Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Halima amefanya vyema, si vibaya chama kikatoa shukran rasmi kwa jeshi la polisi, hata kama ni kwa kinafiki. Pia nashauri sana Tundu Lisu ashauriwe kutokwenda kesho msibani. Kwangu bado Lisu ana hasira na lile shambulio, kwa vyovyote atataka kuionyesha serikali na hasa rais Magufuli kuwa amepona. Na mashabiki wake wanaweza kuonyesha furaha iliyopitiliza ambayo itaipa serekali kuchukua maamuzi hasi.

Kwakuwa wamemstahi leo, ni vyema angeachana na huo msiba, kuna nafasi kubwa ya kushindana na ccm. Na kama itawezekana kuanzia sasa Lisu pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano huu rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi binafsi.
Jamani yule bwana mnasema amepona mbona anatembea kama kaa au kiuno wamekipunguza huko ubelgiji?
 
Asanteni sana @tanpol !!! Tunawapenda SANA!! SISI ni watu wema!!! Tanzania ni YETU SOTE. Tusiruhusu maslahi ya WATU wachache watuvurugie UPENDO wa ASILI wa TAIFA LETU-Halima Mdee
Watasifiwa na hatutoacha kuwasifia watekelezapo wajibu wao kiweledi... wakichemka tutasema maana Tanzania ni yetu sote na urithi wa vizazi vijavyo.
Kuna wimbo huimbwa "...raia kama raia... nitarudi..." ni ndugu zetu twaishi nao kwa wema...
LAZIMA TUAMINIANE
 
Halima amefanya vyema, si vibaya chama kikatoa shukran rasmi kwa jeshi la polisi, hata kama ni kwa kinafiki. Pia nashauri sana Tundu Lisu ashauriwe kutokwenda kesho msibani. Kwangu bado Lisu ana hasira na lile shambulio, kwa vyovyote atataka kuionyesha serikali na hasa rais Magufuli kuwa amepona. Na mashabiki wake wanaweza kuonyesha furaha iliyopitiliza ambayo itaipa serekali kuchukua maamuzi hasi.

Kwakuwa wamemstahi leo, ni vyema angeachana na huo msiba, kuna nafasi kubwa ya kushindana na ccm. Na kama itawezekana kuanzia sasa Lisu pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano huu rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi binafsi.

Unamshauri TL ambane na CCM kwa sera? Mbona hujaishauri CCM ifanye hivyo hivyo badala ya kupambana na Lissu na upinzani kwa risasi na mauaji?
 
Inakuuma sana kwa ile nyomi/poor on you mkuu
Leo Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe wameonesha usaliti kwa mara nyingine. Awali walijiweka kama wanajali wananchi ila leo wamekuwa tayari kuangamiza watanzania kisa Lissu.

Walijivika joho la WHO huku wakihubiri Sera za kubaki ndani maarufu kama Karantini kumbe ni unafiki mkubwa.
Tuwapime, tuwashangae, tuwakatae.
 
Mh tundu lisu dunia imeona ulichofanyiwa na ujio wako umewatia aibu watesi wako.

Mapokezi yako yawape heshima waliokuja kukulaki. Ili waiandike historia Yao ya mapenzi na amani kupitia wewe.

Tal the great

Hivi wewe unayetoa huu ushauri kwa TL ulishawahi hata kujeruhiwa kwa kisu na vibaka ukatoroka? Unaelewa nini kuhusu risasi kupita mwilini? Unajua nini kuhusu kuwa katika coma kwa masaa 6?

Kama hujui jibu la moja wapo ya maswali hayo basi funga kopo lako kalale. Ushauri huo kawape CCM waliotumwa na shetani kuondoa uhai wa Mtanzania mwenzao bila chembe ya huruma.
 
Hongera sana jeshi la polisi,ila walichofanya leo ni kuhakikisha Lisu hapati kuvuma kimataifa kama ambavyo polisi wangemkamata siku ya leo,ushauri tena,wamuache bila kumgusa ili wasimuweke katika ramani ya vyombo vya habari,zaidi atabaki youtube na twitter ila wakimgusa,dunia nzima itamtangaza na hapo tutaongea mengine.
An alternative apology. Hakuna kitu kama hicho. Ujasiri wa Lissu hata wao wameshikwa na butwaa
 
Back
Top Bottom