzuia nisitoe mahali. Basi nikasema niachane nae nitafute mwingine.

Baba mkwe alivosikia tu, alimpiga stop mchungaji asiingilie familia yake.

Nilipo muoa tu nikampiga marufuku kwenda kusali kwenye kanisa nililomkuta akisali. Nikamwambia sasa utasali ninakoenda Mimi, mpaka sasa niponae Roman Catholic.

NB: MPE MSIMAMO WAKO MKEO, MZUIE HAKUNA KWENDA KUSALI HUKO KWENYE HILO KANISA. AENDE KUSALI UNAKO SALI WEWE. MSIMAMO NI MUHIMU SANA.
 
Imani ziko tofauti mfano Kwa katoliki Ibada Huwa haizidi hata dakika 45 maximum saa moja mengine ibada masaa mawili ,mengine mfano kanisa la sabato siku nzima Huwa kanisani sababu huamini hiyo siku ni ya Mungu hivyo siku nzima lazima watumie kanisani kumaliza ibada mapema au la hutegemea Imani na Imani wengine hubaki kanisani siku nzima wengine Huwahi mapema ibada iishe haraka wakakumbatiane na wake au waume zao nadhani kuwahi au kuchelewa kumaliza ibada sio kigezo sana Cha kusema kanisa Fulani ni genuine or not Kwa muda wanatumia kwenye ibada ni hoja dhaifu sana hii umetoa
 
Watu wenye makanisa vya hivyo wanaviendesha Kwa nguvu za giza na Huwa wanachakata wake za watu sana ,Kuna mmja yupo huko dar ni mwathirika tayari niliwahi kuabudu kwake na kutumika kama mtumishi ,baadaye nikagundua uozo wake mwingi nikatoka kwenda tag,hivi Sasa hataki hata kunisalimia,na sikugombana naye,mimi niliamua kujiondokea tuu ila asilimia kubwa ya wanawake wa kanisani kwake na mabinti aliwapitia.Huyo bwana ukikaa naye hata kama hakufahamu atakuambia Siri zako zote za ndani,hii kitu inamfanya aaminike na mabinti sana.sasa hivi anakanisa kubwa linaweza kuwa na hata zaidi ya watu mia mbili.
 
Child neglect is a form of child abuse, peleka kesi dawati la jinsia na ustawi wa jamii muunganishe na huyo mchungaji pale polisi...s.h.e.n.z zake
 
Kanisa genuine ni lazima lijali Hali za washirika wake,maandiko yanasema yule asiyejali wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko asiyeamini`kama mchungaji Hana matumizi mazuri ya muda ni tatizo,Kwa kuwa kwenye ibada Kuna watoto na mchana watakuwa wale chakula Cha kawaida,huwezi kuwashindisha watu Kutwa nzima na njaa Kwa kigezo Cha ibada,mtu mwingine ana hiyo jumapili peke yake Kwa ajili ya mapumziko,kuona familia na watoto,kufua kufanya usafi n.k
 
πŸ™†πŸ™†πŸ™†πŸ™† Yaani hayo yanafanyikia nchi gani huko uliko mkuu?
 
Mimi ningechoma kanisa kabisa wanangu hawawezi kushinda njaa kwa sababu wapumbavu wachache.
 
Ref Flora and Emmanuel Mbasha.
Km beck 3 amemfundisha good care ampandishe shemeji yetu cheo na hii itamfanya awe na muda mwingi wa kwenda madhaba -huni.
 
Duuu! Inasikitisha Sana.

Kuna familia Moja jamaa aliweka fedha ndani Kwaajili ya kuendeleza Ujenzi wa nyumba Yao ili wahamie. Sasa siku imefika jamaa anamwambia mkewe leta Ile hela kazi ikaanze. Mwanamke akajibu nimetoa sadaka kanisani hivyo nilimpa mchungaji ili tupate baraka zaidi.

Jamaa alimshika mkewe akampa makofi kadhaa na kumwambia tuongozane kanisani Kwa huyo mchungaji. Alipofika jamaa alitoa panga na kumwambia mchungaji leta pesa aliyokupa huyu mke wangu. Mchungaji akajalibu kujitetea weee! Jamaa akamwambia nakufyeka, mchungaji akatoa pesa fasta.

Jamaa akamwambia mkewe marufuku kwenda kusali huko ila mwanamke akang'ang'ana na kumwambia mumewe eti ooo! nimeitwa na bwana kumtumikia hivyo bola tuachane. Mpaka sasa mwanamke aliachana na mumewe Kwa sababu alishindwa kutii maelekezo ya mumewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…