jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,530
- 9,550
Usidanganye watu bro kuwa hizo kazi kama zina laama bali shauri vijana wafanye hzo kazi in proffesional way mimi ni graduate toka 2012.1. Kuokota chupa za plastic za kupima kwa kilo.
Hii kazi inauhusiano wa moja kwa moja na ukichaa.
Katika tafiti yangu ndogo nimegundua wanaojihusisha na hii kazi lazima akili ziruke kidogo.
Kuna mmoja hapo External alikuwa mzima kabisa hadi alipoanza kuzunguka na mfuko huko barabarani kutafuta chupa/makopo ya maji/soda n.k! Mwingine ni wa Maramba mawili, hawakuchukua muda sana akili kuvuruga.
Jihadhari na hii kazi, hata maisha yawe magumu kiasi gani...
2. Bodaboda (esp. Graduates) Hapa nawazungumzia vijana walioenda shule kidogo, at least una shahada. Jiepushe sana na Bodaboda!! zinaharibu sana akili.
Vijana wengi waliohitimu vyuo vikuu na kujiingiza kwenye boda, kuchomoka huwa ni shughuli sana, japo wapo wachache sana wanaojitahidi.
3. Udalali; (hii kwa graduates pia)
Wapo vijana wengi wa sasa hasa kwa Dar wakimaliza vyuo wanaaanza kazi ya udalali wa nyumba na viwanja.
Kigamboni huko wamejazana sana, wengi wao ni walevi tu hakuna cha maana wanachoweza kufanya zaidi yakupata pesa na kuishia kwenye ulevi.
Hii kazi Usifanye. Haina matunda yoyote kwenye future yako.
4. Usidange; (hasa mabinti) umemaliza chuo huna ishu ya maana mjini rudi kwenu kakae na wazazi wako huku ukiendelea kutafuta cha kufanya.
Nawasilisha.
Na kazi yangu ilianzia kwenye bolt nkahamia udalali mpaka leo napozungumza na wewe nina kampuni na nimesajiliwa kama dalali na kila siku navusha gari toka nje na kila siku nauza gari za watu.
Na kupitia kazi hyo naweza kuthubutu kusema kuwa kuna wafanya kazi weng sana wa non and government nmewapita mbali.