Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji

Bora hata usikijue maana ukikijua unaweza kukijaribu.

Ukiingia kinakutamanisha kwa kukupa pesa kubwa ndani ya dakika moja alafu ukinogewa ujue ndiyo unafilisika.

Akilia inakuja kuzinduka una buku kutoka milion
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nishifikia asilimia 95 ya mawazo ya kujiua siku nilipomalizwa kabisa nikabaki na zero.

Ila kwa sasa niko 60 % karibu na kujiuq.

Hasa nikiwaza namna ya kuipata tena hiyo pesa, sina kazi, umri umesonga sijaoa ndiyo kunanipa stress kabisa.
Hayo mawazo ya kujiua yafute kabisa maana unayaruhusu we mwenyewe, anza upya tafuta kibarua cha kujimudu, jipange jipe muda then tafuta mwanamke wa kuanza nae maisha, kamari hiyo ya hivyo acha kabisa bora ubet mpira kuliko hayo ma aviator.

Naelewa situation yako maana hata mim nilipitia haya lakini nikavuka salama. Kukata tamaa ni mwiko kumbuka sababu ni tamaa zako, R I P kwa hela zote zilizopotea ukiwa unatafuta hela.

Aisee katika kitu namshukuru Mungu mimi ni mgumu sana kukata tamaa hata niwe kwenye gumu gani najua nitavuka tu hata kama litanigharimu na kuniumiza. We mkamaria kama umeweza maumivu ya kupoteza unashindwaje kuanza upya? Komaa kiume dunia na mafanikio haiitaji watu wanyonge, be strong meeeeeen, act tough meeeeeen.
 
Nice words.

Mpaka hapa nahisi nimepunguza asilimia kadhaa za karibu na kifo.
 
Nice words.

Mpaka hapa nahisi nimepunguza asilimia kadhaa za karibu na kifo.
Achana na mawazo ya kujiua sio solution ya matatizo yako, ukipitia changamoto yeyote acha kabisa kuwaza kifo kama suluhu, huo ni udhaifu uliotukuka.

Kama mimi nilipitia hayo na nikavuka licha ya maumivu makali kwanini wewe ushindwe?

Uza simu anza upya tafuta cha kufanya kadri muda unavyoenda mambo yatakuwa sawa.

Epuka kuazima hela kwa watu na kuahidi kurejesha ukiwa na hiyo simu yenye uwezo wa kukufanya ucheze aviator, kwa sasa hata ukipewa hela utakimbilia kucheza tena(najua hili wengi watakataa/utakataa) ila nimepitia na ninajua kwa kuyaona kwa wengi. Jijenge mwenyewe taratibu taratibu na usifosi uazime hela usiomudu kurudisha, utajivunjia uaminifu na upo kwenye kipindi kigumu cha kusimama upya kuna muda utahitaji msaada na wakukusaidia ndio hao wanaokuamini, usiwapoteze.

Nakuandikia magazeti kwa sababu nimeyapitia haya na sipendi kuona mtu anayapitia naelewa maumivu yake.
 
Aviator wakat naijua niliambiwa na walionielekeza kuwa niweke pesa ndogo sana kujifunza, niliambiwa mia 2 lakin mimi nikaweka 1000 ndani ya dakika chache nikapiga 10000

Nikaona mbona mchezo ni rahis Sana, nikaamua kudeposit 60,000,
Kindege kilivyoona hyo hela kikapandisha mashetani, yaan sasa kikawa hakihesabu tena,kikiruka kidogo kinaanguka mpaka hela yote ikaisha
 
Mbona zako waga unatunga na bado tunasoma, Kwahiyo unataka uendelee kutunga wewe tu au sio

Kama katunga fresh, sie hayatuhusu kikubwa alichotunga kuna watu kinawatokea kwenye real life kila siku
MI siandiki msome.
 
Muda muda muda muda.

Napata tumaini kupitia wewe kwa sababu umeamua kuishi kwenye hisia za maumivu yangu.

Ila Baba muda plus rasilimali ndiyo changamoto.

Imagine mwanaume 30 years single, economically kwa sasa niko zero, job opportunity zero, rasilimali ya kuanza nayo ili niinuke upya nijitetee ni zero.

Nilipata opporrunity ya kutokea (hiyo 7 milion) lakini nika lose the chance.

Ama kweli hakuna rangi nitaacha kuona kama wadau wanavyosema.

Kila nikiwaza nilicho kipoteza nahisi moto unaniunguza tumboni.

I feel more than hell.

Bora basi ningepoteza 7 milion lakini nna kazi ya kuingiza chochote kwa mwezi, nako hamna.

Ningepoteza basi seven milion lakini nna rasilimali ya kuuza nianze upya, nako hamna zaidi ya hii samsung galaxy A 14.

Yaana mimi najiona kabisa ni marehemu anaesogeza siku tu hapa
 
kuna haya makorokoro

hawa wachina wanayoyamiliki ni wakutimua upesi sana mosi yana dhalilisha sarafu yetu,kuzichakaza na kuleta umasikini hivyo kuongeza utegemezi

haingi akilini mchina anamka asubui kukusanya pesa kijingajinga tuh
 
Miaka 20 iliyopita nikiwa na umri wako huo nilipata janga kubwa sana nikaona dunia si yangu tena. Nilifanya upambavu mkubwa sana na nikapoteza kazi nzuri huku jela ikinisubiri. Hapo nina familia na wananitegemea mimi, nilichukua uamuzi wa kujitoa roho, nikanunua frajili 20, nikachukua bia (Tusker) moja nikachanganya na Konyagi nikabugia yote. Nilikwenda kuponea hospitali kwa msaada mkubwa wa wife. Leo maisha yanaendelea na yote yaliyopita yalishapita. Tulia jipange upya, maisha ni zawadi muhimu sana na thamani yake haipimiki, tunapaswa kuyakumbatia kwa nguvu zetu zote hadi pale yatakapoondolewa kwetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…