Video: Tundu Lissu atoa ufafanuzi wa hoja aliyoitoa Babati Aprili 26, 2024 kumjibu Fatma Karume kuhusu 'Ubaguzi na Muungano wetu'

Kidogo nashindwa kuelewa wewe na mimi tunapishana wapi katika hili.

Mimi nilielewa, na siku zote najuwa kwamba mbunge anayechaguliwa kwenye jimbo la Zanzibar, anachaguliwa na watu wachache sana, sana; ukilinganisha na mbunge anayechaguliwa katika jimbo la uwakilishi Tanganyika.
Na kwa maana hiyo, mbunge wa Zanzibar huwakilisha watu wachache sana ukilinganisha na Mbunge wa Tanganyika.

Hebu nieleze, hili lipo sawa, au bado ni tofauti na wewe unavyo elewa?

Nakuomba jibu lihusu swali hilo tu pekee kabla ya kwenda mbele zaidi na maelezo mengine.
 
Unaumia ukiwa mchambawima, mchafukoge, makunduchi, kibandamaiti au wapi?
 
Hapana.
Wakitaka kuitawala Zanzibar ni kazi rahisi kabisa.
Ukweli halsi ni kinyume na hivi unavyodhani wewe. Huenda huijui Zanzibar.
ni kikundi kidogo sana kilichoko Zanzibar ambacho hupiga kelele zaidi ya wingi wao, hasa toka Pemba.
Kwenye swala la maslahi ya Zanzibar, Wazanzibari hawatofautiani.
 
Kidogo nashindwa kuelewa wewe na mimi tunapishana wapi katika hili
Mimi kumwuita Lissu "MBAGUZI" ndio tofauti zetu. Uchaguzi wa Lugha na hisia za mwanasiasa ndio mwelekeo wa ubatizo wa jina lake.
Upo sahihi kabisa. Ni ukweli usiopingika. (Usisahau kuwa Zzibar ni nchi iliyokuwa na utaratibu wake na utamaduni wake hata kabla ya kuungana).
Kwa kuongezea tu, hata Tanganyika mbunge wa Mafia anawapiga kura wachache sana ukilinganisha na mbunge wa Kawe au Kinondoni. Hali hii utaipata mahali pengi hata huku Tanganyika.
 
Wewe huna ujualo kuhusu hayo mambo halafu unajifanya mjuaji wakati wewe ni mbumbumbu
 
Lissu atatuelewa tu. Msikilize alivyowahutubia waandamanaji Morogoro tar 30/4. Katoa hotuba nzuri isiyo na mihemko na hisia za kibaguzi ukilinganisha na ile aliyoitoa babati. Haya ni matokeo ya kumpigia kelele! Tutaendea kumpigia kelele kila anapotereza, lugha za kibaguzi hazina afya kwa Taifa. Ajirekebishe!

Shukurani kwa wote waliosimama kidete na kumrekebisha, kumuonya na kumsahihisha Lissu katika hotuba yake ile ya KIBAGUZI.

Iko hivi: Naweza nikapingana na maamuzi ya kuhamishia makao makuu kwenda Dodoma. Hapa chini natoa hotuba mbili, moja ya kibaguzi na nyingine ya kihoja:
1) Mzananki mmoja, kutoka Butiama anaamua kuwahamisha nyie wagogo na ardhi yenu yote ichukuliwe na Serikali. Ngombe zenu mtafugia wapi? hakuna! Kwanini huyu Mzanaki kutoka huko Kaskazini Mara asinyanganye ardhi ya wakulya huko kwao nakujenga makao makuu huko.....Imejaa hisia za KIBAGUZI.
2) Rais na serikali ya Tanzania imeamua kuhamishia makao makuu Dodoma. Kitendo hiki kinamadhara makubwa kwa wakazi wa Dodoma, ikiwa pamoja na kuhamiswa toka katika ardhi yao ambayo itachukuliwa na serikali...... Unajenga hoja.
 
Akimalizana na Zanzibar atahamia katika siasa za Majimbo. Kwa mihemko hii ya Lissu ndio utajua kuwa Singida sio Arusha au Moshi. Kila jimbo litakuwa na sheria zake na Polisi wake. Isome katiba ya CHADEMA na Ilani zao za uchaguzi 2010, 2015, 2020. Utanielewa tu.
 
Ukweli halsi ni kinyume na hivi unavyodhani wewe. Huenda huijui Zanzibar.
Kwenye swala la maslahi ya Zanzibar, Wazanzibari hawatofautiani.
Wanatofautiana sana inapokuja kwenye maslahi ndani ya CCM au nje; ACT Wazalendo.
Matatizo ya Muungano wetu yapo kwenye makundi hayo mawil, huko visiwani. Kati ya wanaolinda "Mapinduzi Tukufu" yasizolewe na wale wasio yatambua mapinduzi hayo.
Kuwemo kwenye muungano ndiyo kete wanayoitumia kundi la Mapinduzi Tukufu, kuwatumia waTanganyika kuhakikisha usalama wao.
 
Mimi kumwuita Lissu "MBAGUZI" ndio tofauti zetu. Uchaguzi wa Lugha na hisia za mwanasiasa ndio mwelekeo wa ubatizo wa jina lake.
LOoo. Kumbe?
Hii itakuwa ni mada nyingine tunayoweza kuitumia kujadili tofauti zetu katika uelewa huo.
Yeye kaueleza anaoona ni ubaguzi wa waZanzibari dhidi ya waTanganyika; wewe ukaona ni mbaguzi; ila wewe unabaki ukiwa siyo mbaguzi!
 
Hapana, mfano wa Mafia siyo sahihi hata kidogo katika kuelezea uwakilishi wa wabunge toka Zanzibar. Mkuu, kama ni maswala ya utamaduni, hata huko Tanganyika kulikuwepo tamaduni nyingi tu kila sehemu. Mnapoingia kwenye muungano ni muhimu muwe na mambo mengi yanayowaunganisha na kuyakubali kwa kuweka baadhi ya tamaduni zenu binafsi pembeni kwa manufaa ya muungano wenu. Huwezi kuingia kwenye Muungano ili ukadumishe tamaduni zako huko bila kujali wengine ulioungana nao huko.
 
Wanatofautiana sana inapokuja kwenye maslahi ndani ya CCM au nje; ACT Wazalendo.
Uko sahihi unapozungumzia vyama vya siasa, ila linapokuja swala la maslahi ya nchi hakuna tofauti wote huwa na msimamo mmoja.
Kuwemo kwenye muungano ndiyo kete wanayoitumia kundi la Mapinduzi Tukufu, kuwatumia waTanganyika kuhakikisha usalama wao.
Ni kweli ukizungumzia Watanganyika kuhakikisha usalama, ila bado linapokuja swala la maslahi ya Zanzibar wanakuwa na msimamo mmoja usioyumba.
 
Mi nadhani wewe na mimi tunakubaliana kwa kiasi kikubwa. Sioni sababu ya kutafuta visababu vinavyotutenganisha hapa.
 
Huna hoja yeye kafafanua katiba kaelezo ubovu wakatiba hajasema kwamba wazazibari ni wabayal Wala hajawatukana
 
Huja mwelewa lisu au unajizima Data, hajasema tuwachukie MAJIRANI anfafanua katiba ambayo kwayo ndio inaleta ubaguzi
 
Naona kuna shida ya kuelewa point kuu ninayotaka kuzungumzia. Nilipoandika mfano wa Mafia, lengo kuu lilikuwa kwa ujumla, si Zzibar tu bali hata bara ubunge kati ya jimbo na jimbo haulinganishwi kwa idadi ya watu.
Nilichotaka kusema, Lissu kama anataka kuwa muwazi basi vile vile alaumu kwanini Mafia ina mbunge mwenye hadhi sawa na mbunge wa Kawe, kama idadi ya watu ndio vigezo?

Suala la Muungano. Kwanza tukubaliane kuwa ni nchi 2 ndio zilizoungana, sio mikoa 2. Kumbuka Zanzibar ilkuwa na kiti umoja wa mataifa kilichokuwa na uzito sawa na Tanganyika. Tunaposema Tanzania imepiga kura umoja wa mataifa kupitisha suala fulani, kura hiyo ina uzito sawa na kura ya Burundi na Rwanda zenye watu chini ya 6 mil kila moja. Hivyo suala la nchi huheshimiwa kama nchi bila kujali kuna watu wangapi. Twende pamoja!

Mwaka 1964 Tanganyika ilikuwa na watu 12 milioni na Zanzibar takriban laki 3.5. Ni nchi mbili zenye uzito sawa kimataifa. Hivyo kulihitajika majadiliano yenye uzito sawa kwa kila upande. Katika kulinda hadhi ya watu wa Zanzibar ambao walikuwa 3.5 milioni, na Tanganyika Mengi yalifikiwa. Unaweza kukubaliana na baadhi ya mambo au hapana. Kwa maneno mengine Kila nchi ilitakiwa kuwa na kura ya Veto kwa kila nchi.
 
Bado, hata Wilaya ya Mafia yenyewe, yenye wananchi zaidi ya 67,000; na ukubwa wa kilomita za mraba 640 huwezi ukailinganisha kwa vyovyote na jimbo la uchaguzi lolote toka Zanzibar; hata kwa vigezo hivyo pekee. Sasa tuliungana ili iweje, Zanzibar ifaidi matunda ya Muungano bila ya yenyewe kupoteza chochote? Iendeshe mambo yake yenyewe bila ya kujali kuwa imo kwenye Muungano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…