Wabunge waikataa ripoti ya Tume ya Mto Mara. Wataka iundwe tume huru

Wabunge waikataa ripoti ya Tume ya Mto Mara. Wataka iundwe tume huru

Proved unakwitwa huku sasa kimeumana. Profesa dhidi ya Profesa ukituambia tuheshimu taaluma.

Tuliheshimu taaluma siku zote tukiomba wenye meno waumane.

Hapa sasa menyewe kwa menyewe 😂😂.
Angalau prof mmoja kaamua kumuuma mwenzake...ila tusubiri ripoti nyingine ili tujiridhishe kabisa.
 
DKT.MUSUKUMA AJIUZULU

Mhe. Joseph Musukuma amejiuzulu nafasi yake ya ubalozi wa mazingira baada ya kutokuridhishwa kwake na ripoti ya uchafuzi mto Mara.Amelishauri bunge liikatae ripoti kwa sababu ni proffesorial rubish, "magugu Maji hayauwi samaki,wala hayazalishi mafuta"
Hivi hii ripoti ilishawekwa wazi ili watu waisome?

Mambo haya ya kisayansi kuyadakia juu juu tu bila kujua kilichoandikwa ndani yake siyo sawa. wanaweza kuishia

Kinachokuzwa sana ndani ya ripoti hiyo ni mikojo ya ng'ombe na mikojo, kwa sababu ni jambo la ajabu sana hili, lakini pengine kuna mambo mengine yaliyotajwa ndani ya ripoti ile yenye maana zaidi ya hii mikojo ya ng'ombe.

Ninapata taabu sana, na kwa kweli siamini kamwe, kwamba wasomi hawa wanaweza kuishia kwenye mikojo ya ng'ombe kuwa sababu ya kuua samaki . Hawa watakuwa ni ma-Profesa wa aina gani hawa!

Na itambulike pia, kwamba mto mara haupo mkoa wa Mara pekee, huu ni mto unaotokea nchi jirani, na huko kunafanyika mambo mengi yanayohusu mto huu pia.
 
Angalau prof mmoja kaamua kumuuma mwenzake...ila tusubiri ripoti nyingine ili tujiridhishe kabisa.

Nchi ngumu hii wakiita bongo nyoso:

IMG_20220405_163738_661.jpg

Mwendo wa kuingizana chaka baada ya chaka.
 
Baada ya kuwasilishwa bungeni leo ripoti ya Uchafuzi wa Mto Mara, wabunge wameikataa na kutaka kuundwe tume huru ya uchunguzi.

"Ripoti ya Kamati ya Kitaifa kuhusu Uchafuzi wa Mto Mara ina upotoshaji. Isiwekwe hata kwenye tovuti ya wizara. Hakuna mafuta Ziwa Victoria. Ikiwekwa kwenye tovuti, UNESCO watanishangaa mimi mtaalamu wa eneo hili," Prof. Muhongo.

Chanzo: Nipashe
Pia soma

Prof manyele amewaaibisha Wanazuoni.
 
Hahahaaaa........ Kazi imeanza.

Nilisema hapa bunge la chama kimoja huwa ni matata sana!
Bunge la Jamii Forum ndilo lililoikataa wao wanatafuta pa kutokea. Kuna mbunge wa kukataa ripoti ya seriakali hapo? Repoti ya Osollo ilikuwa hivihivi ulimsikia nani anasema No?
 
Kuna mafuta ziwani hapo hahahahaha

Ova
 
mliisha ambiwa ya kuwa 81% ya watanzania wapo vijijini. halafu karibia wote ni STD VII. Sasa huenda hii ripoti ikawa ni kwa ajili yao .
 
Yaani wanasiasa ni shida kweli,
Wanakataa ripoti ya wataalamu
Kwa mawazo na siasa tu
Kaaaazi kweli kweli
 
" Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake", ilisikika sauti ya chief akiwaambia wafuasi wake. suala ni Je nani atamfunga paka kengele???
 
tatizo hapa si kuchafuka kwa mto mara, ila wa Tanzania wengi mna majibu yenu ambayo tayari mmeisha yapigia mstari, haya basi kwanza andaeni data za uongo kama alivyo fanya jiwe kwenye makinikia, ndiyo mumtie hatian yuho 'mtuhumiwa' wenu, vinginevyo mtachezeshwa root reggae ……………..
Ukiwa na akili timamu ni kawaida kuwa na hisia. Ukiumwa unaweza kuhisi ni Malaria kutegemea movements zako.
Sasa wewe unategemea yaliyoandikwa na Tume yawe ni majawabu ya kisayansi? Au nawe ni msomi aina ya Manyere?
 
Inasemekana kapokea karibu 300 Milioni.
Kutoka serikalini yaani mgodi ule kwasasa serikali ndio mmiliki Mana ndo mwenye hisa asilimia 60 ,yaani serikali imemuhonga waziri wake .........umagufulification ndio ulipelekea hivyo Mana hiyo kuhusu mgodi ule serikali ndokila kitu

Ccm kiboko
 
Hahahaaaa........ Kazi imeanza.

Nilisema hapa bunge la chama kimoja huwa ni matata sana!
Hahaaa!!hakuna lolotee, hii hali inatokana na uhuru anaoutoa mh.rais, kwani kipindi cha awamu ya 5, nani alithibutu hata kukosoa?!!leo eti mbunge wa ccm anasema bunge kutoonyeshwa live, walikuwa gizani!!kitu ambacho kilikuwa ni dhabi, siasa za kiafrika bila unafika hutoboi!!!
 
Baada ya kuwasilishwa bungeni leo ripoti ya Uchafuzi wa Mto Mara, wabunge wameikataa na kutaka kuundwe tume huru ya uchunguzi.

"Ripoti ya Kamati ya Kitaifa kuhusu Uchafuzi wa Mto Mara ina upotoshaji. Isiwekwe hata kwenye tovuti ya wizara. Hakuna mafuta Ziwa Victoria. Ikiwekwa kwenye tovuti, UNESCO watanishangaa mimi mtaalamu wa eneo hili," Prof. Muhongo.

Chanzo: Nipashe
Pia soma

Hii ripoti tunaweza kuipata huku mitaani? Anayeweza kuipata, tunaomba aitume.
 
Hahaaa!!hakuna lolotee, hii hali inatokana na uhuru anaoutoa mh.rais, kwani kipindi cha awamu ya 5, nani alithibutu hata kukosoa?!!leo eti mbunge wa ccm anasema bunge kutoonyeshwa live, walikuwa gizani!!kitu ambacho kilikuwa ni dhabi, siasa za kiafrika bila unafika hutoboi!!!
Kwani huyo Nape leo alikuwa na akili ya nani tofauti na wakati ule?
 
Back
Top Bottom