Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Nadhani GSM kama wana akili waache kucheza michezo ya wanasiasa. Hakuna aliyejua Nape atakuja kuwa Waziri karibuni.

Makonda anaweza kuja kuwa Rais au Waziri na mwenye ma mlaka ndipo utakapoona GSM wanakimbia nchi.
Ni kwasababu tu nchi yetu ndio hii Tanzania, ukiwa rais/waziri uko juu ya sheria.
 
Na huyo GSM umesha jiiuliza kwa nini wampe Mkuu wa Mkoa wa DSM zawadi yenye thamani kubwa Kama hiyo!? What do they wanted in return kutoka kwa Mkuu,ambacho hawajakipata au hajakitimiza na wakaamuwa wamdai Mali yao waliompaa!?
Hofu ya madaraka makubwa ya kifalme yanayotiririka kutoka ofisi namba moja.
 
Nafuu tuwatetee hao unaowaona waarabu kuliko mtanzania mwenzetu aliyempiga Jaji Joseph Warioba, alimuua Ben Saanane na kumwagia risasi 16 Tundu Lissu

issue ni unafiki wa wao kujifanya ndugu zetu aka Watanzania wenzetu halafu gizani wanatumaliza na wakijinadi hapa sio kwao, wakati mwingine hata kunyanyapaa ndugu zetu kwa kuwatumikisha kama watumwa..

Sijatetea Wazungu, wao wanakuja kama wageni kabisa kuja kufanya biashara hivyo tunajua kabisa ni wavamizi na tukiwaruhusu ni ujinga wetu, sasa hawa wanafiki wanajifanya watanzania wenzetu hapa huku si kweli...

Sina nia mbaya wala ubaguzi, ila nimekiexperience hiki kitu nina uzoefu nao...ndio maana ni kosa kubwa kuruhusu hawa watu washike uchumi, wakiushika lazima wawaslave..
 
Kwa sababu yeye ni kapuku mbangaizaji mnyonge
 
Kuna mbunge aliwahi kulalamika juu ya utajiri wake wa haraka mwanzoni kabisa mwa ukuu wake wa mkoa sikumbuki alikuwa nani, leo ndiyo naelewa kumbe alishuhudia mambo mengi
 
Hii imesababisha malori mengi ya Tz yasajiliwe Zambia, udikteta umefukuza wawekezaji wengi sana awamu iliyopita
 
Mataga pori sio rahisi waruhusiwe kushika tena usukani na watoto wa mjini, wamejifunza.
 
Kufanya biashara kwa utulivu katika mazingira kama haya ni vigumu sana.
Tunahitaji sana Katiba Mpya.
 
Pia kuna kitu kinaitwa "weaponization of law", hii hufanyika hata kwa watu wasio na kitu cha kuficha.
Ukiona hivyo Basi walikuwa na vitu vya ovyo nyuma yao au walikuwa wanafanya ya ovyo. Huwezi kukubali kirahisi kufanya jambo kama Unajua huna cha kuficha.
 
Kwenye hili suala la Makonda kwa kweli kabisa serikali haifanyi sawa. Kila siku serikali inahubiri watu wasijichukulie sheria mkononi na watii sheria bila shuruti. Lakini ninapokuja suala la Makonda inapata kigugumizi kwa mtu ambaye hata wito wa mahakamani anagomea yeye ni nani katika nchi hii. Na inaleta picha gani kwa watanzania milioni 60 wa nchi hii. Watu wanamlaumu hapa GSM lakini inawezekana walishatoa taarifa lakini zikakaliwa nao wao wanamuona mporaji yupo anatamba na hachukuliwi hatua sasa kwanini wasifanye hayo wanayofanya hata kama sio sahihi? Mtu ana tuhuma lukuki halafu eti anaachwa mtaani mpaka ajitokeze mtu binafsi Kubenea amshtaki wakati vyombo husika vinavyoendeshwa kwa kodi na tozo zetu vipo. Tena mtu huyo aliyejitolea anapata vikwazo kibao vya kumfisha Makonda kwa Pilato.

Je vyombo vya dola havioni kuwa vinachangia katika suala hili la Makonda? Na kama GSM kaanza kudai mwenyewe je ni wa ngapi wapo njiani kwenda kuchukua mali zao kwa Makonda? Na ni wangapi watadai kistaarabu? Mtu akifanya makosa makubwa mara nyingi Polisi au Mahakama huwa zinamuweka sehemu salama lupango ili wenye hasira kali wasimdhuru, je vipi kwa Makonda kwa nini asiwekwe sehemu salama ambapo ni lupango ili wenye hasira kali wasije kumdhuru?

Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama kikubwa cha upinzani hapa chini alituhumiwa tu ugaidi wa kumbumba akafikishwa mahakamani na akakaa ndani mpaka alipofutiwa mashtaka. Marehemu Ditopile alikuwa "best man " wa raia namba moja wa nchi wakati huo alituhumiwa kuua dereva dala dala alifikishwa mahakamani na akakaa ndani ili watu wenye hasira kali wasije kumdhuru ingawa baadaye alipata dhamana. Na mifano ipo mingi kama ya wa kina Mramba, Yona , Kiula, Sabaya, n.k. Sasa kwa Makonda basi tuelezwe ni kitu gani hasa "special" alicho nacho ambacho kinazuia asifikishwe mahakamani kujibu tuhuma. Na kama ni msafi mahakama si itamsafisha na kumuachia huru aendelee na maisha yake kama kawaida.

Kuna watu hapa wanajivika upofu eti Makonda ana hati halali kama vile hawakuwepo hapa nchini na hawajui yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia. Pamoja na uchafu mwingi wa GSM lakini kwenye hili nyumba atakuwa alitoa hati kwa Makonda mbele ya manati ya mzungu au alitishiwa kupewa kesi ya uhujumu/madawa maana ndio ilikuwa michezo yake zama zile. Na ndio maana anaidai nyumba yake kwa nguvu na uchungu mkubwa.
 
Makonda sio sawa na wewe, mimi au yule.
 
But reality still in real.
Tungewavua nguo kwa maovu yenu mna bahati.

Although msimpige mwenzenu mawe huku dhambi zenu zipo pembeni zikiwasubiri mmalize kurusha mawe.
Hatuwezi kuukalia kimya UFEDHULI wa Makonda eti kwa sababu na sisi tuna dhambi zetu. Dunia haiendi hivyo, huyu Bashite na Sabaya walikuwa wanamtumikia DIKTETA Magufuli wakidhani hawezi kutoka madarakani au kufa. Walikuwa sawa na Bob Astles na Maliyamungu chini ya Iddi Amini.

"Mkundu ukifa mavi hutawanyika",
 
Kuna mbunge aliwahi kulalamika juu ya utajiri wake wa haraka mwanzoni kabisa mwa ukuu wake wa mkoa sikumbuki alikuwa nani, leo ndiyo naelewa kumbe alishuhudia mambo mengi
Alikuwa Joseph Selasini aliyekuwa Mbunge wa Rombo kupitia CHADEMA
 
Una uhakika unachoongea kuhusu Bakhresa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…