Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alan Shearer & Roy KeaneMastaa hawa wawili walikuwa ngumi mkononi. Kila walipokutana basi ilikuwa balaa kubwa ndani ya uwanja. Mambo yalianzia mwaka 2001, wakati Keane alipomkosa kwa konde kali straika Shearer. Baada ya hapo, yaliibuka majibizano makubwa kwenye korida za kuingilia vyumbani. Shearer alikwenda kulipa kisasi ndani ya uwanja kwa kupiga kiwiko katika mechi iliyopigwa uwanjani Old Trafford. Wawili hao walikuwa kawatazamani usoni hadi walipostaafu soka.
 
Ian Wright & Peter SchmeichelIlianza kwa madai kwamba Wright amefanyiwa vitendo vya kibaguzi na kipa Schmeichel. Jambo hilo likazua chuki na bifu kubwa baina ya wachezaji hao na kila walipokutana kwenye mechi basi ilikuwa vita kubwa. Schmeichel alisafishwa hakutenda kitendo chochote cha kibaguzi, lakini hilo halikumaliza bifu la wawili hao wakati Arsenal ilipomenyana na Man United. Kuna mechi moja iliyofanyika Highbury, Wright alimchezea rafu mbaya Schmeichel kwa kumrukia miguu miwili. Kwa sasa wapo vizuri.
 
494346a0-e863-43fc-8cfd-1809e6854819.jpg
 
John Terry & Wayne BridgeBifu nyingine za wachezaji zimekuwa zikizaliwa ndani ya uwanja tu, lakini hii ya John Terry na Wayne Bridge imetokea nje ya uwanja. Kabla ya hapo, wawili hao walikuwa marafiki wakubwa, lakini mambo yaliharibika baada ya Terry kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mchumba wa Bridge, mrembo Vanessa Perroncel. Jambo hilo lilianzisha bifu kubwa baina ya wachezaji hao wawili ambao wote walikuwa wakiichezea timu ya taifa ya England. Terry alivuliwa unahodha wa England kisa bifu hilo.
 
Roy Keane & Patrick VieiraHili bifu lilikuwa utamu wenyewe wa mechi za Manchester United na Arsenal. Kila mechi hizo mbili zilipofanyika, basi walichokuwa wakikifikiria watu ni shughuli itakayoonyeshwa na manahodha wawili, Roy Keane na Patrick Vieira. Ilikuwa ubabe. Keane akimchezea rafu mchezaji yeyote ya Arsenal, Vieira alikuwa akilipa kwa mchezaji wa Man United. Kukunjana jezi ndani ya uwanja kilikuwa kitu cha kawaida kwa wachezaji hao kwenye mechi zao.
 
Diego Costa & YeyoteKuna kundi kubwa la wachezaji waliowahi kulumbana na straika Diego Costa. Ni wachezaji kibao wamelumbana na straika huyo, lakini bifu lake dhidi y beki wa zamani wa Liverpool, Martin Skrtel lilikuwa balaa zaidi. Wawili hao walipokutana, ilikuwa balaa. Ilikuwa vuta nikuvute, viwiko, kuvutana kukanyagana na vurugu za kila aina.Mashabiki walivutiwa na bifu lao kwa sababu liliwakutanisha mastaa wawili waliokuwa wakorofi na uhuni mwingi.
 
Back
Top Bottom