Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wawadanganye wajinga wengi hii ni dunia nyingine kabisa hakuna jambo hata moja litakalojificha kwa namna yoyote ile tusubiri 2025 tukawashtaki kwa wanannchi.
.Kwani kwenye huo mkataba kuna vifungu vya Qur'an na Biblia kiasi kwamba viongozi wa dini wazungumze na waziri??- ni kwanini wasingezungumza mapema kabla ya mkataba kutiwa saini ??
Kwa nini mkutano kama huu hakuitisha kabla ya kusaini Mkataba??
Nguvu wanayo tena kubwa sana ila huwa hawaitumii kwa mambo ya kiduniadunia kama siasa, kesi na vitu vya hivyo. Gusa masilahi ya kiroho ya dini yao uone shughuli.Labda viongozi wa Kikristo. Wa Kiislamu hawana nguvu kihivyo.
.Halafu ni nchi gani nyingine ambayo walipouza bandari waliita viongozi wa Dini ?
Wewe agreement umeiona? Wapi?Asante kwa ufafanuzi.
Utaratibu wa kuanza kufanya hizo amendment mbona hautangazwi.? Haya mapungufu yaliyoonekana kwa Sasa , kwa nini yasiwe amended Sasa?
Kama Mkataba wa Fei Toto ulishindikana kutafsiriwa itakuwa huu wa Likampuni la Dunia😀😀An agreement is not enforceable by law and, by the consent of the parties, it ca be ammended at any time
Tatizo lenu mnapewa kwenye mitandao extracts za vifungu vya kwenye mikataba mingine halafu manaambiwa kuwa ni vya agreeement kati ya DP WORLD na TPA. Mbona hili swala liko wazi sana na wala halihitaji mjadala wa nguvu kiasi hiki?
Halafu shida ni ni nini, ni sheria au ni Kiingereza cha kisheria?
.Chadema 2025 mmsha pata agenda,hata sisi CCM hatutaki hii kitu.tumieni hiyo nafasi vizuri
Kakobe,Boganza,na wengineo walikiwasha awamu ya Tano.Askofu Gervais Nyaisonga huwa ni kibaraka wa CCM, bora angekuwepo katibu mkuu wa tec Dr Charles Kitima
Acha uzushi. Spika wa bunge kaongea wazi kwamba mkataba umeletwa bungeni baada ya kusainiwa. Halafu jiulize Kama hayo makubaliano sio enforciable by law juzi bunge lilikiwa linapitisha Jambo gani?. Kama halina nguvu kisheria lilienda bungeni kufanya Nini? Acha upotoshaji.Wewe agreement umeiona? Wapi?
Wasikilize wabunge wako pamoja na Waziri wako; acha kuhangaika na upotoshaji wa kisiasa ulioko kwenye mitandao
Kakobe alikiwasha akafanyiwa audit ya maana , akaufyataKakobe,Boganza,na wengineo walikiwasha awamu ya Tano.
[emoji119][emoji119][emoji119]
Punguza upotoshaji. Eti kuuziana ng'ombe. Hayo uliyoandika ungeenda kumwambia spika Tulia wa bungeni aliyetuambia mkataba umeshasainiwa ndio maana umeletwa bungeni kupitishwa na Bunge ili iwe sheria ya kimataifa au tuseme iwe na binding force under international tribunals and courts. Acha kupotosha.Hakuna mkataba uliosaniniwa kwa sasa ila ni makubaliano tu ambayo yapo kwenye maandishi
Kilichotokea ni kwamba TUCHUKULIE MFANO kwamba wewe nyumbani kwako unafuga mbuzi, na mimi kwangu nafuga ng'ombe. Ikafikia mahali tukaamua mimi na wewe tushirikiane kuchunga mbuzi na ng'ombe zetu kwa zamu na hivyo vijana wetu wachungaji wakakutana na kuweka makubaliano hayo kwenye maandishi kwamba tutaKapokuwa tumeanza ushirikaino wetu, vijana wangu kutoka nyumbani kwangu MZEE A watakuwa wanachunga ng'ombe na mbuzi kwa wiki moja, halafu baada ya hapo wanachunga vijana wako wewe MZEE B
Hadi kufikia hapa MJI WA MZEE A ukawa umeweka maubaliano ya aina hii na MJI WA MZEE B ambayo yatakuja kutekelezwa baadaye
Muda ukishafika, wachungaji wenyewe sasa (tuseme MCHUNGAJI A KUTOKA MJI WA MZEE A na MCHUNGAJI B KUTOKA MJI WA MZEE B ) watasaini sasa mkataba wao wawili unaosema kuwa kuwa kila mmoja wao atakuwa anachunga mbuzi na ng'ombe kwa wiki moja, halafu baada ya hapo anachukua zamu mwingine
Kwa hiyo hadi hapa, WACHUNGAJI A NA B bado hawajasaini mkataba wowote, isispokuwa kuna makubaliano tu kati ya MIJI YA WAZEE WAO A NA B
Ikija kutokea tuseme muda wa kuweka mkataba kati ya wawili hawa ukafika halafu mmoja wao (MCHUNGAJI A AU MCHUNGAJI B) akawa hajaridhika, mkataba kati ya wachungaji hawa hautawekwa na hakuna mmoja wao atakayekwenda kushtaki mahakamani kwa sababu hapajawahi kuwepo mkataba kati yao, isipokuwa makubaliano tu kati ya KAYA/ MIJI ya wazazi wao
Hakuna mkataba wowote ambao umeshasainiwa kati ya TPA na DP WORLD
Hadi muda huu, hakuna mkataba wowote ambao umeshasainiwa kati ya TPA na DP WORLD Vile vile hakuna mkataba uliosainiwa kati ya nchi yetu na Dubai, isipokuwa kilichosainiwa ni AGREEMENT kati ya Tanzania na Dubai; kwa Dubai kuwekeza kwenye sekta ya Bandari NOT ALL AGREEMENTS ARE CONTRACTS, BUT...www.jamiiforums.com
Changamoto hizo zingejadiliwa na kufafanuliwa vizuri;Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na viongozi wa dini mbalimbali kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.
Mkutano huo unafanyika kwenye Ukumbi wa Kurasini Centre, TEC Jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 12, 2023.
Baadhi ya viongozi wa Dini mbalimbali walioshiriki katika mkutano huu ni;
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji, Moses Matonya
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Stanley Hotay
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Viongozi wa Dini kuhusu haki za kiuchumi na uadilifu wa uumbaji (ISCEJIC), Sheikh Khamis Mataka
Katibu mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKATWA), Alhaj Nuhu Jabir Mruma
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Pwani na Mashariki, DkT. Alex Malasusa
Mwakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA)
Prof. Makame Mbarawa...
Azimio hilo la ushirikiano limepitishwa na Bunge Juni 10, 2023, lakini pamoja na hivyo Serikali ya Tanzania imeona kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu mkataba huo.
Nchi yetu imeendelea kuwekeza katika Bandari zetu kwa vyanzo tofauti, pamoja na hatua mbalimbali, bado Bandari hazijafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
Mfano wa Meli kusubiri kutia nanga kwa Dar es Salaam ni siku tano tofauti na wastani wa siku 1 na saa 6 kwa Bandari ya Mombasa.
Ufanisi wa Bandari unashindwa kufikia kiwango cha kimataifa unatokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa mifumo mizuri ya TEHAMA na mitambo ya kisasa inayobadilika kutokana na teknolojia.
Athari za kutokuwa na Bandari ya kisasa ni meli kusubiri muda mrefu, kunakosababisha gharama kuongezeka, mfano kwa meli kusubiri kwa siku ni Tsh. Milioni 58.
Kukosesha mapato ambayo yangeweza kutumika kuboresha uchumi wa Taifa.
Ufanisi wa uendeshaji wa Bandari bado ni wa kiwango cha chini, Meli kutumia muda mrefu kupakua mzigo, meli kubwa kushindwa kuingia kwenye Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuingia Bandarini.
Kutokana na changamoto hizo, Mwaka 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba na Kampuni ya TICTS uliodumu kwa miaka 22, ulioipa haki kampuni hiyo katika Gati namba 8 hadi namba 11 wakati maeneo mengine yakiendelea kuwa chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Mwaka 2017 Serikali ilifanya mabadiliko makubwa katika mkataba lakini Mwaka 2022 Serikali iliona hakuna umuhimu wa kuendelea kufanya kazi na TICTS.
Desemba 2022, baada ya kuona mkataba huo hauendani ma matarajio ya Serikali, ndipo ikaanzisha mchakato wa kupata mwekezaji Bandarini.
Serikali ilipokea mapendekezo ya kampuni mbalimbali kutoka Hong Kong, Ubelgiji, India, Ufaransa, Denmark.
Baada ya mawasilisho ya kampuni hizo na sifa zao za kimataifa, Serikali iliamua kufanya mazungumzo na Kampuni ya DP World kutokana na uzoefu wake katika soko la Barani Ulaya, Asia, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Afrika.
DP World ina uzoefu mkubwa wa usafirishaji, Kampuni hiyo ina miliki zaidi ya meli 100 za mizigo.
Uamuzi wa Serikali iliona makampuni mengine yaliyoomba hayana uzoefu wa shughuli za uendeshaji wa Bandari Afrika wakati DP World inaendesha zaidi ya bandari 30 Duniani.
Februari 27, 2022, Serikali ilisaini makubaliano ya kulenga ushirikiano, baada ya hatua hiyo Serikali iliunda timu ya Wataalamu kufuatilia ushirikiano huo baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai.
Lengo la Mkataba huo ni kuweka msingi wa makubaliano ya Nchi na Nchi ili kuwezesha kuingia makubaliano ya mikataba mingine mbalimbali kama ya upangishaji na uendeshaji.
Kulingana na Katiba, Serikali ya Tanzania ilianzisha mkachato wa kuridhiwa na Bunge ili utekezaji wake uweze kuanza.
Mkataba huo umeweka vifungu muhimu kwa ajili ya kulinda maslahi ya Nchi ikiwemo ajira za Watanzania, ardhi ya Watanzania, ukomo wa mikataba, masuala yanulinzi na usalama na masuala mengine yote yenye umuhimu wa Nchi.
Mikataba hiyo pia itazingatia, kuweka bayana ukomo wautekelezaji, muda wa marejeo ya mkataba mwaka mmoja hadi mitano kutegemea na mkataba husika, viashiria vya utendaji wa mkataba, itakuwa chini ya ofisi ya Mwanasheria wa Serikali kwa kuzinagatia maslahi ya Taifa
Italinda wafanyakazi wazawa na kuwajenga uwezo, mifumo ya TEHAMA ya Kampuni ya DP World itasomana na ile ya Serikali.
Taasisi muhimu zote za Serikali zitaendelea na utekeleaji wake wa majukumu katika maeneo ya Bandari, mwekezaji atachukua hatua zote za Utafiti wa masoko ya Dar es Salaam.
Wewe ndio huelewi kitu. Eti agreement is not enforciable by law. Kasome definition ya Contract kwenye sheria za Tanzania. The Law of Contract Act RE 2019, section 2 a contract is any agreement enforciable by law. Wewe unatuambia agreement is not enforceable by law lakini sheria inatuambia Contract ni agreement enforceable by law. Tukusiklize wewe au sheria.An agreement is not enforceable by law and, by the consent of the parties, it ca be ammended at any time
Tatizo lenu mnapewa kwenye mitandao extracts za vifungu vya kwenye mikataba mingine halafu manaambiwa kuwa ni vya agreeement kati ya DP WORLD na TPA. Mbona hili swala liko wazi sana na wala halihitaji mjadala wa nguvu kiasi hiki?
Halafu shida ni ni nini, ni sheria au ni Kiingereza cha kisheria?