Nilikuwa chuo nikajichanganya biashara flani inafanywa kienyeji na pisi kali. Nikaona potential ya kuifanya vyema kwa concentration, sikupata mafanikio kivile. Baadae ndio nikajua wala hata hawaitegemei kuishi ndio maana nashangaa wanaifanya kizembe, nikaacha kujipa stress.
Tangu hapo nikagundua kitu ambacho hakitajwi kwenye business research, fanya research ya kina nani wanafaa biashara flani, the same thing ambavyo mdada mfupi una kitambi huwezi kuwa air hostess ndivyo biashara nyingine zinakataa watu, mdada una mapunye unauzaje skin products.
Na ukitaka kuiiga biashara chunguza wanaoifanya hiyo wanaitegemea kuishi au kuna kitu kingine. Sio uko Mwenge unauza simu pekee unashindana na mwingine ana mishe nyinginezo uko. Kama mnafanana vyanzo vya mapato hapo tafuta unakwama wapi