Muungano wa kweli ni makubaliano kati ya pande mbili. Ni muhimu kufahamu kuwa muungano wa kweli hutanguliwa na kura za maoni kwa nchi zinazoungana. Hii inamaanisha kuwa Tanganyika wanapiga kura wenyewe na Zanzibar nao wanapiga kura wenyewe kama wanataka muungano. Hivyo kura za watanganyika 12 milioni (1964) uzito wake ni sawa na kura laki 3.5 za Zanzibar (Hapa ndio Lissu anafahamu wazi lakini anataka kudanganya watu na suala la Wabunge). Kama Zanzibar wakisema Hapana na Tanganyika wakasema Ndio, kisheria hapo hakuna Muungano.
Hakuna muungano wa aina moja, ni juu ya nchi mbili wamekubaliana nini. Hilo karatasi/contract ya Muungano ndio kila kitu na si maoni ya vijiweni. Kama karatasi limeandikwa kuwa Zanzibar itakuwa nchi yenye Rais wake na wawakilishi wake ndani ya Muungano itakuwa hivyo. Nawashangaa watu wanaolazimisha Zanzibar kuwa mkoa kwa kigezo cha idadi ya watu. Huu ni upotoshaji.
Kuna nchi zilizoungana kama Senegal na Gambia na kuitwa Senegambia. Lakini Muungano huo ulivunjika baadae baada ya Senegal kutaka kuifanya Gambia kama mkoa katika Muungano.
Wewe ni mtu mtulivu katika mijadala, nakupongeza kwa hilo.
Aya ya kwanza kuhusu kura ya maoni, ninakubaliana nawe kwamba wakati huu inafaa wananchi wahusishwe kuhusu huu muungano wetu; uendelee kuwepo, na kama uendelee uwe katika sura gani.
Najuwa unafahamu, kwamba wananchi hawakuhusishwa katika uamzi huo waasisi walpokubaliana pawepo na muungano. Hapa pia najuwa unaelewa kwa nini haikuwa hivyo.
Nafahamu pia kwamba, muungano ulivyo sasa, siyo ule uliokuwepo mwanzo. Maswala ya "kero nyingi za muungano" toka upande mmoja wa muungano ndizo zilizosababisha kwa kiasi kikubwa tukafikia hapa tulipo leo; kinyume kabisa na matarajio ya muungano walioutegemea waasisi; kwamba baada ya muda, tukisha zoeana vya kutosha na kuchanganyika kati yetu, hofu zilizokuwepo wakati ule zingekuwa zimepungua na kuruhusu muungano wa karibu zaidi. Badala yake, kero zilipo pamba moto, badala ya kuwa karibu, ndiyo tukawa tunatafuta njia ya kuua muungano.
Hili kundi linaloibua maswala ya kero kila mara, ni kundi lile lile lililokuwa haliutaki muungano toka mwanzo. Na kundi hili limepata nguvu zaidi walipopata wenzao waliokuwemo ndani ya CCM toka Zanzibar, ili wachochee kazi hiyo ya kuulegeza muungano ndani kwa ndani chamani.
Na kama nilivyokwisha sema huko nyuma, ndani ya CCM toka Tanganyika, kumekuwemo na ombwe la watu wanaoweza kusimama na kuutetea muungano. Huko kumejaa wanafiki tupu. Udhaifu huo ndio umetoa fursa kwa Zanzibar kuanza kufanya mambo yake ionavyo inawafaa wao badala ya kuangalia maslahi ya wote katika muungano
Watu wa CCM visiwani ndio walikuwa wamewashikiria kwa nguvu wenzao toka Tanganyika, kwa sababu tu za kulinda maslahi yao kwa jina la kuyaenzi Mapinduzi Tukufu. Na ni hawa, pamoja na kutekwa na lile kundi lisilo penda muungano, bado wanawang'ang'ania CCM wa Bara waendelee kuwakingia maslahi yao dhidi ya hao wasiotaka muungano.
Ni wakati mzuri sasa, huu muungano upekwe kwa wananchi, waamue wenyewe wanachotaka juu ya huu muungano.
Sasa hata hapa naona kuna shida, siyo hasa kwa upande wa Tanganyika; bali kwa upande wa Zanzibar. Pamoja na wingi wao ulivyo Tanganyika, hata wakiukataa muungano, kama lile kundi la CCM litapata waZanzibari wa kutosha kubaki kwenye muungano, Tanganyika hawezi kujitoa. Bila shaka hii ndiyo 'veto' uliyokuwa ukiizungumzia.
Hata ikitokea ikawa hivyo, maoni yangu ni kwamba kura hiyo ya maoni itatupatia fursa ya kuutazama upya muundo wa muungano wetu.
Kama kuna makosa ya kiuandishi humo ndani, naomba uniwie radhi, maana nilitiririka tu, yoka juu hadi mwisho.