Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji

Sasa kwanini ujimalize na ushajua ulipoangukia
 
Pesa jumla nilitupa kwenye betting toka nilipoanza 2013 mpaka sasa ni equivalent to milioni 20. Na bado kuna pesa nilitupa kwenye project mil 9. Kawaida tu usipagawe. Utazoea utasahau ndani ya muda mfupi. La muhimu acha kamari.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Nilijaribu niliweka buku ikapanda adi elf 5 nilipoweka iongezeke zaidi ikaliwa yote
Sina ham na aviator
Sasa kama buku iliniuma hivi je wewe wa milioni 7
Muhindi akamatwe🤣🤣🤣🤣
 
Kindege ni program ya kubet ipo kwenye playstore.
Unadownload na kuanza kucheza kwa kutia hela ili upate fedha.
Mh mbona Playstore hua haiweki app za betting? Hawa wamepenyaje
 
Pole sana mkuu, kubali kuwa umepoteza na anza upya ikiwezekana badili mazingira uza ulichonacho kaanze maisha upya sehem nyingine na usijejaribu kusema utairudisha hiyo hela na kutaka kuirudisha kupitia kamari, utapoteza kila kitu mpaka uhai.
Nishifikia asilimia 95 ya mawazo ya kujiua siku nilipomalizwa kabisa nikabaki na zero.

Ila kwa sasa niko 60 % karibu na kujiuq.

Hasa nikiwaza namna ya kuipata tena hiyo pesa, sina kazi, umri umesonga sijaoa ndiyo kunanipa stress kabisa.
 
Jipige kifuani mara3 kisha utamke maneno aya
->Mimi ni mjinga sana
->Mimi ni mpuuzi na kilaza kiwango cha Sgr
->Mimi ni Zumbukoko nimepeleka mafao yangu kwenye kamari

->Mimi nina nyota ya umaskini

ukisha maliza kutamka ayo njoo nikupe odds 5 za uhakika ufute huo ujinga ulio jaa akilini mwako
 
Pole sana kijana. Unaweza kunicheki pm kwa msaada zaidi. Tafadhali naomba usipuuze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…