Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Walikua wanatamani sana kumkamata na kuzuia huo msafara wa leo, ila walihofia dunia nzima inalitazama hili swala la Lissu kurudi nchini pia wananchi wangechukua sheria mkononi (Wangefanya vurugu kuvunja magari, maduka, wangevunja airport, wangechoma matairi na fujo nyingine).

Tusijidanganye eti polisi wetu wamejifunza kuwa na busara au hekima, hilo halipo, mazingira tu ya leo yamewabana polisi.
Kwa iyo unataka kusema hakuna mtz aliewaambia wasizingue, bali ni ivyo vitisho vya mabwana zenu wa kizungu
 
1 JPM

2 LISU


3.MEMBE
Tusitegemee mchuano mkali kabisa kati ya jpm na mgombea mwingine yoyote kutoka vyama vya upinzani kwakuwa tayari sehemu kubwa ya utekelezaji wailani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi umetendeka, kadhalika na yale yaliomo katika ilani ya vyama vingine.
wanao Dhani lisu ataleta ushindani wanaudhaifu katika kumtazama lisu as presidential candidate, kwa sababu hoja nyingi za bwana lisu si zakuinua uchumi bali zakunusuru wapinzani na kiu ya raia si hiyo.

Kila la kheri Tanzania kila la kheri Mtanzania mlinda Amani
Itoshe kusema kua MATAGA ni kikwazo mojawapo cha maendeleo nchini. over!
 
Halima Mdee amefanya vyema leo kulipongeza jeshi la polisi, si vibaya chama kikatoa shukran rasmi kwa jeshi la polisi, hata kama ni kwa kinafiki. Pia nashauri sana Tundu Lisu ashauriwe kutokwenda kesho msibani. Kwangu bado Lisu ana hasira na lile shambulio, kwa vyovyote atataka kuionyesha serikali na hasa rais Magufuli kuwa amepona. Na mashabiki wake wanaweza kuonyesha furaha iliyopitiliza ambayo itaipa serekali sababu kuchukua maamuzi hasi dhidi ya cdm.

Kwakuwa wamemstahi leo, ni vyema angeachana na huo msiba, kuna nafasi kubwa ya kushindana na ccm. Na kama itawezekana kuanzia sasa Lisu pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano hii rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anapambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi lake binafsi. Ni juu yetu wapinzani kutumia kukubalika kwa Lisu kwa njia chanya kuliko kuvutana
Mkuu kwa mara ya kwanza Leo umeshauri vizuri!!
 
Leo Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe wameonesha usaliti kwa mara nyingine. Awali walijiweka kama wanajali wananchi ila leo wamekuwa tayari kuangamiza watanzania kisa Lissu.

Walijivika joho la WHO huku wakihubiri Sera za kubaki ndani maarufu kama Karantini kumbe ni unafiki mkubwa.
Tuwapime, tuwashangae, tuwakatae.
 
Binafsi sikuwa na matarajio ya kwenda uwanja wa taifa kwenye sherehe za kumuaga mpendwa wetu mkapa.

Na hii sio kwamba sikuona uthamani wake kama Rais mstaafu La hasha, Mkapa kafanya mengi mazuri na namuombea anakoenda Alazwe mahala pema.

Lakini kwa Lissu Kama atakuwa na Ratiba ya kwenda na Mimi lazima niwepo na hapa tayari Niko kwenye basi natoka mkoani nakuja Dar.

Mwaka 2015 nilimpa kura yangu namba one anayeongoza Sasa, mwaka huu sikutegemea kupiga kura lakini Kama Lissu akigombea nitasafiri kwenda nilikojiandikishia nikapige kura.

Naombeni kujua ratiba ya Lissu kesho kama atakuwepo kwenye uwanja wa Mkapa
Karibu Mjini Dar tutaambatana na kiobgozi wetu mpenda amani na haki. Unajisikia Ufahari ulioje kwenda msibani na Lissu??
Kesho msibani kutafurika.
 
Leo Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe wameonesha usaliti kwa mara nyingine. Awali walijiweka kama wanajali wananchi ila leo wamekuwa tayari kuangamiza watanzania kisa Lissu.

Walijivika joho la WHO huku wakihubiri Sera za kubaki ndani maarufu kama Karantini kumbe ni unafiki mkubwa.
Tuwapime, tuwashangae, tuwakatae.

Covid-19 karudi Wuhan, China.
 
Lisu ajihadhari sana na Mbowe, Lema, Halima Mdee na Ester Bulaya, hawa ndio walimpigia kura ya HAPANA hafai kuwa mgombea urais, wanamtaka Nyalandu, ujio wake umewakasirisha wanaweza kumdhuru, asipokee maji ya kunywa, chakula wala kushikana nao mikono.
Unafikiri cdm Ni Kama hilo lichama chakavu??
 
Back
Top Bottom