Vibonge tambueni kuna tofauti ya kula chakula kingi na kula kula ovyo

Kupungua inahitaji wito sana aise..ujitoe haswa
kwa sasa kiukweli nimeamua nimepunguza mno kula japo vishawishi vingi mno katika kipindi hiki nilikutana na offer moja ninayoipenda lunch wali samaki mkubwa na maharage na saladi nikasema pita kule.
siku nyingine nikakutana na ugali makange angalau hapa nikaagiza ndizi za kuchoma na mishkaki miwili
kiukweli naenda vizuri japo kuacha soda sio mchezo nimefanikiwa kwa sasa.
 
anza kupunguza chakula hasa jioni ikumbukwe kuwa njaa iko kichwani lakini tumbo ni stoo tu hivyo kula kidogo
Kabisa mkuu, nilijaribu kufata nikafanikiwa,ukiwa mnene njaa ikiuma unaeza hisi unakufa😁
 
Kabisa mkuu, nilijaribu kufata nikafanikiwa,ukiwa mnene njaa ikiuma unaeza hisi unakufa😁
maji ni ya msingi sana kipindi hiki na kuongeza movement tunahitaji kupungua ila huu ukali wenu wa maneno ni hatari.
siku moja nilikaa na watu walinishambulia kuhusu unene nikawajibu kwani nimewaambia kuwa nataka kupungua nilijitetea mpaka wakacheka lakni ndani kwangu nilijua hii leo nimepigwa.
 
🤣🤣🤣🤣! Mimi coke sijui kama nimelogezewa...dah...! Siwez acha kula nyama au samaki...kitu sili kbs ni pork
 
We ni ke
 
Kuna ulaji unaosababishwa na stress..... Huu upo sana especially kwa akina dada wanakuwa wanakula sana fast foods a.k.a Junkfoods matokeo yake wanakuwa na vitambi na matumbo kama mbuzi mwenye mimba au chura.
 
Kauli yako hii ya "njaa iko akilini tumboni ni store tu" nitaitumia sana kuwasaidia vibonge wanye bidii ya kupungua
 
Haaaa!

Yani kutwa nzima unakung'uta tu misosi😀😀😀 hapa lazima mtu ufumuke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…