Kidogo nashindwa kuelewa wewe na mimi tunapishana wapi katika hili.Dodoma ninayoizungumzia ni ile aliyoizungumzia Lissu katika Video. Kama hujaisikiliza hiyo video (ipo kwenye uzi huu), tafadhali isikilze kwanza ndio twende pamoja. Katoa mfano wa idadi wapiga kura wa Dodoma na wabunge wake akilinganisha na wale wapga kura wa Zanzibar na wabunge wake. Kazi kwako, ndio urudi tujadiliane.
Sifa za majimbo ya uchaguzi muulize Lissu, kwa maana mimi nikiziorodhesha hutridhika. Ngoja huyo mchungaji Lissu aseme hadharani. Ndio utajua kuwa una mchungaji BAGUZI, na hana tofauti na wale makaburu wa A. kusini ktk miaka ya 1960. Aende Ubelgiji akaishi huko.
Mimi nilielewa, na siku zote najuwa kwamba mbunge anayechaguliwa kwenye jimbo la Zanzibar, anachaguliwa na watu wachache sana, sana; ukilinganisha na mbunge anayechaguliwa katika jimbo la uwakilishi Tanganyika.
Na kwa maana hiyo, mbunge wa Zanzibar huwakilisha watu wachache sana ukilinganisha na Mbunge wa Tanganyika.
Hebu nieleze, hili lipo sawa, au bado ni tofauti na wewe unavyo elewa?
Nakuomba jibu lihusu swali hilo tu pekee kabla ya kwenda mbele zaidi na maelezo mengine.