Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na viongozi wa dini mbalimbali kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.
Mkutano huo unafanyika kwenye Ukumbi wa Kurasini Centre, TEC Jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 12, 2023.
Baadhi ya viongozi wa Dini mbalimbali walioshiriki katika mkutano huu ni;
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji, Moses Matonya
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Stanley Hotay
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Viongozi wa Dini kuhusu haki za kiuchumi na uadilifu wa uumbaji (ISCEJIC), Sheikh Khamis Mataka
Katibu mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKATWA), Alhaj Nuhu Jabir Mruma
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Pwani na Mashariki, DkT. Alex Malasusa
Mwakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA)
Prof. Makame Mbarawa...
Azimio hilo la ushirikiano limepitishwa na Bunge Juni 10, 2023, lakini pamoja na hivyo Serikali ya Tanzania imeona kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu mkataba huo.
Nchi yetu imeendelea kuwekeza katika Bandari zetu kwa vyanzo tofauti, pamoja nah atua mbalimbali, bado Bandari hazijafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
Mfano wa Meli kusubiri kutia nangani kwa Dar es Salaam ni siku tano tofauti na wastani wa siku 1 na saa 6 kwa Bandari ya Mombasa.
Ufanisi wa Bandari unatokanana changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa mifumo mizuri ya TEHAMA na mitambo ya kisasa inayobadilika kutokana na teknolojia.
Athari za kutokuwa na Bandari ya kisasa ni meli kusubiri muda mrefu, kunakosababisha gharama kuongezeka, mfano kwa meli kusubiri kwa siku ni Tsh. Milioni 58.
Kukosesha Nchi mapato ambayo yangeweza kutumika kuboresha uchumi wa Taifa.
Ufanisi wa uendeshaji wa Bandari bado ni wa kiwango cha chini, Meli kutumia muda mrefu kupakua mzigo, meli kubwa kushindwa kuingia kwenye Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuingia Bandarini.
Kutokana na changamoto hizo, Mwaka 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba na Kampuni ya TICTS uliodumu kwa miaka 22, ulioipa haki kampuni hiyo katika Gati namba 8 hadi namba 11 wakati maeneo mengine yakiendelea kuwa chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Mwaka 2017 Serikali ilifanya mabadiliko makubwa katika mkataba lakini Mwaka 2022 Serikali iliona hakuna umuhimu wa kuendelea kufanya kazi na TICTS.
Desemba 2022, baada ya kuona mkataba huo hauendani ma matarajio ya Serikali, ndipo ikaanzisha mchakato wa kupata mwekezaji Bandarini.
Serikali ilipokea mapendekezo ya kampuni mbalimbali kutoka Hong Kong, Belgium, India, Ufaransa, Denmark.
Baada ya mawasilisho ya kampuni hizo na sifa zao za Kimataifa , Serikali iliamua kufanya mAzungumzo na Kampuni ya DP World kutokana na uzoefu wake katika soko la Barani Ulaya, Asia, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Afrika.
DP World ina uzoefu mkubwa wa usafirishaji, Kampuni hiyo ina miliki zaidi ya meli 100 za mizigo.
Uamuzi wa Serikali iliona makampuni mengine yaliyoomba hayana uzoefu wa shughuli za uendeshaji wa Bandari Afrika wakati DP World inaendesha zaidi ya Badari 30 Duniani.
Februari 27, 2022, Serikali ilisaini makubaliano ya kulenga ushirikiano, baad ayah atua hiyo Serikali iliunda timu ya Wataalamu kufuatilia ushirikiano huo baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai.
Lengo la Mkataba huo ni kuweka msingi wa makubaliano ya Nchi na Nchi ili kuwezesha kuingia makubaliano ya mikataba mingine mbalimbali kama ya upangishaji na uendeshaji.
Kulingana na Katiba, Serikali ya Tanzania ilianzisha mkachato wa kuridhiwa na Bunge ili utekezaji wake uweze kuanza.
Mkataba huo umeweka vifungu muhimu kwa ajili ya kulinda maslahi ya Nchi ikiwemo ajira za Watanzania, ardhi ya Watanzania, ukomo wa mikataba, masuala yanulinzi na usalama na masuala mengine yote yenye umuhimu wa Nchi.
Mikataba hiyo pia itazingatia, kuweka bayana ukomo wautekelezaji, muda wa marejeo ya mkataba mwaka mmoja hadi mitano kutegemea na mkataba husika, viashiria vya utendaji wa mkataba, itakuwa chini ya ofisi ya Mwanasheria wa Serikali kwa kuzinagatia maslahi ya Taifa
Italinda wafanyakazi wazawa na kuwajenga uwezo, mifumo ya TEHAMA ya Kampuni ya DP World itasomana na ile ya Serikali.
Taasisi muhimu zote za Serikali zitaendelea na utekeleaji wake wa majukumu katika maeneo ya Bandari, mwekezaji atachukua hatua zote za Utafiti wa masoko ya Dar es Salaam.