Viongozi wa Dini wanazungumza na Serikali kuhusu Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai
Mfano wa Meli kusubiri kutia nanga kwa Dar es Salaam ni siku tano tofauti na wastani wa siku 1 na saa 6 kwa Bandari ya Mombasa.
Sasa huu ndio ujinga ambao mtu hata Profesa anaweza kuwa nao na asijitambue kuwa ni mjinga.

Kama ni kweli, Kwamba "wastani wa meli kusubiri Mombasa ni siku 1 na saa 6", kwa nini tusijifunze kwa hao Mombasa wanavyofanya vizuri hivyo ili na sisi tupate mafanikio hayo?
Mombasa kwani imeuzwa lini?

Huyu Mbarawa nilimpa heshima kubwa sana enzi za Magufuli, na alipotumbuliwa sikuelewa kwa nini ilikuwa hivyo, kumbe naye kichwani ni mweupe kiasi hiki?

Naye ni FISADI mkubwa?
 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa anazungumza na viongozi wa dini mbalimbali kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai.

Mkutano huo unafanyika kwenye Ukumbi wa Kurasini Centre, TEC Jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu Juni 12, 2023.

Baadhi ya viongozi wa Dini mbalimbali walioshiriki katika mkutano huu ni;
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji, Moses Matonya
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Stanley Hotay
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Viongozi wa Dini kuhusu haki za kiuchumi na uadilifu wa uumbaji (ISCEJIC), Sheikh Khamis Mataka
Katibu mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKATWA), Alhaj Nuhu Jabir Mruma
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Pwani na Mashariki, DkT. Alex Malasusa
Mwakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA)

Prof. Makame Mbarawa...
Azimio hilo la ushirikiano limepitishwa na Bunge Juni 10, 2023, lakini pamoja na hivyo Serikali ya Tanzania imeona kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu mkataba huo.

Nchi yetu imeendelea kuwekeza katika Bandari zetu kwa vyanzo tofauti, pamoja na hatua mbalimbali, bado Bandari hazijafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.

Mfano wa Meli kusubiri kutia nanga kwa Dar es Salaam ni siku tano tofauti na wastani wa siku 1 na saa 6 kwa Bandari ya Mombasa.

Ufanisi wa Bandari unashindwa kufikia kiwango cha kimataifa unatokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa mifumo mizuri ya TEHAMA na mitambo ya kisasa inayobadilika kutokana na teknolojia.

Athari za kutokuwa na Bandari ya kisasa ni meli kusubiri muda mrefu, kunakosababisha gharama kuongezeka, mfano kwa meli kusubiri kwa siku ni Tsh. Milioni 58.

Kukosesha mapato ambayo yangeweza kutumika kuboresha uchumi wa Taifa.

Ufanisi wa uendeshaji wa Bandari bado ni wa kiwango cha chini, Meli kutumia muda mrefu kupakua mzigo, meli kubwa kushindwa kuingia kwenye Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuingia Bandarini.

Kutokana na changamoto hizo, Mwaka 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu iliingia mkataba na Kampuni ya TICTS uliodumu kwa miaka 22, ulioipa haki kampuni hiyo katika Gati namba 8 hadi namba 11 wakati maeneo mengine yakiendelea kuwa chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Mwaka 2017 Serikali ilifanya mabadiliko makubwa katika mkataba lakini Mwaka 2022 Serikali iliona hakuna umuhimu wa kuendelea kufanya kazi na TICTS.

Desemba 2022, baada ya kuona mkataba huo hauendani ma matarajio ya Serikali, ndipo ikaanzisha mchakato wa kupata mwekezaji Bandarini.

Serikali ilipokea mapendekezo ya kampuni mbalimbali kutoka Hong Kong, Ubelgiji, India, Ufaransa, Denmark.

Baada ya mawasilisho ya kampuni hizo na sifa zao za kimataifa, Serikali iliamua kufanya mazungumzo na Kampuni ya DP World kutokana na uzoefu wake katika soko la Barani Ulaya, Asia, Marekani ya Kaskazini na Kusini na Afrika.

DP World ina uzoefu mkubwa wa usafirishaji, Kampuni hiyo ina miliki zaidi ya meli 100 za mizigo.

Uamuzi wa Serikali iliona makampuni mengine yaliyoomba hayana uzoefu wa shughuli za uendeshaji wa Bandari Afrika wakati DP World inaendesha zaidi ya bandari 30 Duniani.

Februari 27, 2022, Serikali ilisaini makubaliano ya kulenga ushirikiano, baada ya hatua hiyo Serikali iliunda timu ya Wataalamu kufuatilia ushirikiano huo baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai.

Lengo la Mkataba huo ni kuweka msingi wa makubaliano ya Nchi na Nchi ili kuwezesha kuingia makubaliano ya mikataba mingine mbalimbali kama ya upangishaji na uendeshaji.

Kulingana na Katiba, Serikali ya Tanzania ilianzisha mkachato wa kuridhiwa na Bunge ili utekezaji wake uweze kuanza.

Mkataba huo umeweka vifungu muhimu kwa ajili ya kulinda maslahi ya Nchi ikiwemo ajira za Watanzania, ardhi ya Watanzania, ukomo wa mikataba, masuala yanulinzi na usalama na masuala mengine yote yenye umuhimu wa Nchi.

Mikataba hiyo pia itazingatia, kuweka bayana ukomo wautekelezaji, muda wa marejeo ya mkataba mwaka mmoja hadi mitano kutegemea na mkataba husika, viashiria vya utendaji wa mkataba, itakuwa chini ya ofisi ya Mwanasheria wa Serikali kwa kuzinagatia maslahi ya Taifa

Italinda wafanyakazi wazawa na kuwajenga uwezo, mifumo ya TEHAMA ya Kampuni ya DP World itasomana na ile ya Serikali.

Taasisi muhimu zote za Serikali zitaendelea na utekeleaji wake wa majukumu katika maeneo ya Bandari, mwekezaji atachukua hatua zote za Utafiti wa masoko ya Dar es Salaam.
Hii inawauma sana CHADEMA kuona Professor Mbarawa anavyohangaikia Nji yake waowanasema ni Mzanzibari si wao. As we speek wako EU kwa mabeberu nadhani watajarinu kumfitinisha lakini Bunge letu ni imara na ni Zalendo.
 
Kama ni kweli, Kwamba "wastani wa meli kusubiri Mombasa ni siku 1 na saa 6", kwa nini tusijifunze kwa hao Mombasa wanavyofanya vizuri hivyo ili na sisi tupate mafanikio hayo?
Mombasa kwani imeuzwa lini?


🙏🏻🙏🏻🙏🏻 💯% ✔
 
Hawa viongozi wa dini wataongeza au kupunguza nini katika huo mkataba?!
Wanataka kula ubwabwa tu hao.
Ungejua kwanza ni nani aliyeitisha hicho kikao ndipo ungeelewa maana ya kikao hicho.
Hawa watu wa dini sasa wanatafutwa ili watumike kupoza jamii, ambayo wengi wao ni washiriki wa hizo dini.
 
Mbarawa, umewaambia hao mapadre kwanini bandari na ardhi ya Zanzibar havimo Kwenye mkataba?
Vyote vimo katika mkataba huu, ni tundulissu ndiye aliyemdanganya Mbowe haraka haraka akakurupuka kuwa Zanzibar haimo eti akidai TPA ni ya Tanzania Bara tu kumbe ina mamlaka hadi Zanzibar. Aidha, Tundu alimpotosha Mbowe kuwa Professor Mbarawa hana madaraka Zanzibar kumbe anayo. Sasa Watanzania wote tunaanza kuona ni watu gani wako CHADEMA - wabinafsi, wabaguzi, waongo, walaghai.
 
Vyote vimo katika mkataba huu, ni tundulissu ndiye aliyemdanganya Mbowe haraka haraka akakurupuka kuwa Zanzibar haimo eti akidai TPA ni ya Tanzania Bara tu kumbe ina mamlaka hadi Zanzibar. Aidha, Tundu alimpotosha Mbowe kuwa Professor Mbarawa hana madaraka Zanzibar kumbe anayo. Sasa Watanzania wote tunaanza kuona ni watu gani wako CHADEMA - wabinafsi, wabaguzi, waongo, walaghai.
Shut up!
 
Ungejua kwanza ni nani aliyeitisha hicho kikao ndipo ungeelewa maana ya kikao hicho.
Hawa watu wa dini sasa wanatafutwa ili watumike kupoza jamii, ambayo wengi wao ni washiriki wa hizo dini.


Lazima Rais Samia ajue kwa swala hili la bandari kachemka vibaya na sio tu litamgharimu yeye pekee bali Chama chake kwa ujumla, wamezoea kutuona Watz ni mazuzu.

CCM siku moja ilitakiwa ianguke na suala la bandari litakuwa "a starting point" ya kuanguka kwake.
 
Ila siyo mapadre, ni viongozi wa dini kwa mujibu wa mleta mada.
Ila wasomi ni mapadre wengine ni elimu ya dini (madrasa), haya ya technicalities za higher mental powers hawayawezi (mnisamehe). (Hivi Mh. Mufti elimu yake ni kiwango gani?) sina nia ya kukejeli ni kutaka kujua namna wanavyoweza kudadavua mkataba ule na kuuelewa kisheria
 
Wewe ndio huelewi kitu. Eti agreement is not enforciable by law. Kasome definition ya Contract kwenye sheria za Tanzania. The Law of Contract Act RE 2019, section 2 a contract is any agreement enforciable by law. Wewe unatuambia agreement is not enforceable by law lakini sheria inatuambia Contract ni agreement enforceable by law. Tukusiklize wewe au sheria.
Not all agreements are contracts! However, a contract is also an agreement.

Hapa siongei kama layman, japo mimi siyo mwanasheria
 
Badala azungumze na wataalam wa sheria wamhoji maswali anazungumza na wazee wa dini wao na mikataba wapi na wapi. Hii nchi ina vituko kweli
Kwa mawazo Yako unafikiri mtu akiitwa padre au askofu basi atakuwa amesoma dini TU. Usije kusimama mbele ya maaskofu ukatamba na kadigrii Kako kamoja ka uchumi au kilimo utajua hujui.
 
Punguza upotoshaji. Eti kuuziana ng'ombe. Hayo uliyoandika ungeenda kumwambia spika Tulia wa bungeni aliyetuambia mkataba umeshasainiwa ndio maana umeletwa bungeni kupitishwa na Bunge ili iwe sheria ya kimataifa au tuseme iwe na binding force under international tribunals and courts. Acha kupotosha.
Unajua kwa sababu Mh Spika yeye ni a Lecturer by profession, inabidi awe anaanza Bunge kwa kutoa Lecuture kwanza kwa Watanzania, halafu hapo ndiyo tutaweza kumwelewa vizuri
 
Ila wasomi ni mapadre wengine ni elimu ya dini (madrasa), haya ya technicalities za higher mental powers hawayawezi (mnisamehe). (Hivi Mh. Mufti elimu yake ni kiwango gani?) sina nia ya kukejeli ni kutaka kujua namna wanavyoweza kudadavua mkataba ule na kuuelewa kisheria


Je, na hao mapadre nao wamesomea sheria ili waweze kujadili hizo technicalities za sheria za mikataba??.

Suala kubwa hapo ni morality, yaani wameenda kupewa somo la Morality (uzuri) kuhusu huo mkataba ili wakitoka hapo na wao waende kuwatuliza wafuasi wao (sisi wananchi).
 
Unajua kwa sababu Mh Spika yeye ni a Lecturer by profession, inabidi awe anaanza Bunge kwa kutoa Lecuture kwanza kwa Watanzania, halafu hapo ndiyo tutaweza kumwelewa vizuri


Huyo ni Lecture wa sheria asiyekuwa na moral authority ya cheo chake na elimu yake.

Unawezaje kuwakumbatia "wabunge" wasiokuwa na chama kuwemo ndani ya bunge??-- sio kuvunja sheria za nchi huko??.

Tulia haaminiki kabisa, huyo ni CCM stooge.
 
Back
Top Bottom