uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 17,060
- 32,400
Ukiingia kwenye huu mfumo wa Tausi kupitia tausi.tamisemi.go.tz una vitu vingi sana ndani japo vingine naona havifanyi kazi.
View attachment 2888384
Nimefurahishwa sana na uuzaji wa viwanja ambapo unanunua kiwanja unakiona kwenye ramani kama ilivyo google map, tofauti na ile ya kwenye karatasi. Wengi tuna viwanja ila hata location hatujui mpaka twende physically.
View attachment 2888388
Hii inampa uhuru mtu kununua kiwanja popote nchini bila kufika ili mradi anakiona.
Tatizo naloliona hapa ni moja tu, Wilaya nyingi zimepima viwanja ila havipo humu.
Nini unatakiwa kufanya
-> Jisajili kwa kutumia NIDA na TIN yako
-> Nenda land sale module
utaona viwanja vyote vinavyouzwa na Halmshauri nchi nzima
-> Chagua Halmashauri unayotaka kununua kiwanja
-> Chagua kiwanja kutoka kwenye ramani
-> Lipia kupitia control number ya ada ya maombi utakayopewa
-> ukimaliza kulipia utapata control number nyingine ya ada ya kiwanja, ukishalipia kiwanja ni chako!
Unaendelea na hatua za kupata hati.
View attachment 2888389
"Hii inampa uhuru mtu kununua kiwanja popote nchini bila kufika ili mradi anakiona"
Tanzania? Kununua kiwanja bila kufika? He he he! We unaishi Tanzana? Haujui migogoro ya ardhi yote chanzo sio mifumo, ni watumishi wa wizara ya ardhi?