Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye uprofesa wa mambo ya kale kaandaeitini ketu umo. Kwenye wosia wa falsafa za kihenga kuhusu maisha pia umo. Yaani ni fulu pakeji [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Halafu kizazi hiki kinachoishia aisee ni kiboko. Yupo mtoto wa braza. Ni hawa kizazi kipya. Fulu mlegezo na swaga za akina Fifite Senti. Kabahatika tumemsomesha somesha akasoma soma. Fulu kujitapa yaani. Kaja home kumuona bibi yake (alikuwa anakaa Arusha kwa babake). Sijui alipata wapi ujasiri lakini siku moja ya mnada akatafuta wafanya biashara wa ng'ombe akawaambia ana ng'ombe anauza. Wakakubaliana bei. Huyoo akajitolea kwenda kuchunga siku hiyo ng'ombe wa mama niliomnunulia mimi mwenyewe. Huko akauza ling'ombe lile dume kubwa zee la familia (liyagamba) na jike mmoja aliyekuwa ananyonyesha.

To cut the long story short mpaka mama anakata roho anawaambia watu aliokuwa anaagana nao kuwa "Mwambieni Mabula awarudishe wale ng'ombe nilionunuliwa na mwanangu". Alikuja kwenye msiba wazee wakamkataza kulia wala kulisogelea kaburi na wazee wa ukoo walikuwa wamepanga kumtandika ila akaushtukia mchezo akaondoka. Baadaye mimi nilimtafuta na kujaribu kuongea naye. Nilimuuliza kama alikuwa anajua shida aliyokuwa ameachiwa na bibi yake. Ndipo sasa akafurumka kulia fulu kuomba msamaha. Nikamshauri aende kwa wazee akaongee nao. Wazee wakasema hawawezi kumsaidia kwa sababu aliyemkosea hayupo. Imagine mama kafariki Desemba mwaka jana lakini hata mwaka haujaisha dogo yaani hayuko sawa kabisa kisaikolojia. Kasoma na alikuwa ameanza kazi nzuri (uhasibu) lakini kafukuzwa. Sasa fulu kucheka peke yake na kujiongelesha
"bibi nisamehe, nisamehe bibi". Wazee wa ukoo wamemshauri anunue mbuzi akachinje juu ya kaburi na atafute fedha aende akawape masikini. Ameshafanya yote lakini hali inazidi kuwa tete.

Nimeamini lawama zipo na zingine hazikawii aisee. Wazazi - wawakilishi wa Mungu hapa duniani [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Duh! Akishaondoka aliyemtamkia maneno yale ni ngumu sana kuwa sawa, ile ni roho inamsumbua.. Mama alifariki akiwa na manung'uniko juu yake.
Anaweza kuishia kuwa kichaa..( Mungu amuepushe)...
 
*USHAMBA WA MSUKUMA UKO WAPI..?*

_Ninavyomfahamu_

1. Hapendi makuu,ukimchokoza anasema *KAYA YA NG'WOBA NAYO KAYA* ili siku ipite salama.

2. Hapendi kesi,ukimdhurumu anasema *MAGUZU MASESE* ili asipoteze muda kufuatilia mambo ya kesi, badala yake afanye
kazi.

3. Hapendi kuumiza moyo kwa hasara iliyotokea, akipata hasara anajipa moyo kwa kusema *JATULWA MBITI JIDATANG'ANHAGA* ili aepuke matatizo ya madonda ya tumbo, moyo presha n.k.

4. Hapendi kujikweza, ukimsimanga ugenini anasema *NG'OMBE NG'ENI IKAPAMAGWA NA DIDA* huo ndo ustaarabu.

5. Ni mvumilivu hata kwenye suala la utafutaji, akianza na mtaji mdogo hujipa moyo kwa kusema *BUSHI BO MBULI BUKAKWILILAGA MU BUTUNGO* wengine husema haba na haba hujaza kibaba.

6.Hatoi siri ovyo ovyo, ukimdadisi anakwambia *KAMANWA MAMBI KALI MU NG'HOMA* ili kuepusha uchonganishi.

7. Kipindi cha njaa huwafariji wana familia kwa kuwaambia *SHILIWA SHIDOHE BALI BAKWILE* ili kuwaondoa hofu akijua baada ya dhiki kuna faraja.

8. Hana roho mbaya, penye watu wengi na nafasi ndogo husema *BITOGILWE BATISHITAGA* ili kujenga upendo na kutobaguana.

9. Hana hasira za kukurupuka, ukimchukiza anasema *AKULIPA WELELO* huku akitafakari cha kufanya.

10. Anajua mambo yote hapa duniani ni ubatili na yote yatapita, akikabiliwa na jambo gumu asiloliweza anasema *NDUHU TAABU*

[emoji654]️[emoji654]️[emoji654]️[emoji654]️Mtafute shoga yako akutafsrie. Ukielewa hutatutania tena. Shwaiiiiiiiiiiiiiniiiiii [emoji16][emoji16][emoji16]. Leo hata lishikamoo lako silitaki [emoji36][emoji36][emoji36][emoji36]
 
Aisee,,, story inasikitisha sana jamaa kawa chizi hv hv masikini,, na tusipokuwa makini vijana wengi wa kizazi hk tutataabika sana,,, wazazi wetu tunawachukulia poa sana wakati sivyo tunavyotakiwa,,
Tufanye yote ila sio kuwakosea wazee wetu jamani!!!

Hata vitabu vitakatifu vimetoa maono hayo!!
 
Tatizo vijana wa sasa hivi mnajidai watoto wa kidijitali, msipokuwa makini mtapambana na hali zenu,, usione mtu anapata baraka ya maisha, siku zote ni mtu wa kuinuliwa tu...Mkilowea mijini huko mnalowea kweli, (kama wazazi wapo vijijini) si wa salamu wala chochote kitu kwa wazazi wenu + bibi + babu (kama wapo hai).. Halafu siku mkipata matatizo mnakuwa mzigo kwa wazazi wenu..
 
Ugumu upo kwenye kauli hii ....
"Mwambieni Mabula awarudishe wale ng'ombe nilio nunuliwa na mwanangu"

Si ajabu hao ng'ombe walisha chinjwa, na bibi yake huko aliko (Rip) anaumia zaidi kupotezewa zawadi aliyo pewa na mwanawe.
Kupona kwake ni hao ng'ombe warudi (katika mila tunaamini misyuka kuwa inasikia na inajibu) kama hawakuchinjwa na matambiko yafanyike.
Lasivyo laana ya tamaa imemuangukia. Mama(Rip) asilaumiwe kwa hilo, muache huyo bwana mdogo aendelee kukata viuno mtaani na visuruali vyake.
Shwaiiniii zake....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…