Uuzwaji wa viwanja vya serikali mtandaoni ni hatua kubwa sana

Uuzwaji wa viwanja vya serikali mtandaoni ni hatua kubwa sana

Ukiingia kwenye huu mfumo wa Tausi kupitia tausi.tamisemi.go.tz una vitu vingi sana ndani japo vingine naona havifanyi kazi.
View attachment 2888384

Nimefurahishwa sana na uuzaji wa viwanja ambapo unanunua kiwanja unakiona kwenye ramani kama ilivyo google map, tofauti na ile ya kwenye karatasi. Wengi tuna viwanja ila hata location hatujui mpaka twende physically.

View attachment 2888388

Hii inampa uhuru mtu kununua kiwanja popote nchini bila kufika ili mradi anakiona.
Tatizo naloliona hapa ni moja tu, Wilaya nyingi zimepima viwanja ila havipo humu.

Nini unatakiwa kufanya
-> Jisajili kwa kutumia NIDA na TIN yako
-> Nenda land sale module
utaona viwanja vyote vinavyouzwa na Halmshauri nchi nzima
-> Chagua Halmashauri unayotaka kununua kiwanja
-> Chagua kiwanja kutoka kwenye ramani
-> Lipia kupitia control number ya ada ya maombi utakayopewa
-> ukimaliza kulipia utapata control number nyingine ya ada ya kiwanja, ukishalipia kiwanja ni chako!

Unaendelea na hatua za kupata hati.
View attachment 2888389


"Hii inampa uhuru mtu kununua kiwanja popote nchini bila kufika ili mradi anakiona"

Tanzania? Kununua kiwanja bila kufika? He he he! We unaishi Tanzana? Haujui migogoro ya ardhi yote chanzo sio mifumo, ni watumishi wa wizara ya ardhi?
 
"Hii inampa uhuru mtu kununua kiwanja popote nchini bila kufika ili mradi anakiona"

Tanzania? Kununua kiwanja bila kufika? He he he! We unaishi Tanzana? Haujui migogoro ya ardhi yote chanzo sio mifumo, ni watumishi wa wizara ya ardhi?
Ngoja tujilipue
 
unataka taarifa ipi si uingie mtandaoni uwe unaviona viwanja vinavyouzwa shida nini? na ununue @ your own willingness au unataka mpaka upewe na bando?
Hutapata hata muda wa kuviona. Soma hoja yangu utanielewa ... Ndani ya robo saa miamba wanakuwa wamevi 'chukua' vyote. Lakini vilivyo maeneo ya kawaida au mbali na mji utaviona vingi tu
 
UPDATE
Nmemaliza kulipia kiwanja changu tatizo nililokutana nalo
1. Siwez view bill yangu ili nione gharama za hati
2. Nilitarajia kua baada ya kumaliza kulipa kiwanja ningepata control number mpya kwa ajili ya kulipa hati
3. Sina uwezo wa kuwasiliana na huduma kwa wateja wa tausi, au sina mawasiliano na watu wa kwimba halmashauri. Kwimba namba zao hazipatikani na tausi hakuna jinsi ya kuwapata
4. Tamisemi kwenye website wame weka namba za kuwa tafuta ila hazijalipiwa so hata nilipiga sina jinsi ya kuwapata.
any update?
 
Nimeupitia na kuna baadhi ya viwanja Nimeanza kulipia sema kuna mapungufu

1. Kuna mda mfumo unakua haupatikani

2. Kuna mda unaingia unakua wilaya ime ongezeka ukija baadae hutaiona tena. Mfano Bagamoyo, bahi, iringa hizi inakuja na kupoteza naanza kuhisi hua wanaziweka akiwa na wateja wao. Mfano bahi na iringa viwanja ilikua bei ya mserereko

3. Kwenye kiwanja ukianza kulipia kulikua na gharama za kuandaa hati, nmechukua mm viwanja viwili ila ss kuna kitu inaitwa Premium kimeongezwa na mwanzo hakikuepo kabisa na ni hela ndefu

4. Ni hongera system ukilipa mda huo huo chat inasoma.

Kama kuna mwenye kuongeza karibu
Na mimi nimeona hizo gharama za hati, halaf ziko separate na gharama za kiwanja sasa sijui zenyewe nalipia kwa control number ile ile ya kulipia kiwanja. Mwenye uzoefu ashee tafadhali
 
Screenshot_2024-05-20-00-37-26-667_com.android.chrome.jpg
 
Na mimi nimeona hizo gharama za hati, halaf ziko separate na gharama za kiwanja sasa sijui zenyewe nalipia kwa control number ile ile ya kulipia kiwanja. Mwenye uzoefu ashee tafadhali
usilipie gharama za hati kwa ile control number, nenda halmashauri ukishalipia watakupa form ujaze ndo ufuatilie hati ofisi za ardhi
 
Back
Top Bottom