Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA waendelea, Kawe kumewaka moto leo

Kuvutia kivipi? Umesahau ya kuwa unaweza kumpeleka punda mtoni ila kamwe huwezi kumlazimisha kunywa maji? Mimi mwenyewe nipo Dodoma kupata burdani kutoka kwa wasanii 200 ila kura yangu ni kwa Lissu
 
Siihitaji campaigned, maana maamuzi nishafanya siku nyingi. Ni Yeye ndio naenda nae.
 
Nipo kwenye mkutano hapa na nimefika muda mrefu sana ili kusikikiza sera mbadala kutoka kwa viongozi wetu na mgombea wetu.

Kabla ya yote jana mgombea wetu alitueleza kuwa tutafanya maandamano ya amani kabla ya mkutano kuanza ila ukweli ni kuwa hatujafanya maandamano hadi sasa na tupo hapa hatujui kinachoendelea.

Watu tupo wachache kuliko jana mbagala, ila hii inaweza kuwa bahati mbaya kwa sababu nadhani wamechagua sehemu ambayo haikuwa sahihi.

Kawe ni sehemu ambayo imezungukwa na sehemu za ushuani ambao huwa hawapendi kabisa mikutano ya kisiasa. Ningekuwa mimi huu mkutano leo ungefanyika ubungo, magomeni au kimara lingetafutwa eneo zuri la wazi maeneo hayo kwa ajili ya mkutano.

Ila yote kwa yote kuna shida ndani ya chama.
 
Daaaah nashindwa kuelewa what next but unaeza kuta watu wameuchuna tu hawataki kujionyesha hadharan kuwa wao Ni wapimzan alafu kwenye sanduku la kura wakafanya maajabu tuwe wavumilivu October 28 sio mbali [emoji3577][emoji3577]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…