Nsalaga Uyole
Member
- Mar 1, 2020
- 56
- 47
Inaruhusu kila kitu chenye maslahi kwa wakubwa,inazuia kila kitu kisichokuwa na maslahi kwao.Hivi katiba yetu inaruhusu mheshimiwa Rais kuomba kujengewa nyumba na raia?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inaruhusu kila kitu chenye maslahi kwa wakubwa,inazuia kila kitu kisichokuwa na maslahi kwao.Hivi katiba yetu inaruhusu mheshimiwa Rais kuomba kujengewa nyumba na raia?
Mnapenda uchonganifu na umbea. Fanyeni kazi muda wa kazi huu
Ni kwasababu tu nchi yetu ndio hii Tanzania, ukiwa rais/waziri uko juu ya sheria.Nadhani GSM kama wana akili waache kucheza michezo ya wanasiasa. Hakuna aliyejua Nape atakuja kuwa Waziri karibuni.
Makonda anaweza kuja kuwa Rais au Waziri na mwenye ma mlaka ndipo utakapoona GSM wanakimbia nchi.
Hofu ya madaraka makubwa ya kifalme yanayotiririka kutoka ofisi namba moja.Na huyo GSM umesha jiiuliza kwa nini wampe Mkuu wa Mkoa wa DSM zawadi yenye thamani kubwa Kama hiyo!? What do they wanted in return kutoka kwa Mkuu,ambacho hawajakipata au hajakitimiza na wakaamuwa wamdai Mali yao waliompaa!?
Nafuu tuwatetee hao unaowaona waarabu kuliko mtanzania mwenzetu aliyempiga Jaji Joseph Warioba, alimuua Ben Saanane na kumwagia risasi 16 Tundu Lissu
Kwa mzungu hiyo ni sawa kwa sababu ni wenzetu ! Ila kwa mmanga hapana maana si mwenzetu !! Hizo ni chuki kwa wale ambao sio wa upande wetu !! Huo ni ubaguzi usiotakiwa hapa duniani !!
Hakuna kitu kama hicho !! Tembea duniani uone watu wanavyoishi !! Utajifunza mengi
Hunasa kwenye tundu bovu ??!! Au ?!
Mbona wwe Makonda hajakusingizia kua unauuza madawa ya kulevya!? "If you don't know the rules don't play the game'!!! Hayo Maneno alikuwa anapenda sana Marehemu Dingi yangu kuniambia! nilipokua mdogo sikumuelewa,hadi nilipokua Mkubwa na kuanza ku play the game ndiyo nikaanza kumuelewa! Na masikini wakati naanza kuelewa Maneno ya Dingi na yeye ndiyo Umauti ukamnyemelea na kumchukuwa!!
Siasa za kiafrika is unpredictable kwaiyo kaa kwa kutulia usiongozwe na hisiaAkili za matope, shuleni ulienda kusomea ujinga?
Hii imesababisha malori mengi ya Tz yasajiliwe Zambia, udikteta umefukuza wawekezaji wengi sana awamu iliyopitaKuna mmoja ni dereva wa malori ya mizigo kwenda nje hasa Congo na Zambia.. Aliniambia boss wao anasumbuliwa na watu wakidai wametumwa na mamlaka.
Mara ni lazima uchangie mifuko ya cement 500 pamoja na nondo za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu eneo fulani..Kilichomshangaza akaona taarifa ile kwenye TV mifuko 200 tuu tena nondo hazikuwekwa.
Kila mwezi anagongewa mlango na watu kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya..nk wakisema order kutoka juu.. Tunahitaji 40 M kwa ajili ya eneo hili nk.. Ilibidi nusu ya malori yake abadili no kuwa za Rwanda na Zambia.. Ili ionekane kampuni imeyumba na hana uwezo wa kila mwezi kuchangia mahela ya miradi ya maendeleo.
Mkuu wanasiasa si watu wa kuweka nao bifu hasa unapokuwa mfanya biashara. Kama GSM wana mtu wa PR wataliona hili nalosema. Hivi nani alijua Makala atakuja kuwa mkuu wa mkoa wa Dar???? Ninachomaanisha hapa ni kuwa wanasiasa wana mitaji mikubwa ya network, mtu anaweza kuwa idle kwa muda ila siku mtu wake akimkumbuka basi anaweza kulipiza kisasi. Msipe kichwa GSM. Na kumbukeni Makonda na Mama ni kitu kimoja.
Kuna mmoja ni dereva wa malori ya mizigo kwenda nje hasa Congo na Zambia.. Aliniambia boss wao anasumbuliwa na watu wakidai wametumwa na mamlaka.
Mara ni lazima uchangie mifuko ya cement 500 pamoja na nondo za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu eneo fulani..Kilichomshangaza akaona taarifa ile kwenye TV mifuko 200 tuu tena nondo hazikuwekwa.
Kila mwezi anagongewa mlango na watu kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya..nk wakisema order kutoka juu.. Tunahitaji 40 M kwa ajili ya eneo hili nk.. Ilibidi nusu ya malori yake abadili no kuwa za Rwanda na Zambia.. Ili ionekane kampuni imeyumba na hana uwezo wa kila mwezi kuchangia mahela ya miradi ya maendeleo.
Ukiona hivyo Basi walikuwa na vitu vya ovyo nyuma yao au walikuwa wanafanya ya ovyo. Huwezi kukubali kirahisi kufanya jambo kama Unajua huna cha kuficha.
Makonda sio sawa na wewe, mimi au yule.Kwenye hili suala la Makonda kwa kweli kabisa serikali haifanyi sawa. Kila siku serikali inahubiri watu wasijichukulie sheria mkononi na watii sheria bila shuruti. Lakini ninapokuja suala la Makonda inapata kigugumizi kwa mtu ambaye hata wito wa mahakamani anagomea yeye ni nani katika nchi hii. Na inaleta picha gani kwa watanzania milioni 60 wa nchi hii. Watu wanamlaumu hapa GSM lakini inawezekana walishatoa taarifa lakini zikakaliwa nao wao wanamuona mporaji yupo anatamba na hachukuliwi hatua sasa kwanini wasifanye hayo wanayofanya hata kama sio sahihi? Mtu ana tuhuma lukuki halafu eti anaachwa mtaani mpaka ajitokeze mtu binafsi Kubenea amshtaki wakati vyombo husika vinavyoendeshwa kwa kodi na tozo zetu vipo. Tena mtu huyo aliyejitolea anapata vikwazo kibao vya kumfisha Makonda kwa Pilato.
Je vyombo vya dola havioni kuwa vinachangia katika suala hili la Makonda? Na kama GSM kaanza kudai mwenyewe je ni wa ngapi wapo njiani kwenda kuchukua mali zao kwa Makonda? Na ni wangapi watadai kistaarabu? Mtu akifanya makosa makubwa mara nyingi Polisi au Mahakama huwa zinamuweka sehemu salama lupango ili wenye hasira kali wasimdhuru, je vipi kwa Makonda kwa nini asiwekwe sehemu salama ambapo ni lupango ili wenye hasira kali wasije kumdhuru?
Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama kikubwa cha upinzani hapa chini alituhumiwa tu ugaidi wa kumbumba akafikishwa mahakamani na akakaa ndani mpaka alipofutiwa mashtaka. Marehemu Ditopile alikuwa "best man " wa raia namba moja wa nchi wakati huo alituhumiwa kuua dereva dala dala alifikishwa mahakamani na akakaa ndani ili watu wenye hasira kali wasije kumdhuru ingawa baadaye alipata dhamana. Na mifano ipo mingi kama ya wa kina Mramba, Yona , Kiula, Sabaya, n.k. Sasa kwa Makonda basi tuelezwe ni kitu gani hasa "special" alicho nacho ambacho kinazuia asifikishwe mahakamani kujibu tuhuma. Na kama ni msafi mahakama si itamsafisha na kumuachia huru aendelee na maisha yake kama kawaida.
Kuna watu hapa wanajivika upofu eti Makonda ana hati halali kama vile hawakuwepo hapa nchini na hawajui yaliyokuwa yanafanyika nyuma ya pazia. Pamoja na uchafu mwingi wa GSM lakini kwenye hili nyumba atakuwa alitoa hati kwa Makonda mbele ya manati ya mzungu au alitishiwa kupewa kesi ya uhujumu/madawa maana ndio ilikuwa michezo yake zama zile. Na ndio maana anaidai nyumba yake kwa nguvu na uchungu mkubwa.
Ni mafia kwa msambwanda alionao labda?Paul Makonda huyo uliyemdhulumu NI Mafia. Hilo NI angalizo tu
Hatuwezi kuukalia kimya UFEDHULI wa Makonda eti kwa sababu na sisi tuna dhambi zetu. Dunia haiendi hivyo, huyu Bashite na Sabaya walikuwa wanamtumikia DIKTETA Magufuli wakidhani hawezi kutoka madarakani au kufa. Walikuwa sawa na Bob Astles na Maliyamungu chini ya Iddi Amini.But reality still in real.
Tungewavua nguo kwa maovu yenu mna bahati.
Although msimpige mwenzenu mawe huku dhambi zenu zipo pembeni zikiwasubiri mmalize kurusha mawe.
Alikuwa Joseph Selasini aliyekuwa Mbunge wa Rombo kupitia CHADEMAKuna mbunge aliwahi kulalamika juu ya utajiri wake wa haraka mwanzoni kabisa mwa ukuu wake wa mkoa sikumbuki alikuwa nani, leo ndiyo naelewa kumbe alishuhudia mambo mengi
Una uhakika unachoongea kuhusu BakhresaHiyo Mali Makonda hajanunuwa,hao GSM walimpa Kama zawadi! Sasa jiuulize Mfanyabiashara Mkubwa unampaje Mkuu wa Mkoa zawadi yenye thamani kubwa Kama ile!? Je Wanataka nini in return!? Mbona Konda Boy hajapewa Nyumba au Kiwanja na Baharesa!? Baharesa biashara zake zimeonyooka ndiyo maana hana hata muda wa kujipendekeza kwa Viongozi! Ukiona Mfanyabiashara Mkubwa anajipendekeza kwa Viongozi ujuwe huyo ana machafu yake kwenye biashara zake na anataka Ulinzi tu!!